Monday, March 24, 2014

sura ya nne inaenderea


Sura ya nne

                            FASHION SHOW

Baada ya pumziko  fupi la siku tatu  kuisha makundi yote matano pamoja na washiriki walikutana tena  safari hii hadhira haikupewa nafasi ya kushiriki kwani  kwa siku tatu za mbeleni washiriki walipaswa kubuni mavazi na mitindo  mbalimbali na baada ya siku tatu  hadhira ilipewa nafasi ya kushuhudia  mizigo mipya  kutoka kwa vijana wenye vipaji na ubunifu wa hali ya juu.

Siku hiyo vitambaa vya aina mbali mbali walipewa vilikuwepo vya  utamaduni wa kimasai maharufu kama lubega, ngozi za wanyama kama vile pundamilia,simbachui,chetta,ngombe,kondoo,manyoya ya kuku,kanga,tausi,kuku na mikufu havikukosekana.


Vitambaa vya sufu,vitambaa vya pamba na vinginevyo laini laini walipewa sasa walichoitaji ni ubunifu wa mavazi aina yoyote ile.sheria mpya ilitangazwa kwamba kila kundi lilihitaji kutoa watu watatu watakaochuana  vikali iwapo kundi au makundi ya hao watu watafanya vibaya ndipo hao wenye kundi au makundi watafungasha virago ili kurudi makwao.

Kundi la lazima tushinde wakapewa kila kitu kilichohitajika kwenye ile shughuri pevu. Wao binafsi walipenderea kushona aina tatu za mavazi, kwanza kabisa walitengeneza  aina ya vazi la bakiti jeupe na kikoi chake akavishwa bibie lerato. Pili wakashona vazi lipendwalo na mwanamke wa Nigeria  vazi lililo daliziwa kwa maua maua pamoja na kiremba chake akavishwa mama silvano, na mwisho wakashona vazi la kanga hili vazi walilipa jina la mama Africa  bibie andunje akavishwa akapendeza.kwa bahati nzuri wengi wa washiriki kwenye kundi ili walikua na utaalamu wa kushona kwa kutumia cherehani.

Baada ya kumalizia shughuri ile pevu likaitwa kundi la wakari classics.nao wakapewa walichotaka,hawakua na makuu sana siku ile maana hofu ya kutokufanikiwa iliwatawala sana,ukitegemea hakuna yeyote miongoni mwao aliyejua kushona kwa kutumia  mashine ya cherehani ,lakini Mungu alivyo mwema walipata wazo kwamba iliwapasa wasife mioyo yao,waoneshe uzarendo wao hata kama mahari pale hakuna uzarendo, hivyo basi wakapata idea ya kushona kwa kutumia sindano ya mkonono iliyojulikana kwa jina la sewing niddle.

vijana watatu wa kiume wakaitwa mbele yao wakapimwa vizuri kila pande ya mwili wao, na baada ya kuridhika na ule upimaji vitambaa vya aina mbalimbali vilikatwa,taratibu zingine zilienderea kufuatwa kwa kutumia chalks,mikasi,uzi na sindano kulinganana na vipimo.

 Kwanza kabisa walichukua ngozi ya kondoo na kushona siglend na bahati nzuri ile ngozi ya sufu ilikua na manyoya mengi ,pili waka shone short au kaptura yenye ngozi ya sufu, na tatu wakashona kofia ya mkeka na kuweka ngozi ya sufu na wakamalizia kwa kushona viatu vya ngozi ya ngombe kwa kuwekea ngozi ya kondoo vazi lile alivishwa Beni Toto.

Baada ya shughuri ile pevu wakachukua kitambaa laini hicho wakakidarizi kwa kushona suti yenye rangi mbili mbele nyeupe na upande wa nyuma nyeusi,pia wakatafuta kofia nyeupe iliyopambwa ua jeusi akapewa Elia Abelia.

Baaada ya kazi ile matata wakashona  vazi moja matata lenye rangi nyeupe lililosheheni manyoya ya sufu nyeupe sufu safi iliyotoka nchi ya Canada bara la Australia,sufu ile ilisheheni manyoya pande zote tena vazi likawa refu .walipoulizwa lile vazi ni maalumu kwa ajiri ya nini wao wakajibu ni maalumu kwa ajiri ya kipindi cha baridi au kipindi cha barafu.chini ya lile vazi walitupia kiatu kimoja kirefu cha ngozi ya ngombe kilikua ni kirefu kama  magwanda ya jeshiniukitegemea kiatu kile kilizidia urefu mpaka kufikia mapajani viatu vile ni viatu ambavyo utengenezwa sana nchini Kenya akapewa Nairobi akavaa akawaka kwa kupendeza.na baada ya shughuri ile nene walipomaliza wakapewa ishara ya kuondoka.

Likaitwa kundi la sisi ni balaa na kundi la samba dumezi na simba jikezi maana safari hii yote kwa pamoja yaliunganishwa kwa pamoja nao wakapewa nafasi ya kubuni chochote walichoona kingewafaa kushonwa na kuwatoa vizuri kwenye mashindano yale.wakakaa chini ili wafikirie kwa pamoja ni kitu gani bora cha kubuni…lakini hawakua na chochote cha kufikiria,kwani miongoni mwao wapo waliopenda kubuni vazi la shetani wengine vazi la malaika na wengine vazi lenye mfano wa nyumba,ilimradi kila mshiriki alitaka abuni chake kitokacho moyoni. Lakini kiongozi wao neema mwakyusa aliingia na wazo la kiubunifu waliitaji kubuni mavazi ya kwenye maumbo ya siri ya binadamu.

Kwanza kabisa vijana wa watatu wawili  wa kike  na mmoja wa kiume wakajongea mbele utadhania jongoo anavyotembea wanawake wawili wakapimwa mmoja sindiria pamoja na chupi,ile sindiria na chupi vikadaliziwa maua maua akapewa sister Abella.kijana wa kiume akashonewa singlend pamoja na chupi nyeusi yenye mchanganyiko wa rangi nyeupe, nyuma ya ile chupi likaandikwa neno DUME LA MBEGU.zikashonwa socks ndefu nyeusi  pamoja na kiatu kimoja cheupe akapewa Johnson John

Baada ya kumalizia kazi ile ngumu sasa likabaki kundi moja matata na machachari kundi la hamtuwezi nalo likapewa ukurasa wa kuonesha vitu vyao vitu vikari vyenye ujuzi wa hali ya juu,kwa bahati nzuri vijana wengi wa kundi ili walikua na uwezo wa kushona kwa kutumia mikono na utaalamu wa kutumia mashine ya kushonea.

Wao binafsi walikubaliana kushona nguo za utamaduni au nguo za kizazi kipya,lakini nguo za utamaduni zilipewa nafsi kubwa sana,wakatwaa vitambaa vya kimaasai wakatwa pia ngozi ya ngombe,mbuzi,chui na kondoo,hawakusahau pia vijiti,fimbo,magome na urembo wa aina mbali mbali wa kiasili ulioambatana na shanga,herein,vipini vya puani,bangiri, na vikuuku vya miguuni.

Hatua ya kwanza ambayo wao waliifanya ilikua ni kuliviringisha vizuri lile vazi la kimaasai,kisha pamera akapewa alivae lilikua na rangi ya blue iliyo nakishiwa  kwa nakshi nakshi nyingi za urimbwende yaani shanga nyingi kwenye lile vazi .shingo ya pamera ikapambwa vizuri kwa shanga zenye umbo la duara.hawakuishia hapo wakachukua ngozi ya chui na ya kondoo wakamtengenezea pamera viatu pamoja na kikapu cha ngozi ya chui iliyochanganywa na ya kondoo pia wakamtengenezea pamera viatu na kikapu ndani ya kikapu wakaweka nyama,achilia mbali kibuyu kikubwa chenye maziwa kilifungashwa vizuri.

