SEHEMU YA PILI
Siku iliyofuata boga akamwambia
dady anaenda kwenye mashindano talent show,dady hakua na kinyongo akamkubalia
mwanawe na pia alipomwona pamera alifurahi sana kwani pamera alikua ni binti
mchangamfu na Mwenye furaha na pia alikosa aibu kabisa,pamera na boga wakaenda
mwenge pamera akiwa amemshika boga mkono
wakayacheki majina yao kwenye notice board kwa bahati nzuri wote wawili
walibahatika kuingia kwenye yale mashindano,walichaguliwa vijana therathini.
Vijana wote wakatambulishwa kwa hadhira iliyokuwepo pale kwenye
hall,msemaji mkuu au msema chochote wa siku hiyo alikua ni Mc maharufu kwa
vitimbwi vichekesho pamoja na vituko vya hapa na pale MASANJA MKANDAMIZAJI Pamoja na mchezesha music almaharufu kwa jina
la DJ CHOKA .Lakini pia ukumbi ulipambwa na vifaa vya kimuzic kama vile
magitaa,matarumbeta,vinanda,violin,ngoma za asili na vifaa vingine vingine
vingi bila kusahau microphone pamoja na speeker kwa ajili ya kutole na kuingizia sauti.
Yalizaliwa makundi sita kila kundi liliwabeba vijana watano watano
kundi la kwanza liliitwa HARDER TO TOUCH, kundi ili liliwabebavijana wa kiume
watatu na wa kike wawili majina yao
waliitwa MIZANI,KINOMANOMA,GODZILLA,MAMAJUSI,na RWANDAI. Kundi la pili liliitwa WAKARI CLASSICS kundi ili liliwabeba vijana
kama vile BENITOTO,ALL DAYZ CONFIDENCE,NAIROBI,YOUNG MBARA, na ELIA ABELIA.
Kundi lao liliwabebe vijana wote wa kiume.Kundi la tatu lililoitwa LAZIMA TUSHINDE liliwakusanya vijana kama
vile MALIPO MARIBORO,LERATO,PANDA HILL,MAMA SILVANO, na ANDUNJE,
Kundi la SISI NI BALAA
liliwazoa wasanii wake majina yao ni
JOHSON JOHN,SISTER ABELLA,ADAMSON ,NEEMA MWAKYUSA na DIANA NYOKS, achilia mbali
majina ya kundi hili kundi la tano lililoitwa SIMBA DUMEZ NA SIMBA JIKEZ
liliwakusanya wajanja wake kama vile IRENE POO,GOD LISTEN PETER JOSEPH,SABA
SABA,NDANDA NGABI na SHAA DIANA ROZE, kikundi cha mwisho wao walijipa jina
la HAMTUWEZI hawa walijipanga vizuri kwa majina yao kama vile PAMERA,BOGA
TALENTER,POMONI DIA,COMMOROW na LOSHORO
Mc masanja mkandamizaji akawaambia kuwa wote pale hawapo kuuza sura
zao(kujionesha tu) ila wapo palekuonesha vipaji vyao vya hali ya juu,uwezo
ubunifu juhudi pamoja na kujituma kwao ili waweze kushinda mamilioni ya
shilingi na kuitangaza vizuri ramani ya
nchi yetu kimataifa.Wote walitakiwa kushiriki au kushirikiana katika
categorization mbali mbali zikiwemo
1.MAPISHI YA VYAKULA
VYA AINA MBALIMBALI
2.UFUNDI WA KUBUNI MAVAZI YA AINA MBALI MBALI(fashion show moder)
3.MAIGIZO
4.KURUKA KAMBA
5.KUOGELEA
6.MUZIC(kuimba,kucheza,kutunga na kushirikiana katika performance)
7.UBUNIFU KATIKA UCHORAJI
8.UREMBO NA UTANASHATI
9.USAFI KWA UJUMLA
10.KUKIMBIZA BAISKERI KWA MIGUU
11.KUVUTA KAMBA
12.MPIRA
13 KUKIMBIA,.KUKIMBIZA
KUKU, KULA NA KUNYWA
14.UBUNIFU
WA KUJIBU MASWALI KWA LUGHA YA KIINGEREZA
15. MAZOEZI YA
VIUNGO NA MAPAMBANO
MAPISHI
Siku ile vijana walipewa kazi moja tu ya kuandaa mapishi ya aina mbalimbali kila aina ya vyakula
ililetwa hapakukosekana aina yoyote ya chakula kwani hata wasivyovijua
vililetwa mbele yao vikiambatana na viungo mbalimbali vya hayo mapishi bila
kusahau mafuta chumvi,au sukari ili kufanya vyakula viwe vitamu.Zikaletwa mbele
yao
cabbage,Chinese,spinach,carrot,matango,spagget,unga wa kupikia vyakula
vya aina mbali mbali ikiwemo ugali na mikate ya ngano,samaki.mchele, nyama ya
kuku ya nguruwe ya mbuzi ya bata, dagaa,sukuma wiki, mnafu,ngogwe,njegere,kunde
bamia,na vinginevyo vingi pasipo kusahau matunda. Sasa kazi ikaanza kila mtu
aliitaji kushiriki vizuri ili kuleta mvuto wa kazi ile.Wakapewa mavazi maharumu
kama yale ya wapishi wa mahoteini nao wakajivika vema wakaonekana kama wapishi haswa.
