Sunday, January 6, 2013

WAJIBU WAKO MWALIMU

song.....wajibu wako mwalimu

1Elimu kutupatia,
 maharifa kuyasikia,
 ujuzi kuufikia,
 wajibu wako mwalimu.

2Darasani kuingia,
 ujinga kuufagia,
 wanafunzi tupe njia,
 wajibu wako mwalimu.

3Zarau na majigmbo,
 vipe nafasi ya fimbo,
 uvumilivu uwe wimbo,
 wajibu wako mwalimu.

4Mshika mbili ponyoka,
 kutanga tanga wataka,
 angalia unavyo choka,
 wajibu wako mwalimu.

5Elimu haina mwisho,
 uvivu upe hitimisho,
 mwendo huo rekebisho,
 wajibu wako mwalimu .

No comments:

Post a Comment