Pomoni  dia akatengenezewa nguo ya ajabu haswa kwani msichana yule alivikwa nguo iliyotengenezwa kwa kutumia  mifuko ya naironi au kama inavyoitwa RAMBO akafungashiwa na kifuko cha sarufet pamoja na magazeti hakika alivutia mno hata kiatu chake kilipambwa kwa kutumia gunia la kuwekea nafaka kama vile mahindi,maharagwe,mtama,kunde alizeti na njegere akatengenezewa ungo ulionakishiwa kwa kutumia gunia matunda mbali na mboga mboga nazo ziliwekwa kwenye ule ungo, akatwikwa chungu cha asili pamoja na mwiko wa asili  vilivyo nakshiwa shanga za asili ili kuleta mvuto kwa watazamaji.

Boga talenter akapewa vazi zuri la chui akapewa upinde mshale,mkuki pamoja na fimbo.juu ya kichwa chake akavishwa taji tukufu la kifalume lenye rangi ya dhahabu,viatu vyake vilitengenezwa kwa kutumia ngozi ya punda milia,achilia mbali kiti alichokalia kilinakshiwa kwa kutumia  ngozi ya simba na baada ya kutengeneza kiti chake safarii hii ilitengenezwa nyumba maalumu,nyumba yenye umbo la mbao lililomtosha yeye  mwenyewe ikapigiliwa vizuri ikapambwa maradufu kwa rangi  za

nakshi,nakshi, chumba kilikua ni kimoja tu pasipo choo pasipo sebule ila kiti kiti kimoja cha kifalme kiliwekwa banda lilipendeza likavutia kwa rangi ya bendera ya Tanzania.Vijana wanne yaani god listen,ndanda ngabi,Irene paul,na saba saba walifanya kazi ya kulibeba lile jumba kwa kutumia mbao maalumu kazi ikaisha.

Baada ya ile kazi nene tena inayo chosha,vijana wale wakapewa muda wa siku tatu mbele ili kupumzisha vichwa na akili zao na baada ya hapo wangerejea tena ili kuonyesha ufundi na utaalamu wao wa kiubunifu,ubunifu wa kimataifa.







 SIKU YA FASHION SHOW

Baada ya pumziko la siku tatu kwisha sasa nafasi ilioyo bakia ilikua ni nafasi ya kuonesha nini kipya cha kujivunia kutoka kwenye nyuso za vijana machachari vijana wa pande za sinza,temeke,kinondoni,manzese kawe,ubungo,studio,mbagara,sinza,kimara,tabata,gongo la mboto,kitunda,kinyerezi,magomeni mapipa,manzese midizini,mabibo tandika na buguruni.na wengine wengi kutokea mikoani kama vile mbeya iringa,taabora,Zanzibar,pemba,na unguja,rukwa,pwani,rufiji, na hata Arusha achiria mbali kilimanjaro na tanga.

Siku ile ilibadirika kidogo kwani tofauti na siku zingine ambazo msema chochote alikua mmoja sasa mwingine aliongezeka, masanja mkandamizaji, Bamboo pia alikuwepo Bamboo alikua ni mchekeshaji maharafu wa vichekesho vya the comedy  katika kituo cha East Africa television

Kipindi hiki waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari kama vile televisheni,radio,magazett,website na blog walikuwepo achilia mbali wabunifu mbali mbali wa mavazi nao walikuwepo kama vile mbunifu hassan hasssano,mbunifu martini kadinda, mwanamitindo wa kimataifa miriamu odemba. Na wengineo wengi walikuwepo kushuhudia kwa macho yao kwani macho hayana pazia wala usitegemee kuambiwa njoo ushuhudie mwenyewe.

 Watu walitulia wakijisikilizia muziki mwororo kutoka kwa kijana machachari aliyekuja kwa kasi na  kupachikwa jina la mwanamuziki DIAMOND PLATTINUMZ wa kundi laWASAFI CLASSICSS aliwafanya watu wa injoy kwa wimbo wake matata wa NUMBER ONE alio tengenezea video south Africa

Baada ya hadhira ile kukaa na kungojea kwa muda ili kujua ni nini vijana watawavumbulia Mc massanja akishirikiana na Mc bambo walifungua pazia ili kuyakaribisha makundi yale yaoneshe utundu wao.kundi la wakari classics likapewa salute na heshima zote kwani safari ya kwanza ya kupanda milima na kuvuka mabonde walifanya vema sasa walitegemewa kuvumbua vitu vipya zaidi kwani waswahili wana kawaida ya kusema kipya kinyemi iweje kikose kidonda,kipya utembezwa na kibaya utangazwa.

Kwa mada na mapozi akapita kijana beni toto  pale kwenye zuria jekundu zuri refu utadhania bara bara ya rami,akawaonesha hadhira na waandishi wa habari nini cha kujivunia,singlend short,na viatu vya sufu watu wakapiga makofi na kumshangiria,Elia Abelia akakatiza kwa heshima zake zote utadhania anaenda kwenye harusi tena harusi yake yeye mwenyewe,vigere gere na vifijo vilimulika ukumbi ule kama vile taa ya group yenye mwanga mkari kama jua.hakika alipendeza kwani baadhi ya wanawake uvumilivu uliwashinda wakaachia mabusu ya midomoni mwao ……mwaaaaaaaa…….mwaaaaaaa…….kisssssss….kissssssss…..mwaaaaaa baby.

Safari hii Nairobi akaonesha kitu chake kikari cha kimataifa we acha tu kijana aling’aa,aliogaaa,alitakataaa,alipakaa,alivutia na kuacha midomo wazi kwa vazi lake refu lenye manyoya ya sufu,tena vazi la kipindi cha joto na viatu vikari kama   meno ya simba, picha ziliwaka waaaaaa…..waaaaaaa……waaaaaaa…..kila upande wenye blog wakaandika vyao na wenye website wakaandika vyao ili kupamba picha za habari.

Mc bamboo akawang’ata sikio ndugu watazamaji kuwa kundi lijalo ni kundi la pili maharufu la lazima tushinde watu waka kaa chonjo kuwatazama ,lerato binti mrefu mweupe akajivuta pale ukumbini kwa vazi lake la batiki nyeupe akifuatana na mama silivano kwa vazi maharufu la kina igeria zito lililo gharimu mamilioni ya shilingi, na baada ya mama silivano anduje naye akakatiza kwa kanga yake moja iliyoonesha maumbo yake yote ukitegemea binti huyu kutokea mkoa wa tabora alijaliwa hips za moto,mguu wa bia makalio yalonesa nessa hali iliyowapa wakati mgumu wanaume wakware

kwani kanga moja na miondoko ile ilisababisha miti yao iliyo jaa utomvu isimame kwa hasira kwani mingine ilianza kumwaga utomvu bila heshima na adabu lakini kwa bahati nzuri walikua wameketi kwenye viti na pia kila mtu alikua bussy kutazama kilicho mleta hakuna aliyejua la mwenzie maana jambo waso lijua litawasumbua.Kundi hili halikutia fora kwani hata baadhi ya wanafiki waliinama chini chini na kuanza kupiga midomo wakidai kuwa kundi limedorora, halina jipya

Mc masanja akalialika kundi la sisi ni balaa pamoja na kundi la simba dumezi na simba jikez waje waoneshe kipi ambacho wanajivunia mbele ya hadhira inayo watazama.

yallab!!! Toba……astaghafrah!!!laana hii laahaulaaah!!!! Msalie mtume!!aibu gani hii iliyoibua vicheko na kuvunja mbavu za watazamaji,wapo walioziba nyuso zao kwa aibu ya mwaka wapo walicheka mpaka mbavu zao kupasuka,waandishi na watazamaji pamoja na makamera men wao walimiminika kujichukuria habari iliyowacha midomo wazi.

