Thursday, November 26, 2015

 
JAMANI NIFARIJINI
Ninaanza kwa huzuni,yale yaliyonikuta,
Sio kwamba niutani,ni kweli yamenipata,
Nilimpenda jamani,mpenzi wangu matata,
Mpenzi wangu amekufa,jamani nifarijini.
 
Tuliishi kwa amani,bila ya korofishana,
Nami nilimuamini,nikamuweka bayana,
Wengine kaweka chini,nikabaki nae bwana,
Mpenzi wangu amekufa,jamani nifarijini.
 
Tuliyapanga vizuri,mambo yetu bila keke,
Akalipa na mahari,ili niwe wake mke,
Mambo yalikua shwari tena bila ya makeke,
Mpenzi wangu amekufa,jamani nifarijini.
 
Wazazi walitambua,jinsi tulivyopendana,
Wakatupa na usia,kwetu sisi waungwana,
Usia tulipokea,dua tukaombeana,
Mpenzi wangu amekufa,jamani nifarijini.
 
Harusi ilipowadia,watu wakakusanyika,
Wengi wakafurahia,nami nikaunganika,
Sikua nayo furaha,kwani wangu hakufika,
Mpenzi wangu amekufa jamaninifarijini,
 
Ikatufika khabari,kipenzi amenitoka,
Kamwe sikua tayari tendo hilo kunifika,
Niliiyona bahari,kwa mbali yanizunguka,
Mpenzi wangu amekufa jamani nifarijini.
 
Ghafra nikaona kiza,chanijia mbele yangu,
kutwa kucha najiliza,sina mfariji wangu,
jamani nimepoteza,aliyekua wa kwangu,
mpenzi wangu amekufa,jamani nifarijini.
 
PENZI ULILONIPATIA
 
         Penzi ulonipatia,penzi uloniachia,
         Utamu linifikia,daima najivunia,
         Raha zilivonijia,nikatamani enderia,
         Penzi ulonipatia.
 
         Hakika nilijilamba,lipoondoa ushamba,
         Ukanifungua kamba,mapambo ukanipamba,
         Najivuna najigamba,we binti usojilemba,
         Penzi uliloniachia,
                                                                                                 
         Ingawaje siku tatu,siku lizonipa vitu,
         Siwezi sahau katu,ewe binti wa kibantu,
         kweli sikushindi kitu,nawatangazia watu,
         Utamu linifikia.
 
         Hapa ukijinilamba,pale nikukutenda
         Hapa ukijinipumba,pale huwezi kwenda,
         Hata watu wa kipemba,watakusifu kunipenda,
         Daima lijivunia.
 
         Hisia zangu moyoni,kumbe unavyozijua,
         Nipokutizama soni,kama unaomba dua,
         Kileleni kufikia,na mimi ninapumua,
         Raha  nika kumwagia,   
 
NAKUPENDA MPENZI
             Wewe ndio langu jua, kizani umenitoa,
             Dia nimekuchagua,kwenye hii dunia
             Kwako tuli metulia,Wanichombeza kwa penzi,
             zuri ka tamthilia,Nakupenda mpendwa,
             Nakupenda mpendwa,pasi na kufikiria
 
             Mpenzi wangu nilinde,Mbali sana nisiende,
             Tena pia unipende,Usinifanye nikonde,
             Nakupenda mpendwa,pasi na kufikiria,
             Nakupenda mpendwa,pasina kufikiria,
             Nakupenda mpendwa,pasinakufikiria.
 
             Kila baya kila zuri,Na kwako ulipende,
             silifanye mauwende,utanifanya nikonde,
             Mpendwa unilinde,mbali sana usiende,
             Nakupenda mpendwa, pasi na kufikiria.
             Nakupenda mpendwa,pasina kufikiria.
 
            Mpenzi wangu nilinde,kwengineko nisiende,
            Usifanye nijutie,Nijutie  ulimwende,
            Kwako tuli metulia,Kwa mwingine nisende,
            Nakupenda mpendwa,pasi na kufikiria,
            Nakupenda mpendwa,pasina kufikiria.
 