Sheria iliyowekwa ilikua ni kwamba iwapo kundi moja limeshindwa kufanya
vizuri au makundi yote yameshindwa kufanya vema kwenye yale mashindano basi
watu wote wakundi au makundi husika walitakiwa kufungasha virago na kutokomea
kurundi Nyumbani kwao.
Kundi la Harder to touch kama walivyopenda kujikita wenyewe YOU NEVER TOUCH US,lilikua ni kundi la vijana
wachangamfu,wacheshi,wapole na pia vijana wenye matumaini sana ya kushinda kwa
swagga zao hata siku ya kwanza kupanda jukwani hadhira iliwshangilia mno
wakijipa matumaini ya ya kwamba ushindi ni wao hakuna wa kuwazidi na watashinda
kwa kishindo kikuu cha kushitukiza.
Haraka haraka wakapata wazo kuwa waandae mlo unaoitwa LOSHORO,pishi la
kabilala watu wa kaskazini mwa Tanzania maharufu kama wameru wa Arusha. Wao
walichofanya walichukua ndizi ambazo hazijaiva yaani matokii,wakaumenya mkungu
mzima wa zile ndizi za matokii kisha wakazikata kazikata vipande vipande baada
ya kuzichemsha ndizi zile wakakata nyama vipande vipande nazo
wakazichemsha,wakachukua mahindi ya kukobolewa nayo wakayachemsha vizuri vyote
vikawa vinatokota tokota na kutoa harufu
nzuri ya utamu na unono na baada ya kuona kuwa pishi limeivaa
wakachanganya na maziwa
mgando,ila walipenda sana kutia maziwa fresh lakini ilikua nichaguo lao wenyewe……….kwanza kabisa waliziponda ponda
zile ndizi zikawa uji uji na kisha `wakachanganya na nyama bila kusahau yale
maziwa pamoja na makande pishi likaendelea kutoa unono.Hakika lile pishi
lilikua ni pishi bomba kisawa sawa ingawaje walisahau kutia chumvi ilo nalo
likawa kosa lao kubwa sana.
Pishi la pili walilolizimia kulipika lilikua ni pishi la chapatti
maharagwe,chai nzuri ya maziwa freshi ikatengenezwa maziwa mazito ya moto moto
yakachemshwa chapatti tamu aina ya chapatti kavu zikapikwa pamoja na maharagwe
yalikaangwa vizuri.Upungufu wao ni kwamba walisahau kutia kiungo mahalumu
kiitwacho nyanya ingawaje mafuta ya
kula,pilipili hoho,caroot pamoja na vitunguu viliwekwa vizuri.mbali na ilo
pishi pia chai yao ilikosa sukari jambo
ambalo wao wenyewe kama kundi walisahau kutia sukari.