Si jingine bali ni yale matukio ya kundi hili la nne na la tanokupita wakiwa wamepigilia vichupi,vimini,skafu na vikoi,achilia mbali sindiria.

waandishi wambeya wa magazeti ya udaku kama vile RISASI,UWAZI,IJUMAA,AMANI,na mengineyo mengi tu hawakua nyuma kuandika walicho kinyaka.wasomi na wana falsafa wengi waliibua maswali kuwa sasa mashindano talent show yanaelekea pabaya iweje midume mizima na mijike mizima ioneshe uchi wao mbele za watoto,watoto wa taifa la kesho taifa lililojaa maadili heshima na hekima taifa linalomcha Mungu na yesu kristo mwana wake wa pekee leo hii wana buni sifa chafu jamaniii nyie jamani!!!!.

Wapo walio coment kwenye magazet yao na dibate zao kuwa yale yalikua ni mashindano tu kwa maana hiyo ubunifu na utaalamu ni kitu kilichopewa kipaumbele….therefore wenyechuki waache chuki zao …chuki zao ni  za bure tena zina wasumbua.any way makundi haya mawili yalipongezwa na kuambiwa kwamba yamefanya vizuri jambo la msingi ni ku keep it up wasonge mbele maisha ni safari ndefu,maisha ni milima,maisha ni mabonde,maisha ni mito,maisha  ni every thing.

Mc massanja pamoja na Mc bamboo,waliwataka ndugu watazamaji wakae mkao wa kula na kunywa kwani tayari chakula kiliandikwa mezani na wagawa chakula walikua wapo tayari kuwalisha na kuwanywesha watazamaji vitamu tamu vinono nozi  hawakuwa wengine bali ni kundi la hamtuwezi.kwanza kabisa akapita bibie pamera…….yelloooo!!!! kwa vazi lake la kimasai bibie aliita fora mno,bibie alivyo mrefu kama twiga wa mbunga za ngorongoro akajipamba mavazi yenye shanga akajiachia kwa urembo wa herein,kipini,mikufu ya kimaasai na bangiri za kimaasai bibie alijipaka tope usoni na kila mtu alimsifia.

Dj choka alipomwona bibie pamera anakata mbunga bila wasi wasi,akaweka wimbo wa msanii mmoja maharufu ila kwa sasa hatunaye  tena duniani si mwingine bali ni ABEL LOSHIHIRARA MOTIKA  almaharufu kwa jina la  MR EBBO na wimbo wake wa mi mmaasai bwana…nasema mi mmaasai.


Pamera akaanza kucheza kama vile wanawake wa asili ya kimaasai.pomoni dia binti yule naye akafuatia  akiwa amejikwatua na kujipamba swaafii sana  kwa mavazi yake ya karatasi kila mtu aliye mwona alibaki kupigwa na butwaa  na bumbuwazi kwani hawakuamini kama kweli magazeti yana weza kushonwa na kuwa vazi zuri lenye mvuto wa aina ile hadhira ilifuraia sana kwani vijana walionesha hali ya kujituma zaidi kwani kutokana na jinsi pomoni alivyopendeza hakukosa mchumba pale pale.

Docta bingwa wa matibabu ya moyo katika hospitary ya muhimbili alivutiwa sana na ulimbwende wa pomoni dia,docta Erick akainuka na kwenda kumtunza manoti mekundu mekundu kibao, mapedeshee  nao hawakua nyuma kwani walipoona docta Erick anafanya yake nao wakajitoma zaidi kumwagia manoti  bibie pomoni dia.

ilipofika zamu ya boga talenter kila mtu alibakia na maswali mchanganyiko kwani hawakuelewa ni nini kilichokuwemo ndani ya ile nyumba,wapo waliodhani ni maiti ,wapo waliodhani ni gaidi,wapo waloidhani ni ni nyumba tu iliyo buniwa  wala hakuna chochote……..lakini ukweli ni kwamba uzaniacho ndio kumbe sio na jambo uso lijua ni kama usiku wa kizaa.

Mlango ulipofunguliwa vijana waliombeba boga talenter wakapiga saluti ya heshima kwa mfalme na pia hadhira nayoikafanya ishara yakupiga magoti kama vile waumini wa dini ya kiislamu wafanyavyo wakiwa kwenye ibada zao ilikua ni ishara ya heshima na taadhima kwa mfalme aliyebebwa kwenye kiti chake kitakatifu.

Hakika ukumbi ulijawa na furaha siku ile boga aliwavutia kila mtu si wana michezo si wana siasa si wana falsafa,siwatu wa kimataifa aliwavutia kila mtu ukitegemea duniia nzima ilikua ikiwaangalia wanavyofanya maajabu yao kupitia vyombo vya habari kama vile television ya TBC,ITV,STAAR TV,CHANNEL TEN,SIBUKA TV NA CITZEN TV na zinginezo nyingi.

Hadhira ilishangiria na kupiga makofi na baada ya kuondoka ile fulsa hadimu iliyo tazamiwa na wengi  na iliyotegemewa na wengi kuangalia product mbali mbali zilizotengenezwa na vijana wale wengi wlizinunua na wengine wakatoa oda ya kutengenezewa na kulipia baada ya  kazi kukamilika .

Lakini kabla ya matokeo kutajwa ya nani kashindwa na nani kashindwa Mc masanja nja Mc bamboo waliwataka ndugu watazamaji na ndugu wasikilizaji kutoa michango ya harambe ya kuwasaidia watoto yatima na wajane  pamoja na wakina mama wenye ugonjwa wa kansa ya matiti,pesa nyingi zilichangishwa karibia milioni ishirini ukitegemea ziliitajika million sita tu.Hakika kutoa ni moyo na usambe ni utajiri kwani damu ni nzito kuliko maji.

Baadaya ya kuchangisha pesa zile Mc masanja pamoja na  Mc bamboo waliwashukuru ndugu wageni ,majaji pamoja na washiriki, kwa moyo mzuri walijotolea na kwa ushirikiano bora walioufanya.lakini pia Mc  bamboo aliwatangazia watu wote mahari pale kwamba kuna mtu amepoteza funguo zake za gari,gari aina ya prado gari la kifahari zaidi akamtaka mtu yeyote aliyeiona funguo iyo arudishe mapema.kwani lile gari lilikua ni gari la kigogo fulani wa serkiali ya jakaya mrisho kikwete.lakini hakuna aliyejitokeza.

Baada ya nusu saa kupita majaji wakakaa mezani ili kutoa majibu ya mashindano yale.ukweli ni kwamba majaji walipendezwa sana na kazi ya makundi yote ,kwani ilikua ni kazi ngumu sana ,waliwapongeza sana na pia hawakuacha kuwakosoa pale ambapo waliona kuwa washiriki wamekosea. Au washiriki wanaitaji kurekebisha makosa au kutofanya makosa kabisa  katika mashindano yajayo.


Ikafikia kipindi cha kutangaza washindi wa mashindano yale ya mavazi jaji salama jabiri,akalitangaza kundi la hamtuwezi kuwa ndilo kundi bora na lililofanya vizuri katika mashindano yale ya fashion show,furaha zililipuka sangwe na nderemo vilimiminika utadhania maji ya mto Nile mto usiokauka milele katika jangwa la sahara.


Muheshimiwa waziri mulungu akasimama na kuwapamba maua kundi la wakari classics,kuwa ni kundi bora na la pili katika mashindano yale,vigeregere vilivyo ambatana na muziki wenye beat kari vilisikika mahari pale,ngoma na midundo ya aina mbali mbali vilitawala eneo lile.

