SURA YA
TATU
BOGA TALENTER ANAFURAHI PAMOJA
NA PAMERA
Baada
ya kuisha kwa kazi ile ya mapishi vijana waliosalia walaanza kupongezana kwa kazi nzito waliyo ifanya.siku ile pamera
alimchukua boga talenter akaenda
kumtambulisha kwa wazazi pamoja na ndugu zake kama ni rafiki na mchumba wake
mtarajiwa kwani kabla ya hapo aliwaambia wazazi wake kuwa amepata rafiki mzuri ambaye angependa aje kuwa mume
wake siku za usoni. Wazazi ndugu marafiki na jamaa ya pamera wakafurahi sana
kumuona boga talenter kwani alikua ni kijana
mzuri haswa .penielia na penslavia dadaze
pamera wakaanza kuonesha jicho la husuda.
Roho
ya kumtamania kijana yule ilikua kwa kasi kwani boga talenter kwa utanashati
alikua yupo juu kwani katika wanaume vijana ishirini ambao wangepita mitaani
pamoja na boga talenter hakika mtu aliye watazama asingesita kumsifia boga
talenter kwa uzuri na utanashati.ni jina tu
alilopewa la boga ndilo halikumpendeza ila kwa utanashati kijana aliita
fora hata babaye usiku na mchana alijitwanga maswali yasiyo na majibu ni wapi
mtoto yule alikouta hali ile ya kuwa
bonge la handsome.
Boga
naye akamtambulsha yule mrimbwende pamera kwa
kwa babaye mzee talenter
aliyekuja muda mfupi baada ya mashindano kuanza,wote kwa pamoja walitawaliwa na
nyuso za furahaa ya ajabu.
Siku
ile pamera aliona kuwa uchovu ni mwingi sana ndani ya mwili wake kwani kazi
waliyoifanya ilikua ni kazi nzito na ya kufa mtu,akamwomba boga waende ufukweni
mwa bahari ya hindi kujipumzisha .huko
nako walipofika michezo mbalimbali ilienderea mchezo ambao ulikua ni mgumu sana
kwa boga ulikua ni kuogelea boga hakujua kuogelea hata kidogo alipata shida
sana ya kucheza na maji pamera alipoona udhaifu ule wa boga akaanza kumfundisha
taratibu kwa kutumia mipira maalumu ya kuogelea na maboya ya gari hali ambayo
boga talenter alifurahia zaidi.
Jioni
ya siku ile pamera alimpeleka boga sehemu nzuri ya MLIMANI CITY CINEMA ili kucheki muvi firamu na tamthiriya, sinema
iliyo mvutia sana boga talenter ni sinema ya marehemu STEVEN CHARLES KANUMBA
ilitoitwa ANKO JJ kwani msanii
aliwakonga sana mioyo watazamaji kwa
kipaji chake alicho kionesha jioni ile wakacheki tamthiriya moja ya kikorea iliyo kwenda kwa
jina la JUMONG na wakamalizia kwa firamu
tamu ya mwana dada aliye chipuka kwenye muvi ya FOOLISH AGE wala si mwingine
bali ni ELIZABETH MICHAELI au LULU.
Achilia
mbali kumpeleka boga talenter sehemu
nzuri ya mlimani city cinema binti yule
wa tajiri alimpeleka boga talenter hoter
moja yenye hadhi Ya kimataifa inayoitwa
NYUMBANI LODGE hoter ya mwanamuziki wa
kimataifa LADY JAY DEE. Wakaagiza supper ya kinywaji cha maziwa mazito
CAPPUCCINO kwa utamu ule hata boga aliona
ajirambe mikono kama mtoto mdogo kwani hakuwai kuonja vitamu tamu vya
hoterini,baada ya supper yao kuisha wakaagiza na dinner iliyo sheheni wali kwa
kuku wawili wazima pamoja na juice ya ya
matunda.
Siku
ile kulikua na ugeni wa wanamuziki kutoka mwambao MZEE YUSSUPH na ISHAA
RAMADHANI almaharufu kwa jina la ISHAA MASHAUZI , wanamuziki wale wa nyimbo za
TAARABU walitumbuiza nyimbo zao zilizo wakonga watazamaji kama vile MAMA NIPE
RADHI.ukumbi wote ulibakia kupiga kelele za nderemo na vifijo sio isha mashauzi
tu na bendi yake ya mashauzi classics pia mwanadada lady jay dee akiwa na bend
yake ya machozi aliwapagawisha wapenda
starehe kwa wimbo wake wa YAHAYA. Hakika siku ile ilikua ni siku ya burudani tosha kwa vijana hawa wawili.
Usiku
mnene ulipoingia pamera akamwomba boga talenter wakodishe chumba hoterini ili
walale pale pale lakini boga alisita kwani hakumwaga babaye mzee talenter hivyo
aliingiwa na hofu kuwa mzee wake anaweza kumtafuta kuwa na wasi wasi na mahari alipoenda boga
talenter.
Pamera
akamrudisha boga talenter Nyumbani kwao kisha na yeye akarejea Nyumbani kwa
wazazi wake ilikupumzisha kichwa ubongo
na akili kwani mc masanja aliwatangazia
washiriki kuwa walitakiwa kujiandaa na shindano jingine bab kubwa la fashen
show baaada ya siku tatu zijazo
No comments:
Post a Comment