Pishi la mwisho walilolipika lilikua ni pishi la ndizi za kukangaa zilizotiwa asali,chips
mayai,viazi mbatata vya kukaangwavilivyotiwa pilipili,baada ya kumalizia
mapishi yao wakayaifadhi mahari pazuri kisha wakapewa ruhusa ya kuondoka ili
kupisha kundi la pili nalo lioneshe mahanjumati yake,kwani hadhira ilivutiwa
sana na juhudi pamoja na ujuzi ambao kundi la
HARDER TO TOUCH liliuonesha.
Likapewa
nafasi kundi matata na kundi machachari la la WAKARI CLASSICSS ingawaje ndani
ya kikundi hiki walikuwemo baadhi ya vijana wenye tabia chafu kama vile unywaji
pombe kupita kiasi,uzinifu ,kutukanana matusi ya nguoni,kupigana na pia
kuibiana vitu,lakini vijana walikua wapo super wapo juu katika kujituma na pia
kufanya maujanja ya hapa na pale.Walijinadi kua wao ni wakari na hakuna mtu wa
kuwazingua,kwani wanaweza kuliambia jua simama nalo likasimama,wanaweza
kuliambia jiwe badirika uwe mkate nalo jiwe likabadirika,bahari iwe chumvi nayo
inakua chumvi,nyoka awe samaki naye akawa samaki.Walijigamba na kujinadi sana
hadi hadhira ilipasuka mbavu kwa vicheko mfululizo.
Wao
walikubaliana kuandaa UGALI WA MAZIWA FRESH YA MOTO,ugali ukapikwa kwa kutumia
unga wa dona na maziwa fresh yakachemshwa.pishi la pili lilikua ni mboga mboga wao walichofanya ni
kutengeneza cabbage ya kuchemsha na kutia aina zote za viungo, mchuzi wake
wakauweka pembeni na walipoulizwa mchuzi wa cabbage una saidia nini mwilini
jibu walilo litoa ni kuwa mchuzi ule ni mzuri sana kwa kupunguza mafuta na unene mwilini.
Walipomaliza
hiyo shughuri pevu pishi lililofuata
lilikua ni mayai , mayai haya waliyagawa katika makundi matatu kundi la
kwanza lilikua ni mayai ya kuchemsha
wakatengeneza na chai ya maziwa wao walisema kuwa mayai ya kuchemsha
pamoja na maziwa usaidia kupunguza unene mwilini.
Lakini
walipopika mayai yaliyochanganywa na vitunguu,carrot, pamoja na vipande vya
hoho walidai kuwa haya ni mazuri kwa ajiri ya kunenepesha mwili na kuupa mwili
nguvu pamoja na akili. Wakamalizia kwa kupika mayai yaliyo changanywa na carrot
nyanya na hoho ,vitunguu pamoja na
samaki watatu waliokaangwa kisha mapishi ya kuchanganya changanya vile vitamu
tamu yakaanza.shughuri ile pevu ilipoisha walivitandaza vyakula vyao vitamu
mezani ili hadhira ipate kuonja kunusa nusa ,kububuna,kukodorea macho,
kuvitamani na kujifunza zaidi kutoka kwao kwa kutumia maswali na majibu juu ya
utundu na utaalamu wao katika mapishi.
Kundi
la tatu la LAZIMA TUSHINDE na KUNDI LA SISI NI BALAA ambalo ni kundi la nne wakaitwa wote kwa
pamoja ili kuonesha hadhira manjonjonjo na mautundu ambayo mwenyezi Mungu
amewajalia hawakua na makuu sana upole
busara wema na kujituma ndiyo ilikua sifa yao njema.Walianza na uhandaaji wa
juisi ya matunda,hatua ya kwanza waliyoichukua ilikua ni kutafuta
maembe,maparachichi,machungwa,maboora
mapapai,mananasi,na
matunda mengineyo mengi ya shambani kisha wote kwa pamoja wakayamenya vizuri
tena kwa wingi utadhania mchango wa baharini na hatua ya tatu ilikua ni
kuyasaga kwa kutumia mashine maharumu ya kusagia matunda kwenye jagi, na hatua
ya mwisho ilikua ni kuyaifadhi yale matunda kwenye chombo maalumu kila spice ya
matunda kwenye chombo chake na mahari pake.