Maadam ritta paulsean akawapa hai kundi la tatu la lazima tushinde kuwa ndilo kundi bora machachari nalo lilishika nafasi ya tatu kuibuka katika kinyanganyioro kile.jaji na producer maharufu bongo master jay naye akawatangazia ndugu watazamaji kuwa kundi la sisi ni balaa pamoja na kundi la simba dumez na simba jikez yalikamata nafsi ya nne ila aliyataka kuji keep bussy maana hawakufanya vizuri sana watu wakawapigia vigeregere makofi na nderemo.

Sasa ikawa ni zamu ya nani atoke nani abakie kuenderea na michuano ile,kila mtu aliye kaa upande wa hadhira alijisemea moyoni kuwa kundi la nne ni lazima wafungashe virago vyao kwani walionekana kuwa si lolote si chochote kwenye yale mashindano kazi gani kuonesha vichupi na miili yao ya heshima watu wazima hovyo….vya wazungu wa waachie wazungu na vya wa Africa viachwe Africa.jaji joyce kiria akapewa nafsi ya kutangaza kundi lipi linastahiri kutoka na kundi lipi au yapi yana stahiri kuenderea kudunda.

Maadam joyce kiria akasimama mahari pale naye akayapongeza makundi yote wala hakusita kuyakosoa pale yalipostahiri kukosolewa,lakini mwisho maadam kiria akatangaza kuwa halitakuwepo kundi lolote la kutoka kwani yote yame perform better ushindani ulikua ni mzito na pia ni wenye tija hivyo basi makundi yote yajiandae vema kwa mashindano mapya  yajayo.

ooooosh……my god!!!ndivyo sauti za washiriki zilisikika kumshukuru Mungu kwa kuwa nusuru kuingia kwenye kikapu cha takataka.

Makofi nderemo na vigere gere vilitawala eneo lile,mc masanja akawataka washiriki wote wajumuike kucheza muzik na kisha baada ya hapo ukumbi ule ungefungwa wakatangaziwa kuwa watakua na pumziko la juma moja na baada ya pumziko ilo walitakiwa kurejea tena kwenye mashindano.

mwanamuziki machachari wa muziki wa kizazi kipya bongo  naasibu abdul  au diamond platinumz akapewa nafasi ya kutumbuiza singo  yake machachari tamu masikion mwa hadhira iliyo kwenda kwa jina la  NIMPENDE NANI.kila mara hadhira waliposikia neno nimpende nani, wote kwa pamoja  wakajibu neno  ……woteeee…..

Ukumbi ule ukafungwa na watu wakatawanyika kurudi majumbani kwao maana ilikua ni mida ya saa sita usiku.


 yule kigogo wa serkiali alibaki amechanganyikiwa asijue nini cha kufanya ili aliondoe gari lake maana ufunguo ulipotea na hakujua ni wapi ataipata.alichanganyikiwa…akawa anatembea tembea hapa na pale….masikini kigogo alijiuliza maswali kibao yaso  na majibu.


Oh  my god who stole my car key?........imeenda wapi?.......nani kachukua ?.......nitamwambiaje mama watoto kuwa fungua ya gari zuri kama lile la kifahari imepotea?……..aaaash!!!!..... kadri alivyozidi kutembea ndivyo akawa anahisi kama kuna maumivu kidogo kwenye mguu wake wa kushoto,haraka haraka akavua kiatu ili kuangalia ni nini klinacho muumiza,Mungu wangu wee!!kumbe ni ufunguo,ufunguo wa gari yake mwenyewe furahaa ilimjia chozi lilimbubujika chozi la furahaa chozi la kuuraani uzembe na usahaulifu ulo mkabiri.

Taratibu akaenda kwenye gari lake na kuliwasha kisha akalitoa moto likapaa kama ndege ya  BRITSHI AIR WAYZ.

Tatizo la yule kigogo wa serkiali alikua na tabia ya kusahau sahauvitu mara kwa mara,hata akiwa bungeni muda mwingi alikua akiuchapa usingizi mate yalimtoka mdomoni utadhania  mboga mboga ya mrenda yalimsaidia sana kuchafua karatasi zake za hotuba hata alipoulizwa maswali kwani alijibu?

hapana alienderea na usingizi wake mnono kama samaki aliye shiba.

Hakukumbuka kwamba ni mambo yake ya kitoto yaliyomfanya aiweke funguo kwenye kiatu chake,hata hivyo kigogo yule siku ile alisahau kurudi Nyumbani kwake akajikuta anapita njia ya ohio huko nako akakumbana na wanawake wenye tabia ya kujiuza.

SURA  YA  TATU


                 BOGA TALENTER ANAFURAHI PAMOJA NA PAMERA


Baada ya kuisha kwa kazi ile ya mapishi vijana waliosalia walaanza kupongezana  kwa kazi nzito waliyo ifanya.siku ile pamera alimchukua boga talenter  akaenda kumtambulisha kwa wazazi pamoja na ndugu zake kama ni rafiki na mchumba wake mtarajiwa kwani kabla ya hapo aliwaambia wazazi wake kuwa amepata  rafiki mzuri ambaye angependa aje kuwa mume wake siku za usoni. Wazazi ndugu marafiki na jamaa ya pamera wakafurahi sana kumuona  boga talenter kwani alikua ni kijana mzuri haswa .penielia na penslavia  dadaze pamera wakaanza kuonesha jicho la husuda.


Roho ya kumtamania kijana yule ilikua kwa kasi kwani boga talenter kwa utanashati alikua yupo juu kwani katika wanaume vijana ishirini ambao wangepita mitaani pamoja na boga talenter hakika mtu aliye watazama asingesita kumsifia boga talenter kwa uzuri na utanashati.ni jina tu  alilopewa la boga ndilo halikumpendeza ila kwa utanashati kijana aliita fora hata babaye usiku na mchana alijitwanga maswali yasiyo na majibu ni wapi mtoto yule alikouta  hali ile ya kuwa bonge la handsome.


Boga naye akamtambulsha yule mrimbwende pamera kwa   kwa babaye mzee talenter aliyekuja muda mfupi baada ya mashindano kuanza,wote kwa pamoja walitawaliwa na nyuso za furahaa ya ajabu.


Siku ile pamera aliona kuwa uchovu ni mwingi sana ndani ya mwili wake kwani kazi waliyoifanya ilikua ni kazi nzito na ya kufa mtu,akamwomba boga waende ufukweni mwa bahari ya hindi  kujipumzisha .huko nako walipofika michezo mbalimbali ilienderea mchezo ambao ulikua ni mgumu sana kwa boga ulikua ni kuogelea boga hakujua kuogelea hata kidogo alipata shida sana ya kucheza na maji pamera alipoona udhaifu ule wa boga akaanza kumfundisha taratibu kwa kutumia mipira maalumu ya kuogelea na maboya ya gari hali ambayo boga talenter  alifurahia zaidi.


Jioni ya siku ile pamera alimpeleka boga sehemu nzuri ya MLIMANI CITY CINEMA  ili kucheki muvi firamu na tamthiriya, sinema iliyo mvutia sana boga talenter ni sinema ya marehemu STEVEN CHARLES KANUMBA ilitoitwa  ANKO JJ kwani msanii aliwakonga sana  mioyo watazamaji kwa kipaji chake alicho kionesha jioni ile wakacheki  tamthiriya moja ya kikorea iliyo kwenda kwa jina la  JUMONG na wakamalizia kwa firamu tamu ya mwana dada aliye chipuka kwenye muvi ya FOOLISH AGE wala si mwingine bali ni ELIZABETH MICHAELI au LULU.


