MAPENZI TUYAPE PUMZI
Tuanze kama safari,twende mbali
tukaone,
Mapenzi yetu hatari,nimeshazama
nione,
Nitakupa hata gari mapenzi yetu
yanone.
Mapenzi tuyape pumzi,yapumue kwa
furaha.
Mapenzi tuyape pumzi yapumue kwa furaha,
tusije kuwa machizi,tukaishi kwa
karaha,
tusifanye kama wezi,tupumue kwa
furaha,
Mapenzi tuyape pumzi,yapumue kwa
furaha.
Nakupenda si utani,usiniache jamani,
Penzi lako chini chini,nitulize
kivulini,
Tusiyachome juani,tukajuta maishani,
Mapenzi tuyape pumzi yapumue kwa furaha.
Usiwafate mabuzi,wakakuchuna na
wewe,
Ukafanana na mbuzi,na sura mbaya ya
mwewe,
Penzi letu ni mchuzi ,nimedata kwako
wewe,
Mapenzi tuyape pumzi,yapumue kwa
furaha.
Jamani kipenzi changu,ninakupenda
moyoni,
Asali ya moyo wangu,sasa shubiri ya nini?,
Niponye nafasi yangu,nakupenda si
utani,
Mapenzi tuyape pumzi,yapumue kwa furaha.
Sina kinyongo moyoni,wala kiburi
usoni,
Furahaa yangu machoni ,kicheko
changu kinywani,
Papaso lako mwilini, lanipa joto
jamani
Mapenzi tuyape pumzi yapumue kwa
furaha.
No comments:
Post a Comment