Pishi
la pili lilikua ni pishi la uji(stiff polidige)uji mzito ulitengenezwa,uji
uliochanganywa na maziwa freshi mazito ya ngombe ,ukitegemea walitumia utundu
na ufundi wao kwa kuchanganya blue band,karanga, mahindi,njegere choroko mtama
ulezi,maharagwe ya soya, mchere na ngano.kwa pamoja vilisagwa vizuri
vikachanganywa changanywa uji mzito uliotiwa sukari ya kutosha uliwekwa tayari
kwa ajiri ya mywaji.
Wakamalizia kwa kupika pishi bomba haswa wala
sio lingine bali ni pishi la la supu
ya mafuta mafuta ya ngombe yalochanganywa
na nyama kadha za mbuzi, wakapaliliza na nyama ya kondoo si mchezo kwani
hawakusahau nyama ya kikanda cha nguruwe,kweli mtu ni afya na ni lazima ale
vyakula bora.
Likaitwa
kundi la tano kundi la SIMBA DUMEZI NA
SIMBA JIKEZI ,vijana hawa hata ukiwaangalia hakika usingesita kujisemea hawana
mpizani,vijana walijariwa urembo na utanashati na pia nguvu zao za kuchapa kazi
zilikua hazihesabiki ,ndio maana
wakajiita simba dumezi na simba jikezi, maringo ndio ilikua sifa mahususi ya
kundi hili, waka yavunja moyo
makundi mengine lakini ukweli ni kwamba asokubali kushindwa si mshindani.
Nyama
ya kuku ikaandaliwa,wakai rostisha ile nyama.Nyama ya ngombe ikaandaliwa
mchemsho safi sana,nyama ya mbuzi ikaandaliwa mishikaki bomba haswa na pia
nyama ya kondoo ikapikwa vizuri vizuri kwa kutumia viungo vitamu vitamu bila
kusahau pishi bomba la dagaa wa ziwa Victoria dagaa wanene na tena wenye afya
kama mlima Kilimanjaro.
Pishi
la pili lilikua ni pishi la mboga za
majani wakajiandalia Chinese safi ya kukaanga kwa mafuta tu,wakakata kata mnafu
na kuchanganya pamoja na ngogwe,ingawaje vyakula hivi ni vikari lakini walitumia
utaalamua wa hali ya juu kuviandaa ili kuhakikisha ya kwamba pishi lao halina
dosari yoyote ya ukari,achilia mbali pishi lao la mboga mboga kama vile mchicha,
mrenda waliotia bamia magadi maharagwe pamoja na mboga mboga za majani,pamoja
na hayo yote walipika njegere kavu choroko kavu na kunde kavu……..ama kweli
vyakula bora ni dawa kwani ushindani ulikua ni mkari.
Na
pishi walilolimalizia lilikua ni utengenezaji wa matunda. Matunda yao yalikua
ni mchanganyiko wa vipande vipande vya carrot,maembe,hoho,nyanya,vitunguu,ndizi
za kuiva,matikiti maji,rimon,matango,maparachichi,matunda damu, na maembe
baadhi ya matunda waliyachanganya changanya na na mengine waliyakata kata hivyo
hivyo tu na kuyaifadhi kwenye vyombo maalumu safi.
Hakika
hadhira ilifurahishwa sana na juhudi nguvu na uwezo wa kubuni mambo mazuri ya
jikoni yaliyofanywa na kundi hili watu wengi sana waliwapigia makofi na
kuwapatia kura nyingi sana kundi la SIMBA JIKEZI NA SIMBA DUMEZ,wali wapooza
kwa kuwaambia maneno mataamu ya kuwatoa nyoka mapangoni kwamba ushindi ni wao
bahati yao imegonga mlangoni wala wasiiache ikapita na kwenda zake.
Kundi
la mwisho ambalo ndilo alilokuwepo boga talenter pamoja na
pamera,lililojurikana kwa jina la HAMTUWEZI wakapita ukumbini kama vile rocket
iendayo kwa kasi ya mkorea,hawakua na haja ya kupita kama vile vinyonga wenye
njaa,ingawaje hawakuleta mvuto kwa hadhira ile kundi ili lilijaa vijana wenye
aibu na soni ila tu baadhi yao walikua super
wana nyota za mvuto.