Achilia mbali kumpeleka  boga talenter sehemu nzuri ya mlimani city cinema  binti yule wa tajiri  alimpeleka boga talenter hoter moja yenye hadhi Ya kimataifa  inayoitwa NYUMBANI LODGE  hoter ya mwanamuziki wa kimataifa LADY JAY DEE. Wakaagiza supper ya kinywaji cha maziwa mazito CAPPUCCINO kwa utamu ule hata boga aliona  ajirambe mikono kama mtoto mdogo kwani hakuwai kuonja vitamu tamu vya hoterini,baada ya supper yao kuisha wakaagiza na dinner iliyo sheheni wali kwa kuku wawili wazima pamoja na juice ya  ya matunda.


Siku ile kulikua na ugeni  wa wanamuziki   kutoka mwambao MZEE YUSSUPH na ISHAA RAMADHANI almaharufu kwa jina la ISHAA MASHAUZI , wanamuziki wale wa nyimbo za TAARABU walitumbuiza nyimbo zao zilizo wakonga watazamaji kama vile MAMA NIPE RADHI.ukumbi wote ulibakia kupiga kelele za nderemo na vifijo sio isha mashauzi tu na bendi yake ya mashauzi classics pia mwanadada lady jay dee akiwa na bend yake ya machozi aliwapagawisha  wapenda starehe kwa wimbo wake wa YAHAYA. Hakika siku ile ilikua ni siku  ya burudani tosha kwa  vijana hawa wawili.


Usiku mnene ulipoingia pamera akamwomba boga talenter wakodishe chumba hoterini ili walale pale pale lakini boga alisita kwani hakumwaga babaye mzee talenter hivyo aliingiwa na hofu kuwa mzee wake anaweza kumtafuta  kuwa na wasi wasi na mahari alipoenda boga talenter.


Pamera akamrudisha boga talenter Nyumbani kwao kisha na yeye akarejea Nyumbani kwa wazazi wake  ilikupumzisha kichwa ubongo na akili  kwani mc masanja aliwatangazia washiriki kuwa walitakiwa kujiandaa na shindano jingine bab kubwa la fashen show baaada ya siku tatu zijazo

hallow..hallow...nikiwa kwenye semina mwezi october 2013.....semina iliyodhaminiwa na DERROITE TANZANIA ..tukijadili mabo ya uongozi bora........katika kituo cha watoto walemavu wa CHILD SUPPORTZ TANZANIA...kilichopo block t soweto mbeya
















       SEHEMU YA PILI

Siku iliyofuata  boga akamwambia dady anaenda kwenye mashindano talent show,dady hakua na kinyongo akamkubalia mwanawe na pia alipomwona pamera alifurahi sana kwani pamera alikua ni binti mchangamfu na Mwenye furaha na pia alikosa aibu kabisa,pamera na boga wakaenda mwenge pamera akiwa amemshika boga mkono  wakayacheki majina yao kwenye notice board kwa bahati nzuri wote wawili walibahatika kuingia kwenye yale mashindano,walichaguliwa vijana therathini.

Vijana wote wakatambulishwa kwa hadhira iliyokuwepo pale kwenye hall,msemaji mkuu au msema chochote wa siku hiyo alikua ni Mc maharufu kwa vitimbwi vichekesho pamoja na vituko vya hapa na pale  MASANJA MKANDAMIZAJI  Pamoja na mchezesha music almaharufu kwa jina la DJ CHOKA .Lakini pia ukumbi ulipambwa na vifaa vya kimuzic kama vile magitaa,matarumbeta,vinanda,violin,ngoma za asili na vifaa vingine vingine vingi bila kusahau microphone pamoja na speeker kwa ajili ya kutole  na kuingizia sauti.

Yalizaliwa makundi sita kila kundi liliwabeba vijana watano watano kundi la kwanza liliitwa HARDER TO TOUCH, kundi ili liliwabebavijana wa kiume watatu  na wa kike wawili majina yao waliitwa MIZANI,KINOMANOMA,GODZILLA,MAMAJUSI,na RWANDAI. Kundi la pili liliitwa  WAKARI CLASSICS kundi ili liliwabeba vijana kama vile BENITOTO,ALL DAYZ CONFIDENCE,NAIROBI,YOUNG MBARA, na ELIA ABELIA. Kundi lao liliwabebe vijana wote wa kiume.Kundi la tatu lililoitwa  LAZIMA TUSHINDE liliwakusanya vijana kama vile MALIPO MARIBORO,LERATO,PANDA HILL,MAMA SILVANO, na ANDUNJE,

 Kundi la SISI NI BALAA liliwazoa  wasanii wake majina yao ni JOHSON JOHN,SISTER ABELLA,ADAMSON ,NEEMA MWAKYUSA na DIANA NYOKS, achilia mbali majina ya kundi hili kundi la tano lililoitwa SIMBA DUMEZ NA SIMBA JIKEZ liliwakusanya wajanja wake kama vile IRENE POO,GOD LISTEN PETER JOSEPH,SABA SABA,NDANDA NGABI na SHAA DIANA ROZE, kikundi cha mwisho wao walijipa jina la  HAMTUWEZI  hawa walijipanga vizuri  kwa majina yao kama vile PAMERA,BOGA TALENTER,POMONI DIA,COMMOROW na LOSHORO 


Mc masanja mkandamizaji akawaambia kuwa wote pale hawapo kuuza sura zao(kujionesha tu) ila wapo palekuonesha vipaji vyao vya hali ya juu,uwezo ubunifu juhudi pamoja na kujituma kwao ili waweze kushinda mamilioni ya shilingi  na kuitangaza vizuri ramani ya nchi yetu kimataifa.Wote walitakiwa kushiriki au kushirikiana katika categorization mbali mbali zikiwemo

                               1.MAPISHI YA VYAKULA VYA AINA MBALIMBALI

                                2.UFUNDI WA KUBUNI MAVAZI YA AINA MBALI MBALI(fashion show moder)

                                3.MAIGIZO

                                4.KURUKA KAMBA

                                 5.KUOGELEA

                                 6.MUZIC(kuimba,kucheza,kutunga na kushirikiana katika performance)

                                 7.UBUNIFU KATIKA UCHORAJI

                                 8.UREMBO NA UTANASHATI

                                 9.USAFI KWA UJUMLA

                                 10.KUKIMBIZA BAISKERI KWA MIGUU

                                 11.KUVUTA KAMBA

                                 12.MPIRA

                                 13 KUKIMBIA,.KUKIMBIZA KUKU, KULA NA KUNYWA

                               14.UBUNIFU WA KUJIBU MASWALI KWA LUGHA YA KIINGEREZA

                                 15. MAZOEZI YA VIUNGO NA MAPAMBANO


                                         MAPISHI

Siku ile vijana walipewa kazi moja tu ya kuandaa mapishi  ya aina mbalimbali kila aina ya vyakula ililetwa hapakukosekana aina yoyote ya chakula kwani hata wasivyovijua vililetwa mbele yao vikiambatana na viungo mbalimbali vya hayo mapishi bila kusahau mafuta chumvi,au sukari ili kufanya vyakula viwe vitamu.Zikaletwa mbele yao

cabbage,Chinese,spinach,carrot,matango,spagget,unga wa kupikia vyakula vya aina mbali mbali ikiwemo ugali na mikate ya ngano,samaki.mchele, nyama ya kuku ya nguruwe ya mbuzi ya bata, dagaa,sukuma wiki, mnafu,ngogwe,njegere,kunde bamia,na vinginevyo vingi pasipo kusahau matunda. Sasa kazi ikaanza kila mtu aliitaji kushiriki vizuri ili kuleta mvuto wa kazi ile.Wakapewa mavazi maharumu kama yale ya wapishi wa mahoteini nao wakajivika vema wakaonekana  kama wapishi haswa.

