Sunday, November 29, 2015

HICHO KIPAJI ULAJI
HICHO KIPAJI ULAJI,
MSHAIRI KAMA JAJI,
UKITUMIA UJUZI,...
FANYAYAKO MAPINDUZI.

YAPO MADARAJA CHINI,
YAKULA MOJA SAHANI,
WEWE KAMA MSHAIRI,
WATETEE KWA USHAURI,
YAPO MADARAJA JUU,
YANAYOPENDA MAKUU,
WENGINE NI VIONGOZI,
LAKINI NI MABAZAZI.
WEWE KAMA MJASIRI,
FICHUA ZA KWAOSIRI,
HICHO KIPAJI ULAJI,
MSHAIRI KAMA JAJI,
HICHO KIPAJIA UAJI,
TUMIA KWA MAUAJI,
UMASIKINI NA UJINGA,
MAGONJWA TAFUTA KINGA.
WATAZAME WAKULIMA,
TANGU ZAMA ZA UJIMAA,
WANALILIA MBOLEA,
YA SAMADI NA UREA.
MASOKO NAYO MAJEMBE,
ILI WALIME MAEMBE,
LAKINI KIPI WAMEEKOSEA,
FAIDA INAPOPOTEA.
MATAJIRI WENYE MALI,
WAPO WENGI SERIKALI,,
WANASURA ZA UKAFIL,
MAFISADI NA JEURI.
RUSHWA PAMOJA MAGENDO,
WAMEKOSEA UZALENDO,
FICHUA ZA KWAO SIRI,
NA KUWACHIMBIA KABURI.
HICHO KIPAJI ULAJI,
KIPAJI KANDAMIZAJI,
UKIFANYIE RISECHI,
KUMWOKOA MWANANCHI.
MYONGE NA MASIKINI,
WA MJINI NA KIJIJINI,
USISUBIRI NGOJA NGOJA,
JENGA ZAKO NGUVU HOJA.
VIONGOZI WAKIKUJA,
WATAULIZA MOJA MOJA,
KATOKAPI HUYO KIJAA,
MWENYE KIPAJI ULAJI.

No comments:

Post a Comment