Thursday, November 26, 2015

MPENDE AKUPENDAE
Haya ni mambo machache, yaliyo kwenye mapenzi,
Usiyempenda muache, mpende taye kuenzi,
Maana wengine vicheche, wanapendea ushenzi,
Mpende akupendae, usiempenda mtende.

Mapenzi yamebadilika, siye kama ya zamani,
Wivu umejishagubika, sasa atuamiani,
Michepuko wanataka, hawaitaki foleni,
Mpende akupendae, usiempenda mtende.

Ukipata mtulize, hebu mshukuru mungu,
Usianze ona wivu, wakakupiku wazungu,
Tena asiwe mvivu, kwenye kuchezea rungu,
Mpende akupendae, usiempenda mtende.

Mnunulie zawadi, yeyote aitakayo,
Pia mpe na ahadi, akuifadhi kwa moyo,
Penzi utalifaidi, ukimuweka kumoyo,
Mpende akupendae, usiempenda mtende.

Msiwe kama zamani, kila siku malumbano,
Kujifungia chumbani, na kupeana vibano,
Sasa acheni utani, pendeni mshikamano,
Mpende akupendae, usiempenda mtende.

Dada mpende mwenzio, kaka fanya hivyo pia,
Usimuuzi mwenzio, bahati ikapotea,
Na usijetoa kilio, pindi atapokimbia,
Mpende akupendae, usiempenda mtende.

Sasa kaeni pamoja, na wala msiachane,
Msianze jenga hoja, na mwishoni mgombane,
Kuweni tu na umoja, wapenzi na mpendane,
Mpende akupendae, usiempenda mtende.


.UKISHA PENDAGA BOGA.
Nikikumbuka ninalia, kwani nilimzoea,
Moyoni ninaumia, ninapomfikiria,
Mawazo yananijia, vema kuyapotezea,
Ukishalipenda boga, ulipende na ua lake.

Ni kweli alinipenda, na pete kanipatia,
Na shangaa kanitenda, sababu ajizushia,
Eti mimi sikumlinda, virusi kumpatia,
Ukishalipenda boga, ulipende na ua lake.

Ilikua kama zali, mimi nilipo muambia,
Kutokana na dalili, nilienda kujipimia,
Majibu ya dakitali, mimi niliyapokea,
Ukishalipenda boga, ulipende na ua lake.

Tuliporudi nyumbani, ugomvi ajiaanzia,
Eti mimi ni shetani, kaburini ninamtia,
Mara mimi ni muhuni, akhera aingojea,
Ukishalipenda boga, ulipende na ua lake.

Ni kweli alifungasha, nami akanikimbia,
Na moto aliuwasha, virusi vikaenea,
Aliye mkaribisha, virusi alimgea,
Ukishalipenda boga, ulipende na ua lake.

Watu waliangamia, jamii ukoo pia,
Na kinga hakutumia, ugonjwa ukaenea,
Kinga(dawa)zimemuishia, kabaki kujikondea,
Ukishalipenda boga, ulipende na ua lake.

Mimi najinenepea, na dawa nazitumia,
Masharti najifatia, dokta alonambia,
Huruma na muonea, kwani ameshajifia,
Ukishlipenda boga, ulipende na ua lake.


WAWILI TUNAPENDANA

Wawili tunapendana, kama mnavyotuona,
Katu hatuta achana, tumeshapendana sana,
Umizeni vyenu vichwa, kwa maneno na umbea,
Wawili tunapendana, wala msitujadili,

Kila siku twafurahi, amani tele nyumbani,
Kila muda twafurahi, wala hakuna huzuni,
Pamoja tukifurahi, watu huwa na huzuni,
Wawili tunapendana, wala msitujadili.

Sisi tunavyopendana, jama hamna kifani,
Tena twashirikiana, na sote tunafurahi,
Sisi tunapokutana, kwa mapenzi twajidai,
Wawili tunapendana, wala msitujadili,

Tukiwa mepumzika, pamoja tukifurahi,
Tena watu waudhika, pale tunapojidai,
Tena wana hangaika, kulivunja kwa jinai,
Wawili tunapendana, wala msitujadili.

Pendo letu twalitunza, kamwe lisiharibike,
Hata walitie funza, ili lije haribike,
Pamoja tunalitunza, kamwe lisiharibike,
Wawili tunapendana, wala msitujadili

No comments:

Post a Comment