Walichofanya
wao kama kundi walikubaliana kuandaa
chakula cha jioni kwanza. Pilau iliyo sheheheni
viazi mviringo pamoja na nyama nzito ya bata mzinga pamoja na kuku aina
ya kanga zilipikwa vikanukia sana hadi
hadhira ikaanza kumezea mate harufu tu ilitosha kushibisha ile hadhira.
Walipomaliza shughuri ile wakaunganisha na wali mweupe uliotiwa
nazi,carrot,maharagwe na pia wakakoleza kwa kutia asali iliyoogeza utamu hadi
kwenye visogo vya hadhira.
Pishi
la pili lilikua ni pishi la spagget au
kwa jina lingine tambi hapa napo waliwashangaza watu kwa maajabu yao makuu
waliyo ya fanya kwani watu wengi sana hawakujua jinsi ya kupika spagett sasa
siku ile waliamini kuwa duniani kuna
watu wataalamu na wajuzi wa mapishi.Kwanza spagget au tambi zikakatwa katwa vipande
kisha zikatiwa kwenye maziwa yaliyokua yanachemka baada ya kuiva zikakaangwa
kwenye mafuta na baada ya shughuri ile pevu spagget zikawekwa karrot zilizo
sagwa vizuri pamoja na vitunguu na baada ya pishi ilo tamu likapalilizwa kwa
mboga mboga za majani juu yake wakaweka maua yalonukia na kuvutia.
Walipolimaliza
ilo pishi safari hii wakaunganisha na pishi la vitafunwa vya staftahi hapa
washiriki wakalipa jina ili pishi siku njema ionekayo asubuhi,wakachanganya
unga wa bakery kidogo wakatia na unga wa ngano,keki ilotiwa chocollate
ikaandaliwa,mkate mtamu wa ngano sijui wanaita BUMUNDA likapikwa, maandazi aina
ya donate yakawekwa pale mezani,vipande vya bisscut na karanga za
kukaangwa zikawekwa kwenye sahani ndogo
ndogo ziitwazo visosa.Hawakusahau kutengeneza chai ya maziwa,ya rangi, ya
kahawa naya cocoa.
Wakapewa
tena nafasi ya kuandaa pishi la mwisho
hawakua nyuma katika kuandaa pilipili ya kiutamaduni wao waliipachika jina
la traditionar peeper hii ndio pilipili
inayotengenezwa kwa kusaga nyanya kwa
kutumia mashine maharumu ya kusagia,mpaka nyanya zinakua kama maji
maji,wakachanganya pilipili iliyoitwa pilipili mbuzi kisha wakachanganya na
pilipili moja kari kwa jina la pili pili
kichaa.
Amakweli
kazi ya mapishi ni kazi ngumu sana zio kazi ya kuwaachia wanawake tu
waishughurikie wakiwa Nyumbani bali ni kazi inayoitaji ushirikiano kati ya
mwanaume na mwanamke,kwani umoja ni nguvu utengano ni udhaifu,zoezi ili gumu
utadhania watu wana ng’oa mlima Kilimanjaro kwa mikono yao likaisha vizuri
sana.
Msemachocote(Mc)wa
siku ile ndugu Masanja Mkandamizaji aliwapongeza sana washiriki wote kwa jinsi
walivyoonesha
juhudi
zao,nguvu ushirikiano pamoja na uwezo wa kiubunifu kwani utaalamu walo uonesha
ulitosha kudhihirisha kuwa wapo juu
kinoma.pia aliwapa pole kwa kazi nzito kama ile akawatia mioyo kuwa wavumilivu
kwani ni hadhira pamoja ma majaji ndio walikua na haki ya kusema neno la mwisho
“
wewe bakia au wewe ondoka”
ni
aina gani ya mapishi ina changamoto,udhaifu,au mapungufu, ni aina gani ya
chakula kina radha,tija,harufu,afya,unono utaamu na pia je kinapendeza kuliwa
au la hasha.