 
           Unilinde mpendwa,mbali sana nisiende
           Kwako tuli metulia,kwa mwingine nisiende
          Nakupenda mpendwa,Nakupenda  kwa gwaride
          Tena ikiweza kana,Na wewe pia unipende
           Nakupenda mpendwa, pasina kufikiria
 
           Nipende mpendwa,Usinifanye nikonde
           Usinifanye nijutie,Nijutie ulimbwende
           Unipende mpendwa,Mbali sana nisiende
           Ukiwa kimya mpendwa,Utanifanya nikonde
           Nakupenda mpendwa,pasina kufikiria
 
           Nakupenda mpendwa,kwa mwingine nisiende,
           Usimuone mwalimu,Ukataka uumpende,
           Haujui halitakalo,kwake ni ulimbwende,
           Kwa wengine usiende,wa kwako nikupende,
           Nakupenda mpendwa, pasi na kufikiria.
 
ANAPENDA  KUOLEWA
 
Mawazo yake  dada ngu,anawaza kuolewa,
Ajikalie kwa chungu,moto wake kuchochewa,
Aoshe viombo  chungu,na sabuni atapewa,
Anawaza kuolewa,Anawaza dada yangu.
 
Atamania kuzaa,ajivunie  watoto,
Kamwe hawezi kata,autunze ujauzito,
Na dunia yashangaa,kulea kutunza wito,
Aolewe dada yangu,anawaza dada yangu.
 
Anatamani mapenzi,kitu hicho matatuzi,
Kinompa gugumizi,yu mpweke hana buzi,
Aibu kitu kishenzi,kiletacho uchokozi,
Chamnyima mume dada,anawaza dada yangu
 
Enyi vijana tulivu,namleta kwenu dada,
Wa mwenendo mkamavu,sanda kalawe kushinda,
Onesheni uangavu,kimpata tampenda
Ofa malumu naleta,anapenda kuolewa
 
Mwanaume na mwanamke,ndio nguzo ya umoja,
Wito mikono  tushike,tushikamane pamoja,
Ujasiri tujivike,familia kujengia,
Majukumu tujitwike,anapenda kuolewa
 
Ofa malumu naleta,wajunzi twanga pepeta,
Chelewaye sijejuta,sinambie sikupata,
Naogopa mi kusutwa,habari hiyo ni nyota,
Atakaye ameshinda,anawaza dada yangu.
 
Dada mwenyewe kigori,bikira ni mwanamwari,
Mrembo huyo mdori,mchapa kazi kijori,
Sura na rangi mzuri,msomi wa seKondari,
Elimu yake nasema,anawaza kuolewa.
 
Mwenyezi mungu kaumba,urembo nao kapamba,
Pendo jema si kasumba,namtangaza mchumba,
Tabia meitambua,mchapa kazi najua,
Sababu ni dada yangu,anawaza kuolewa.
 
Mfupi si mbilikimo,rangi yake kahawia,
Mashavuni na vishimo,nyuma tako katupia,
Hapaki tope domoni,nywereze ujisukia
Ni mrembo wa asilia,anapenda kuolewa
 
Hapatikani Asia,Hapatikani Ameika,
Zunguka zungu dunia,pande zote Afirika,
Watu wa kitanzania,binti huyo kaumbika,
kimpata taniambia,anapenda kuolewa
 
Hataki kuja chezewa,anataka kupepewa,
Ndoa ikishafungiwa,baraka mkigawiwa,
Muishi kivumiliwa,penye shida kutatuwa,
Mume na mke pamoja,mujeishi kwa umoja.
 
JAPO NIKUONJE KISHA NIKUACHE.
toto zuri  mwanayamara,mekuona mependeza,
Safari yako  mbagara,ninakuomba geuza,
Mwendo  nazako ishara,moyo wangu ukipoza
Simama nikueleze,moyo wangu usikwaze
 
mevutiwa na madaha,maringo yako we dada,
toto zuri ye jaziha,hakuna mwingine  Dar
fungua moyo paziha,uzuri wako my dia
Nikwite majina yote,sweet wangu malikia.
 