Sheria iliyowekwa ilikua ni kwamba iwapo kundi moja limeshindwa kufanya vizuri au makundi yote yameshindwa kufanya vema kwenye yale mashindano basi watu wote wakundi au makundi husika walitakiwa kufungasha virago na kutokomea kurundi Nyumbani kwao.

Kundi la Harder to touch kama walivyopenda kujikita wenyewe  YOU NEVER TOUCH US,lilikua ni kundi la vijana wachangamfu,wacheshi,wapole na pia vijana wenye matumaini sana ya kushinda kwa swagga zao hata siku ya kwanza kupanda jukwani hadhira iliwshangilia mno wakijipa matumaini ya ya kwamba ushindi ni wao hakuna wa kuwazidi na watashinda kwa kishindo kikuu cha kushitukiza.

Haraka haraka wakapata wazo kuwa waandae mlo unaoitwa LOSHORO,pishi la kabilala watu wa kaskazini mwa Tanzania maharufu kama wameru wa Arusha. Wao walichofanya walichukua ndizi ambazo hazijaiva yaani matokii,wakaumenya mkungu mzima wa zile ndizi za matokii kisha wakazikata kazikata vipande vipande baada ya kuzichemsha ndizi zile wakakata nyama vipande vipande nazo wakazichemsha,wakachukua mahindi ya kukobolewa nayo wakayachemsha vizuri vyote vikawa  vinatokota tokota na kutoa harufu nzuri ya utamu na unono na baada ya kuona kuwa pishi limeivaa

 wakachanganya na maziwa mgando,ila walipenda sana kutia maziwa fresh lakini ilikua nichaguo  lao wenyewe……….kwanza kabisa waliziponda ponda zile ndizi zikawa uji uji na kisha `wakachanganya na nyama bila kusahau yale maziwa pamoja na makande pishi likaendelea kutoa unono.Hakika lile pishi lilikua ni pishi bomba kisawa sawa ingawaje walisahau kutia chumvi ilo nalo likawa kosa lao kubwa sana.

Pishi la pili walilolizimia kulipika lilikua ni pishi la chapatti maharagwe,chai nzuri ya maziwa freshi ikatengenezwa maziwa mazito ya moto moto yakachemshwa chapatti tamu aina ya chapatti kavu zikapikwa pamoja na maharagwe yalikaangwa vizuri.Upungufu wao ni kwamba walisahau kutia kiungo mahalumu kiitwacho nyanya ingawaje mafuta  ya kula,pilipili hoho,caroot pamoja na vitunguu viliwekwa vizuri.mbali na ilo pishi  pia chai yao ilikosa sukari jambo ambalo wao wenyewe kama kundi walisahau kutia sukari.

Pishi la mwisho walilolipika lilikua ni pishi  la ndizi za kukangaa zilizotiwa asali,chips mayai,viazi mbatata vya kukaangwavilivyotiwa pilipili,baada ya kumalizia mapishi yao wakayaifadhi mahari pazuri kisha wakapewa ruhusa ya kuondoka ili kupisha kundi la pili nalo lioneshe mahanjumati yake,kwani hadhira ilivutiwa sana na juhudi pamoja na ujuzi ambao kundi la  HARDER TO TOUCH  liliuonesha.

Likapewa nafasi kundi matata na kundi machachari la la WAKARI CLASSICSS ingawaje ndani ya kikundi hiki walikuwemo baadhi ya vijana wenye tabia chafu kama vile unywaji pombe kupita kiasi,uzinifu ,kutukanana matusi ya nguoni,kupigana na pia kuibiana vitu,lakini vijana walikua wapo super wapo juu katika kujituma na pia kufanya maujanja ya hapa na pale.Walijinadi kua wao ni wakari na hakuna mtu wa kuwazingua,kwani wanaweza kuliambia jua simama nalo likasimama,wanaweza kuliambia jiwe badirika uwe mkate nalo jiwe likabadirika,bahari iwe chumvi nayo inakua chumvi,nyoka awe samaki naye akawa samaki.Walijigamba na kujinadi sana hadi hadhira ilipasuka mbavu kwa vicheko mfululizo.


Wao walikubaliana kuandaa UGALI WA MAZIWA FRESH YA MOTO,ugali ukapikwa kwa kutumia unga wa dona na maziwa fresh yakachemshwa.pishi la pili  lilikua ni mboga mboga wao walichofanya ni kutengeneza cabbage ya kuchemsha na kutia aina zote za viungo, mchuzi wake wakauweka pembeni na walipoulizwa mchuzi wa cabbage una saidia nini mwilini jibu walilo litoa ni kuwa mchuzi ule ni mzuri sana kwa  kupunguza mafuta na unene mwilini.


Walipomaliza hiyo shughuri pevu pishi lililofuata  lilikua ni mayai , mayai haya waliyagawa katika makundi matatu kundi la kwanza lilikua ni mayai ya kuchemsha  wakatengeneza na chai ya maziwa wao walisema kuwa mayai ya kuchemsha pamoja na maziwa usaidia kupunguza unene mwilini.


Lakini walipopika mayai yaliyochanganywa na vitunguu,carrot, pamoja na vipande vya hoho walidai kuwa haya ni mazuri kwa ajiri ya kunenepesha mwili na kuupa mwili nguvu pamoja na akili. Wakamalizia kwa kupika mayai yaliyo changanywa na carrot nyanya na hoho ,vitunguu  pamoja na samaki watatu waliokaangwa kisha mapishi ya kuchanganya changanya vile vitamu tamu yakaanza.shughuri ile pevu ilipoisha walivitandaza vyakula vyao vitamu mezani ili hadhira ipate kuonja kunusa nusa ,kububuna,kukodorea macho, kuvitamani na kujifunza zaidi kutoka kwao kwa kutumia maswali na majibu juu ya utundu na utaalamu wao katika mapishi.


Kundi la tatu la LAZIMA TUSHINDE na KUNDI LA SISI NI BALAA  ambalo ni kundi la nne wakaitwa wote kwa pamoja ili kuonesha hadhira manjonjonjo na mautundu ambayo mwenyezi Mungu amewajalia hawakua na makuu sana  upole busara wema na kujituma ndiyo ilikua sifa yao njema.Walianza na uhandaaji wa juisi ya matunda,hatua ya kwanza waliyoichukua ilikua ni kutafuta maembe,maparachichi,machungwa,maboora


mapapai,mananasi,na matunda mengineyo mengi ya shambani kisha wote kwa pamoja wakayamenya vizuri tena kwa wingi utadhania mchango wa baharini na hatua ya tatu ilikua ni kuyasaga kwa kutumia mashine maharumu ya kusagia matunda kwenye jagi, na hatua ya mwisho ilikua ni kuyaifadhi yale matunda kwenye chombo maalumu kila spice ya matunda kwenye chombo chake na mahari pake.


Pishi la pili lilikua ni pishi la uji(stiff polidige)uji mzito ulitengenezwa,uji uliochanganywa na maziwa freshi mazito ya ngombe ,ukitegemea walitumia utundu na ufundi wao kwa kuchanganya blue band,karanga, mahindi,njegere choroko mtama ulezi,maharagwe ya soya, mchere na ngano.kwa pamoja vilisagwa vizuri vikachanganywa changanywa uji mzito uliotiwa sukari ya kutosha uliwekwa tayari kwa ajiri ya mywaji.


 Wakamalizia kwa kupika pishi bomba haswa wala sio lingine bali ni pishi la  la supu ya  mafuta mafuta ya ngombe yalochanganywa na nyama kadha za mbuzi, wakapaliliza na nyama ya kondoo si mchezo kwani hawakusahau nyama ya kikanda cha nguruwe,kweli mtu ni afya na ni lazima ale vyakula bora.