Hadhira(watazamaji
au wasikilizaji au mashabiki)ikaitwa mbele ili kuanza kufanya utafiti wao kwa
kila chakula, makundi yote yakawekwa pembeni ili kupisha hadhira kujipakulia
kujichotea kujimiminia na kujichana kwa kujilia mautamu yale yalo andaliwa pia
kuchangia mawazo kwa kutoa changamoto mapungufu na madhaifu ya kundi
husika.Kundi la Harder to touch likapewa nafasi ya kuonesha utamu wa
manjonjonjo yao hadhira iliyokuwepo pale haikusita kusema kuwa chumvi haikutiwa kwenye chakula aina ya
loshoro na pia nyanya
hazikuwekwa
kwenye kwenye maharagwe,ingawaje
walijitetea kwa kusema kwamba maharagwe yakitiwa nyanya yanaweza kuchacha ilo
nalo likaibua maswali mbele ya hadira wapo waliokubali na wapo waliopinga
vikari.
Kundila
pili nalo likafanyiwa assessment kundi ili lilibahatika kupita paso udhaifu
wowote la tatu na la nne nalo
yakafanyiwa research yote yaliibuka paso matatizo kundi la tano pia
halikua na any problem lakini watu walilitilia mashaka kundi la sita ingawaje
halikua na kasoro nyingi sana ila tu
hadhira haikuona kama kundi ili lina mchango mkubwa kwenye mapishi yake.
Msema
chochote akaishukuru sana hadira kwa ushirikiano waliouonesha katika kufaidi na
kutoa mawazo yao kulingana na changamoto au pongezi la pishi la kundi husika,kundi
la pili na la tatu,la nne na la tano yakapongezwa zaidi ila kundi la la kwanza na la sita yakawekwa kikaangoni sasa
ikawa ni zamu ya hadhira, kupiga kura ili kuangalia kati ya makundi hayo mawili
kundi la Harder to touch na kundi la Hamtuwezi ni lipi lifungashe virago ili
liyaage mashindano yale hadimu.
Mamia
ya watazamaji wakapewa nafsi ya kupiga kura vipande vidogo vidogo vya karatasi
vikaretwa na kila mtu pasipo ubaguzi wowote alipewa nafasi ya kuandika ni kundi
gani kati ya harder to touch na la hamtuwezi yalifaa kufungasha virago vyake na
kuondoka.hadhira wakapiga kura zile kimya kimya na baaada ya kumalizia upigaji wa kura zile zikapelekwa kwenye panel
ya majaji sita wa hayo mashindano,panel ikakaa kuhesabu kura mbele ya wahusika wote na watazamaji wote.
Kwenye
meza ile ya panel ya majajaji walikaa
watu maharufu Tanzania bara na visiwani
Zanzibar achilia mbali umashuhuri wao ulivuka mipaka mpaka nchi mbali
mbali za Africa mashariki na Africa ya kati ,Kenya Uganda Rwanda Burundi Zaire Malawi
na Zambia.Pannel ile wali upande wa kuria
kiti cha kwanza alikaa mtangazaji maharufu kwenye kipindi chake
kinachoenda kwa jina la MKASI na kinachorushwa na televisheni kubwa Africa
mashariki
SALAMA
JABIRI diva anaye wahoji na kuwatwanga maswali mawili matatu wasanii na watu
maharufu Tanzania na Africa mashariki kama vile wakina Ambwene yesaya(AY)
REHEMA CHARAMILA (RAY C) Mrembo wa Africa NANCY SUMARY na dadaye mwanamuzikia
NAKAAYA SUMARY na wengineo wengi tu kwani hawa ni baadhi yao.
Mtu
wa pili upande ule ule wa kuria alikaa MAADAM RITTA PAULSEN huyu naye alikua
mahuhuri kwa kuwato wasanii mbali mbali ndani na nje ya Africa mashariki
wabunifu na watu wenye vipawa pamoja na vipaji vyao kwa kutumia kampuni yake ya BENCH MARK
PRODUCTION. Bila kumsahau mwana dada wa kipindi cha WANAWAKE LIVE kipindi kinacho onesha mabo
mbalimbali ya wanawake wanavyojituma katika shughuri za kimaendereo
kiujasiliamali,
mwanadada huyu mtetezi wa wanawake na watoto
alisifika sana katika kuangalia changamoto wazipatazo wana wake,migogoro
inayo wakumba wana wake katika kulisukuma gurudumu la maendereo, uhusianao bora
kati ya wana wake na wanaume katika ujenzi wa familia bora zaidi duniani,malezi
mema kati ya mama na mtoto na mambo
mengine kem kem.si mwingine bali ni mrembo wa Africa mashariki na duniani kwote
JOYCE KIRIA.