Nimesikia dunia,pesa ndio yaongea,
mifuko livyojazia,taratibu wasogea,
twende ukanitumia,mwanadada naongea,
Pesa  nguvu ya dunia,kwa maneno na vitendo.
 
Buzi lako unichune,kwa mishikaki na chipsi,
Pesa ni makaratasi,nipe radhi  mezitusi,
Kunywa mtoto  upesi,pata raha za ukwasi,
mimi  nimeshakupenda,nani mwingine…..? hakuna.
 
Kula mtoto kunywa bia,nipapase nishalewa,
Cheza we cheza sikia,ile michezo  kikubwa,
watu watakusikia,punguza ninapagawa,
OOOhsh!! OOOhsh!! , jamani nahisi raha.
 
Nikutumie kwa muda,kisha nikuache zako,
Mi nimevikwa shahada,sina mengi malamiko,
Nikimpenda mwanadada,wala sipati sumbuko,
Ndivyo dunia mejua,sitarehe ni gharama.
 
Siulize we wangapi?,wengi nimewatumia,
Siulize mepatapi?,pesa inawavutia
Hata kama mi mfupi,na nisiyewavutia,
pesa maisha mafupi,ndiyo inajisemea,
 
Hujui nipo salama,au sijawa imara,
Kinga haina maana,kwangu kizee kipara,
Dunia ninayojua,kutumia kutawara,
Wadhaifu chini jua,hunifuata hatua.
 
Tamati naondokia,asubuhi pambazuka,
Mifuko imenishia,sina pa kupumzika,
Chumvi nimeshajilia,familia sikujaliwa,
Sababu ya sitarehe,nakulala hotelini.
 
 NAKUPENDA WEWE KAKA
 
         Nakupenda wewe kaka,moyoni umeshatua,
         Yani kwako nimefika,sitaki kukuachia,
         Wasije hao vibaka,mpenzi kukuchukua,
         Nakupenda wewe kaka,mimi kwako nimefika.
 
         Yaani meona wengi,katika hii dunia,
         Katika sehemu nyingi,hakuna wakukufikia,
         Yani wewe ndio kingi,na mimi ndo malikia,
         Nakupenda wewe kaka,mimi kwako naumia.
 
         Nakupenda tena sana,mpenzi nakuzimia,
         Waogope wasichana,tena mbali wapitia,
         Hata  wenye hela sana,magari na nyumba pia,
         Nakupenda wewe kaka,mimi kwako nimefika.
 
         Kila ninapokuona moyo wangu wasituka
         Ukweli nataka nena,na siwezi kulopoka,
         Mungu atupe neema,na pingu tukajivika,
         Nakupenda wewe kaka,mimi kwako naumia.
 
         Karibu tufunge ndoa,wewe ndo wangu mpenzi,                           
         Kamwe sitakuondoa,kwa kukuletea ushenzi,
         Siwezi kujipodoa,ili kuzidisha penzi,
         Nakupenda wewe kaka,mimi kwako nimefika
 
         Nakupenda kwa moyo wote,kila mtu anajua,
         Nitakufata popote,ili usije kimbia,
         Na mbali nisikutupe,mashosti wakakujia,
         Nakupenda wewe kaka,mimi kwako naumia.
 
         Na ukweli ndio huo,hata roho zikiuma,
         Wapendao michepuo,Tayari wameshanuna,
         Hataki za mipasuo,hata zile za kubana,
         Nakupenda wewe kaka,mimi kwako nimefika
 
       .WAWILI  TUNAPENDANA
 
            Wawili tunapendana,kama mnavyotuona,
            Katu hatuta achana,tumeshapendana sana,
            Umizeni vyenu vichwa,kwa maneno na umbea,
            Wawili tunapendana,wala msitujadili,
 
            Kila siku twafurahi,Amani tele nyumbani,
            Kila muda twafurahi,wala hakuna huzuni,
            Pamoja tukifurahi,watu huwa na huzuni,
            Wawili tunapendana,wala msitujadili.
 