Likaitwa kundi la tano  kundi la SIMBA DUMEZI NA SIMBA JIKEZI ,vijana hawa hata ukiwaangalia hakika usingesita kujisemea hawana mpizani,vijana walijariwa urembo na utanashati na pia nguvu zao za kuchapa kazi zilikua hazihesabiki ,ndio  maana wakajiita simba dumezi na simba jikezi, maringo ndio ilikua sifa mahususi ya kundi hili, waka         yavunja moyo makundi mengine lakini ukweli ni kwamba asokubali kushindwa si mshindani.


Nyama ya kuku ikaandaliwa,wakai rostisha ile nyama.Nyama ya ngombe ikaandaliwa mchemsho safi sana,nyama ya mbuzi ikaandaliwa mishikaki bomba haswa na pia nyama ya kondoo ikapikwa vizuri vizuri kwa kutumia viungo vitamu vitamu bila kusahau pishi bomba la dagaa wa ziwa Victoria dagaa wanene na tena wenye afya kama mlima Kilimanjaro.


Pishi la pili lilikua ni pishi la  mboga za majani wakajiandalia Chinese safi ya kukaanga kwa mafuta tu,wakakata kata mnafu na kuchanganya pamoja na ngogwe,ingawaje vyakula hivi ni vikari lakini walitumia utaalamua wa hali ya juu kuviandaa ili kuhakikisha ya kwamba pishi lao halina dosari yoyote ya ukari,achilia mbali  pishi lao la mboga mboga kama vile mchicha, mrenda waliotia bamia magadi maharagwe pamoja na mboga mboga za majani,pamoja na hayo yote walipika njegere kavu choroko kavu na kunde kavu……..ama kweli vyakula bora ni dawa kwani ushindani ulikua ni mkari.


Na pishi walilolimalizia lilikua ni utengenezaji wa matunda. Matunda yao yalikua ni mchanganyiko wa vipande vipande vya carrot,maembe,hoho,nyanya,vitunguu,ndizi za kuiva,matikiti maji,rimon,matango,maparachichi,matunda damu, na maembe baadhi ya matunda waliyachanganya changanya na na mengine waliyakata kata hivyo hivyo tu na kuyaifadhi kwenye vyombo maalumu safi.


Hakika hadhira ilifurahishwa sana na juhudi nguvu na uwezo wa kubuni mambo mazuri ya jikoni yaliyofanywa na kundi hili watu wengi sana waliwapigia makofi na kuwapatia kura nyingi sana kundi la SIMBA JIKEZI NA SIMBA DUMEZ,wali wapooza kwa kuwaambia maneno mataamu ya kuwatoa nyoka mapangoni kwamba ushindi ni wao bahati yao imegonga mlangoni wala wasiiache ikapita na kwenda zake.


Kundi la mwisho ambalo ndilo alilokuwepo boga talenter pamoja na pamera,lililojurikana kwa jina la HAMTUWEZI wakapita ukumbini kama vile rocket iendayo kwa kasi ya mkorea,hawakua na haja ya kupita kama vile vinyonga wenye njaa,ingawaje hawakuleta mvuto kwa hadhira ile kundi ili lilijaa vijana wenye aibu na soni ila tu baadhi yao walikua super  wana nyota za mvuto.


Walichofanya wao  kama kundi walikubaliana kuandaa chakula cha jioni kwanza. Pilau iliyo sheheheni  viazi mviringo pamoja na nyama nzito ya bata mzinga pamoja na kuku aina ya kanga  zilipikwa vikanukia sana hadi hadhira ikaanza kumezea mate harufu tu ilitosha kushibisha ile hadhira. Walipomaliza shughuri ile wakaunganisha na wali mweupe uliotiwa nazi,carrot,maharagwe na pia wakakoleza kwa kutia asali iliyoogeza utamu hadi kwenye visogo vya hadhira.


Pishi la pili lilikua ni pishi la spagget  au kwa jina lingine tambi hapa napo waliwashangaza watu kwa maajabu yao makuu waliyo ya fanya kwani watu wengi sana hawakujua jinsi ya kupika spagett sasa siku ile waliamini kuwa duniani kuna  watu wataalamu na wajuzi wa mapishi.Kwanza  spagget au tambi zikakatwa katwa vipande kisha zikatiwa kwenye maziwa yaliyokua yanachemka baada ya kuiva zikakaangwa kwenye mafuta na baada ya shughuri ile pevu spagget zikawekwa karrot zilizo sagwa vizuri pamoja na vitunguu na baada ya pishi ilo tamu likapalilizwa kwa mboga mboga za majani juu yake wakaweka maua yalonukia na kuvutia.


Walipolimaliza ilo pishi safari hii wakaunganisha na pishi la vitafunwa vya staftahi hapa washiriki wakalipa jina ili pishi siku njema ionekayo asubuhi,wakachanganya unga wa bakery kidogo wakatia na unga wa ngano,keki ilotiwa chocollate ikaandaliwa,mkate mtamu wa ngano sijui wanaita BUMUNDA likapikwa, maandazi aina ya donate yakawekwa pale mezani,vipande vya bisscut na karanga za kukaangwa  zikawekwa kwenye sahani ndogo ndogo ziitwazo visosa.Hawakusahau kutengeneza chai ya maziwa,ya rangi, ya kahawa naya cocoa.


Wakapewa tena nafasi ya kuandaa  pishi la mwisho hawakua nyuma katika kuandaa pilipili ya kiutamaduni wao waliipachika jina la  traditionar peeper hii ndio pilipili inayotengenezwa kwa kusaga nyanya  kwa kutumia mashine maharumu ya kusagia,mpaka nyanya zinakua kama maji maji,wakachanganya pilipili iliyoitwa pilipili mbuzi kisha wakachanganya na pilipili moja kari kwa jina la pili pili  kichaa.


Amakweli kazi ya mapishi ni kazi ngumu sana zio kazi ya kuwaachia wanawake tu waishughurikie wakiwa Nyumbani bali ni kazi inayoitaji ushirikiano kati ya mwanaume na mwanamke,kwani umoja ni nguvu utengano ni udhaifu,zoezi ili gumu utadhania watu wana ng’oa mlima Kilimanjaro kwa mikono yao likaisha vizuri sana.


Msemachocote(Mc)wa siku ile ndugu Masanja Mkandamizaji aliwapongeza sana washiriki wote kwa jinsi walivyoonesha


juhudi zao,nguvu ushirikiano pamoja na uwezo wa kiubunifu kwani utaalamu walo uonesha ulitosha kudhihirisha kuwa  wapo juu kinoma.pia aliwapa pole kwa kazi nzito kama ile akawatia mioyo kuwa wavumilivu kwani ni hadhira pamoja ma majaji ndio walikua na haki ya kusema neno la mwisho

“ wewe bakia au wewe ondoka”

ni aina gani ya mapishi ina changamoto,udhaifu,au mapungufu, ni aina gani ya chakula kina radha,tija,harufu,afya,unono utaamu na pia je kinapendeza kuliwa au la hasha.


Hadhira(watazamaji au wasikilizaji au mashabiki)ikaitwa mbele ili kuanza kufanya utafiti wao kwa kila chakula, makundi yote yakawekwa pembeni ili kupisha hadhira kujipakulia kujichotea kujimiminia na kujichana kwa kujilia mautamu yale yalo andaliwa pia kuchangia mawazo kwa kutoa changamoto mapungufu na madhaifu ya kundi husika.Kundi la Harder to touch likapewa nafasi ya kuonesha utamu wa manjonjonjo yao hadhira iliyokuwepo pale haikusita kusema kuwa  chumvi haikutiwa kwenye chakula aina ya loshoro na pia nyanya


hazikuwekwa kwenye  kwenye maharagwe,ingawaje walijitetea kwa kusema kwamba maharagwe yakitiwa nyanya yanaweza kuchacha ilo nalo likaibua maswali mbele ya hadira wapo waliokubali na wapo waliopinga vikari.