Upande
wa kushoto waliketi wana ume watatu kwanza alikuwepo MASTER JAY mwanaume huyu
Mwenye sura ya upole hekima aibu na wema ulo mtawala.huyu ni producer maharufu
BONGO kwa kumiliki studio yake inayo kwenda kwa jina la MJ RECORDZ,achilia
mbali uwepo wa master jay pia alikuwepo msomi aliye bobea katika masuala ya michezo,elimu sanaa na utamaduni
ubunifu na vipaji hakua mwingine bali ni muheshimiwa ndugu WAZIRI WA ELIMU
MICHEZO NA UTAMADUNI si mwigine bali ni
PROFFESOR PATRIC MULLUNGU. Mtu almaharufu Tanzania bara na visiwani kwa
hoja zake ziloshiba awapo bungeni akiitetea elimu kuwa ndio ufunguo wa
maisha,ndio bahari ya mafanikio,ndio kitu kisicho na mwisho,ingawaje mwanadamu
ana mwanzo na mwisho wake lakini elimu imekosa mwanzo na mwisho wake.
Na
judge wa mwisho kabisa aliye keti katikati hakuwa mwingine bali ni mtu mdogo
kiumbo ila ana mambo makubwa katika fani na tasnia nyinginezo za sanaa kama
vile tamthiriya,filamu,maigizo, na vichekesho aina ya commedy Tanzania bara na
visiwani Zanzibar .huyu ni mtu maharufu ambaye sanaa yake ipo kwenye kila
kipande cha nyama zake ndani ya damu na ndani ya mishipa yake ya fahamu si
mwingine bali ni msanii anaye kwnda kwa jina la KIKONGWE JOTI ,au kama wamwitavyo watazamaji wa
television ya TBC, ASHA NGEDERE kila
jicho la mwafrica umtazama asha ngedere siku ya jumataano na juma pili.
Hao
ndio panel ya majaji walokaa chini na kuanza kuzi calculate zile kura kwa uhaminifu mkubwa kwani wote walikula
kiapo cha kutodanganya neno lolote wakiamini kuwa msema kweli ndie mpenzi wa
Mungu kura zile zikahesabiwa alfa na omega baada ya mchakato mrefu kama vile
kamba iendayo angani kuuvuta mwezi pasipo mafanikio hatimaye haki
ikatangazwa.katika mchakato wa kuwapata washindi wa mashindano haya kundi la
wakari classics wakapewa nafasi ya
kwanza kuwa ndio kundi bingwa kwa kuyashinda makundi yalofuati.
Kundi
la samba dumezi na samba jikezi likapewa
nafsi ya pili ya ushindi kwani lilionekana limefanya poa sana mbali na
hapo kundi la tatu na la nne ambapo kundi la tatu lilitwa lazima tushinde na
kundi la nne lilitwa sisi ni balaa yote kwa pamoja yakapata nafsi ta tatu kwani
yaliungana na kufanya kitu kimoja.pishi zao zilitia fora sana kwa mahanjumati
yalotokota yalonukia yalo kua manono matamuuu yaani very delicious.
Kundi
la tano la hamtuwezi liliopewa nafsi ya nne ya ushindi ingawaje kundi lile la
kwanza la harder to touch lilivurunda na kupewa asilimia chache hatimaye haki
ikatangazwa kuwa kundi la harder to
touch lifungashe virago lishike njia kwa
kutumia miguu yake.hatimaye kundi la harder to touch likafungasha virago kwa
huzuni utadhani kinda aliye tekelezwa na mamaye kwani walimwaga kilio na kusaga
meno utafikiria nafaka zinavyosagwa kwenye mashine.
Makundi
yalosalia yakapongezwa sana na kupewa nafsi ya kujisukuma zaidi kwani daima
mbele nyuma mwiko hiyo ndio ilokua point ya msingi......
itaenderea sehemu ya tatu
usikose......
No comments:
Post a Comment