            Sisi tunavyopendana,jama hamna kifani,
            Tena twashirikiana,na sote tunafurahi,
            Sisi tunapokutana,kwa mapenzi twajidai,
            Wawili tunapendana,wala msitujadili,
 
            Tukiwa mepumzika,pamoja tukifurahi,
            Tena watu waudhika,pale tunapojidai,
            Tena wana hangaika,kulivunja kwa jinai,
            Wawili tunapendana,wala msitujadili.
 
            Pendo letu twalitunza,kamwe lisiharibike,
            Hata walitie funza,ili lije haribike,
            Pamoja tunalitunza,kamwe lisiharibike,
            Wawili tunapendana,wala msitujadili.
 
.KWANZA WEWE NI FATAKI.
Nimeona maajabu,nikashindwa kua bubu,
Tena watia aibu,na mandevu kama babu,
Kwanza wewe ni fataki,wanitaka sikutaki.
 
Watoto unawataka,muda mwingine wabaka,
Kwa vipesa vya haraka,wasiweze kubanduka,
Kwanza wewe ni fataki wanitaka sikutaki.
 
Sikutaki babu wewe,huna budi utambuwe,
Haunitii kiwewe,moyoni mwako nitowe,
Kwanza wewe ni fataki,wanitaka sikutaki.
 
Sinifanye nizomewe,kwa kutembea na wewe,
Wakaniona ni mwewe,yakupasa utambuwe,
Kwanza wewe ni fataki,wanitaka sikutaki.
 
Hupendi kushughurika,na watu walo zeeka,
Watoto unawataka,matatizo wawaweka.
Kwanza wewe ni fataki,wanitaka sikutaki.
 
Kwa kiburi unatesa,ati wewe wa kisasa,
Kwa kujitapa na pesa watoto kuja wanasa,
Kwanza wewe ni fataki wanitaka sikutaki.
 
Achana na udhaifu,jiepushe na uchafu,
Jivike uadilifu,uje pata utukufu,
Kwanza wewe ni fataki,wanitaka sikutaki.
 
FUNGASHA VIRAGO VYAKO.
Nimeoa maajabu,
Unanitia aibu,
Umekosa ustarabu,
Fungasha virago vyako,
Bibie urudi kwenu.
 
Si vuli sio masika,Ukaa kaeleweka,Mwenye nyingi pilika,
Fungasha virago vyako,Bibie urudi kwenu.
 
Usiye jua kupika,
Hamu yote yanitoka,
Kufikia kutapika,
Fungasha virago vyako,
Bibie urudi kwenu.
 
Usoni kujichubua,kujifanya unajua,kumbe waugua jua
Fungasha virago vyako,bibie urudi kwenu.
 
Kwa kiburi unatesa,
kujiona wakisasa,
na magonjwa ushanasa
fungasha virago vyako,
bibie urudi kwenu.
 
Mwanamke so wajibika,kutwa kucha kuzunguka,taraka umeitaka
Fungasha virago vyako,bibie urudi kwenu.
 
wajua kubabaisha,
Virago vyako fungasha,
Uage hayo maisha,
Fungasha virago vyako,
Bibie urudi kwenu.
 
PENZI LAKO NIMELEWA.
Mapenzi umenifunza,na vema ukanitunza,jinsi ya kuniliwaza,waelewa unaweza,
Penzi lako nimelewa.
 
Mzigo kwako sioni,unayaweza koteni,chumbani ata jikoni,alo kuumba shukurani,
Penzi lako nimelewa.
 
Penzi tamu kama nini?,cha kufananisha sioni,sijui nikwite nani?penzi lisilo mpinzani,
Penzi lako nimelewa.
 
Tamu tamu tena tamu,kamwe sihishiwi hamu,wajua mashamu shamu,mpenzi wangu muhimu.penzi lako nimelewa.
 
Penzi lako nasifia,penzi lako lavutia,ukiwa mbali nukia,utatatani kunitia,
Penzi  lako nimelewa.
 
Mpenzi hupendi mali,kwako umeka mbali,ninakupenda chakali,nipende tufike mbali,
Penzi lako nimelewa.
 
 
Wala sita sema basi,na hayatanighasi ghasi,kwako sina wasi wasi,moyoni una nafasi,
Penzi lako nimelewa

No comments:

Post a Comment