Kundila pili nalo likafanyiwa assessment kundi ili lilibahatika kupita paso udhaifu wowote la tatu na la nne nalo  yakafanyiwa research yote yaliibuka paso matatizo kundi la tano pia halikua na any problem lakini watu walilitilia mashaka kundi la sita ingawaje halikua na kasoro nyingi sana  ila tu hadhira haikuona kama kundi ili lina mchango mkubwa kwenye mapishi yake.


Msema chochote akaishukuru sana hadira kwa ushirikiano waliouonesha katika kufaidi na kutoa mawazo yao kulingana na changamoto au pongezi la pishi la kundi husika,kundi la pili na la tatu,la nne na la tano yakapongezwa zaidi ila kundi la  la kwanza na la sita yakawekwa kikaangoni sasa ikawa ni zamu ya hadhira, kupiga kura ili kuangalia kati ya makundi hayo mawili kundi la Harder to touch na kundi la Hamtuwezi ni lipi lifungashe virago ili liyaage mashindano yale hadimu.


Mamia ya watazamaji wakapewa nafsi ya kupiga kura vipande vidogo vidogo vya karatasi vikaretwa na kila mtu pasipo ubaguzi wowote alipewa nafasi ya kuandika ni kundi gani kati ya harder to touch na la hamtuwezi yalifaa kufungasha virago vyake na kuondoka.hadhira wakapiga kura zile kimya kimya na baaada ya kumalizia  upigaji wa kura zile zikapelekwa kwenye panel ya majaji sita wa hayo mashindano,panel ikakaa kuhesabu kura  mbele ya wahusika wote na watazamaji wote.


Kwenye meza ile ya panel ya majajaji  walikaa watu maharufu Tanzania bara na visiwani  Zanzibar achilia mbali umashuhuri wao ulivuka mipaka mpaka nchi mbali mbali za Africa mashariki na Africa ya kati ,Kenya Uganda Rwanda Burundi Zaire Malawi na Zambia.Pannel ile wali upande wa kuria  kiti cha kwanza alikaa mtangazaji maharufu kwenye kipindi chake kinachoenda kwa jina la MKASI na kinachorushwa na televisheni kubwa Africa mashariki


SALAMA JABIRI diva anaye wahoji na kuwatwanga maswali mawili matatu wasanii na watu maharufu Tanzania na Africa mashariki kama vile wakina Ambwene yesaya(AY) REHEMA CHARAMILA (RAY C) Mrembo wa Africa NANCY SUMARY na dadaye mwanamuzikia NAKAAYA SUMARY na wengineo wengi tu kwani hawa ni baadhi yao.


Mtu wa pili upande ule ule wa kuria alikaa MAADAM RITTA PAULSEN huyu naye alikua mahuhuri kwa kuwato wasanii mbali mbali ndani na nje ya Africa mashariki wabunifu na watu wenye vipawa pamoja na vipaji vyao  kwa kutumia kampuni yake ya BENCH MARK PRODUCTION. Bila kumsahau mwana dada wa kipindi cha  WANAWAKE LIVE kipindi kinacho onesha mabo mbalimbali ya wanawake wanavyojituma katika shughuri za kimaendereo


kiujasiliamali, mwanadada huyu mtetezi wa wanawake na watoto  alisifika sana katika kuangalia changamoto wazipatazo wana wake,migogoro inayo wakumba wana wake katika kulisukuma gurudumu la maendereo, uhusianao bora kati ya wana wake na wanaume katika ujenzi wa familia bora zaidi duniani,malezi mema kati ya mama na  mtoto na mambo mengine kem kem.si mwingine bali ni mrembo wa Africa mashariki na duniani kwote JOYCE KIRIA.


Upande wa kushoto waliketi wana ume watatu kwanza alikuwepo MASTER JAY mwanaume huyu Mwenye sura ya upole hekima aibu na wema ulo mtawala.huyu ni producer maharufu BONGO kwa kumiliki studio yake inayo kwenda kwa jina la MJ RECORDZ,achilia mbali uwepo wa master jay pia alikuwepo msomi aliye bobea katika  masuala ya michezo,elimu sanaa na utamaduni ubunifu na vipaji hakua mwingine bali ni muheshimiwa ndugu WAZIRI WA ELIMU MICHEZO NA UTAMADUNI si mwigine bali ni  PROFFESOR PATRIC MULLUNGU. Mtu almaharufu Tanzania bara na visiwani kwa hoja zake ziloshiba awapo bungeni akiitetea elimu kuwa ndio ufunguo wa maisha,ndio bahari ya mafanikio,ndio kitu kisicho na mwisho,ingawaje mwanadamu ana mwanzo na mwisho wake lakini elimu imekosa mwanzo na mwisho wake.


Na judge wa mwisho kabisa aliye keti katikati hakuwa mwingine bali ni mtu mdogo kiumbo ila ana mambo makubwa katika fani na tasnia nyinginezo za sanaa kama vile tamthiriya,filamu,maigizo, na vichekesho aina ya commedy Tanzania bara na visiwani Zanzibar .huyu ni mtu maharufu ambaye sanaa yake ipo kwenye kila kipande cha nyama zake ndani ya damu na ndani ya mishipa yake ya fahamu si mwingine bali ni msanii anaye kwnda kwa jina la KIKONGWE  JOTI ,au kama wamwitavyo watazamaji wa television ya  TBC, ASHA NGEDERE kila jicho la mwafrica umtazama asha ngedere siku ya jumataano na juma pili.


Hao ndio panel ya majaji walokaa chini na kuanza kuzi calculate zile kura  kwa uhaminifu mkubwa kwani wote walikula kiapo cha kutodanganya neno lolote wakiamini kuwa msema kweli ndie mpenzi wa Mungu kura zile zikahesabiwa alfa na omega baada ya mchakato mrefu kama vile kamba iendayo angani kuuvuta mwezi pasipo mafanikio hatimaye haki ikatangazwa.katika mchakato wa kuwapata washindi wa mashindano haya kundi la wakari classics wakapewa nafasi ya  kwanza kuwa ndio kundi bingwa kwa kuyashinda makundi yalofuati.


Kundi la samba dumezi na samba jikezi likapewa  nafsi ya pili ya ushindi kwani lilionekana limefanya poa sana mbali na hapo kundi la tatu na la nne ambapo kundi la tatu lilitwa lazima tushinde na kundi la nne lilitwa sisi ni balaa yote kwa pamoja yakapata nafsi ta tatu kwani yaliungana na kufanya kitu kimoja.pishi zao zilitia fora sana kwa mahanjumati yalotokota yalonukia yalo kua manono matamuuu yaani very delicious.


Kundi la tano la hamtuwezi liliopewa nafsi ya nne ya ushindi ingawaje kundi lile la kwanza la harder to touch lilivurunda na kupewa asilimia chache hatimaye haki ikatangazwa  kuwa kundi la harder to touch  lifungashe virago lishike njia kwa kutumia miguu yake.hatimaye kundi la harder to touch likafungasha virago kwa huzuni utadhani kinda aliye tekelezwa na mamaye kwani walimwaga kilio na kusaga meno utafikiria nafaka zinavyosagwa kwenye mashine.


Makundi yalosalia yakapongezwa sana na kupewa nafsi ya kujisukuma zaidi kwani daima mbele nyuma mwiko hiyo ndio ilokua point ya msingi......
itaenderea sehemu ya tatu
usikose......