WIMBO
HICHO KIPAJI ULAJI
MSHAIRI KAMA JAJI
UKITUMIA UJUZI
FANYAYAKO MAPINDUZI
YAPO MADARAJA CHINI
YAKULA MOJA SAHANI
WEWE KAMA MSHAIRI
WATETEE KWA USHAURI
YAPO MADARAJA JUU
YANAYOPENDA MAKUU
WENGINE NI VIONGOZI
LAKINI NI MABAZAZI
WEWE KAMA MJASIRI
FICHUA ZA KWAOSIRI
HICHO KIPAJI ULAJI
MSHAIRI KAMA JAJI
HICHO KIPAJIA UAJI
TUMIA KWA MAUAJI
UMASIKINI NA UJINGA
MAGONJWA TAFUTA KINGA
WATAZAME WAKULIMA
TANGU ZAMA ZA UJIMAA
WANALILIA MBOLEA
YA SAMADI NA UREA
MASOKO NAYO MAJEMBE
ILI WALIME MAEMBE
LAKINI KIPI WAMEEKOSEA
FAIDA INAPOPOTEA
MATAJIRI WENYE MALI
WAPO WENGI SERIKALI
WANASURA ZA UKAFILI
MAFISADI NA JEURI
RUSHWA PAMOJA MAGENDO
WAMEKOSEA UZALENDO
FICHUA ZA KWAO SIRI
NA KUWACHIMBIA KABURI
HICHO KIPAJI URAJI
KIPAJI KANDAMIZAJI
UKIFANYIE RISECHI
KUMWOKOA MWANANCHI
MYONGE NA MASIKINI
WA MJINI NA KIJIJINI
USISUBIRI NGOJA NGOJA
JENGA ZAKO NGUVU HOJA
VIONGOZI WAKIKUJA
WATAULIZA MOJA MOJA
KATOKAPI HUYO KIJAA
MWENYE KIPAJI ULAJI
LILIANDIKWA MWEZI WA DECEMBER 2012
BY ELIAKIM MWALUKALI
TCHAOOOO
No comments:
Post a Comment