WIMBO
NAKUPENDA MDUDU MJUSI
1
MPENZI WANGU WEWE MJUSI
MWENYE MACHO WASI-WASI
MOYO WAKO WA WASIWASI
UMBO LAKO HILO JEUSI
MPOLE USIE MAAASI
NA MBIO ZAKO KASI KASI
NAKUPENDA SANA MJUSI
2
NIKUPAKATE KWA URAHISI
UNIPE MAPENZI MPAKA BASI
RANGI HIYO YA UKWASI
UTAJIRI MALI NAFASI
MFANO WAKE HARUMASI
NAKUPENDA SANA MUJUSI
NAKUPENDA SANA MUJUSI
3
IKIFIKA HALI YA MIS
TWENDE MBEYA KWETU KWA BASI
TUFUNGE YETU HARUSI
HILIWENYE WIVU NA KAMASI
WABAYA KAMA MAJASUSI
WABAKI MIDOMO WASI
NAKUPENDA SANA MUJUSI
4
NITAKULISHA NA FIASI
MATAMU TAMU MANANASI
BUSTANI YA MIKAKASI
MATUNDA YA MIKARATUSI
LINGA LINGA KAMA TAUSI
MITI MIZURI YA SANDARUSI
NAKUPENDA SANA MUJUSI
5
JUA LA KASI NA KUSI
NYOTA NAZO MBALAMWESI
NDEGE WENYE NZURI NYUSI
YAWATOKE MATE YA FISI
WAKIKUONA MAMAJUSI
WATAIMBA NYIMBO HALISI
KWA MABUSU NA MAKISS
NAKUPENDA SANA MJUSI
6
KUKUPENDA WEWE SIO MATUSI
KWANI NIMEFANYA UDADISI
ILIKUIONDOA HIYO KESI
HIYO KESI YA WASIWASI
NDIPO TUKAPIMA VIRUSI
MAJIBU YAKAJA HASI
NAKUPENDA SANA MUJUSI
7
NAWATAFUTA WAKANDARASI
PAMOJA NA WENGI WATESI
VIJANA WAJUZI WASUSI
WENYE ELIMU YA KARATASI
KUMJENGEA MAKASI
MPENZI WANGU MUJUSI
HAPATE LALA KWA PISI
NA NYINGI NYINGI BULESI
NAKUPENDA SANA MUJUSI
LILIANDIKWA 2012 DECEMBER
BY ELIA KIM MWALUKALI
No comments:
Post a Comment