“NILITEMBELEWA NA MALAIKA”
Sura ya kwanza
Kwenye kijito cha maji
Ilikua Yapata saa nane na nusu mchana siku ya juma mosi mwezi desember tarehe 25 mwaka 2010 ilikua ni siku
nzuri sana kwa upande wangu,sio tu kwa upande wangu nadhani labda hata kwa watu
wengine wengi waliopo duniani, kwani tarehe hiyo katika historia ya dunia ni tarehe maalumu na
muhimu kwa ajiri ya kusherehekea
kufurahia,kushangiria na kuburudikia sherehe ya kuzaliwa kwa bwana wetu na mwokozi
wetu yesu kristo mwana wa pekee kwa mungu baba kama imani ya wkristo wengi
duniani ilivyo.
Hali ya hewa
ilibadirika ghafra kukawa mkusanyiko na
mawingu mawingu meusi meusi yaliyo ambatana na upepo mkubwa kiasi ulio kua
ukivuma kwa madaha na maringo kwa hali kama ile wahenga wetu walisema dalili ya
mvua ni mawingu,naam mvua ilikua inataka kunyesha na mvua ya siku ile haikua
mvua ya kitoto bali ni mvua ya nguvu. Kila mtu aliye yazoea majira ya mwezi desember haswa haswa kipindi
cha sherehe za chirstmass alitegemea na alitarajia kwamba mvua kubwa kama ile
ingenyesha tu kwani ndio kawaida ya mvua hizi kunyesha huku kwetu Mbeya na kufanya mito na vijito kufurika maji
machafu yaendayo safari za mbali kusiko julikana.
Watoto wengi
wa matajiri walitia fora siku ile kwa kuvaa viwalo vipya vya bei gharama sio tu
watoto wa matajiri na hata wale wanaotoka katika familia za hali ya chini
hawakua nyuma kujichagulia viwalo mbali mbali katika mabanda ya nguo za mituumba nguo maarufu sana huku kwetu
mbeya, kwani hizi ni nguo zenye sifa ya kipekee
sana hizi ni nguo zinazo aminika kuwaziliwahi tumika au ziliachwa na wazungu wa huko ulaya au nchi nyingine
zenye viwanda ili ziuzwe kwa bei ya
chini.
Ni hali
kawaida sana kwa watoto kupenda kuvaa nguo mpya kila msimu wa sikukuu hizi
za Noeli na mwaka mpya,tofauti na watu
wazima ambao wamezoea kuvaa kikawaida kawaida tu kwani wao awana shida na
mavazi kwao mavazi ni kila siku hununua na kuyavaa mapyakwa mtindo wa
kubadirisha badirisha.Sherehe zilinoga zikanogera,zilipendeza
zikapendeka,zilivutia zikavutika, watu walikunywa,walikula na kusaza,watu wengine
walitembea au kutembelehana na kupeana zawadi pamoja na heri ya Noeli.
wakiusubiria
mwaka mpya kwa hamu kuu mfano wa wanawali sita walio hadithiwa katika kitabu
cha mathayo; wakimgoja bwana harusi
ambaye ni yesu hata pale alipotokea walifurahi pamoja na kufanya sherehe.hapo ndipo tunapaswa
kutambua kua imetupasa kusubiri kwani subira yavuta heri na iwapo tutakua na haraka haraka tutakosa
Baraka.
Mara baada ya mimi kupachika kinywani mwangu matonge mawili matatu ya pilau na nyama
ya kuku pamoja na juice ya embe lenye mchanganyiko wa carrot na matango nilijisikia kushiba kwa
kiasi kikubwa palenyumbani kwetu Nikanyanyuka kiuvivu uvivu kutoka kwenye
kigoda,kigoda alichozoea kukikalia bibi yangu
aliye mzaa mama yangu, na baada ya kujinyanyua taaratibu niliingia
chumbani kwangu na hata nilipo fika ndani ya kile kijumba nyasi chetu utusi tusi na giza giza la mule chumbani
vilinifanyanishindwe kuliona vema gitaa langu nililolilihifadhi kwenye kona ya
chumba changu cha kulala karibu karibu na kitanda changu nadhifu kinachonipendeza.
Nilianza
kupapasa papasa ukuta ili kuelekea eneo ambalo gitaa langu lilikuwepo na kwa
bahati nzuri mikono yangu iliweza kuligusa
na kulichukua na kisha baada ya kutoka
nje ya kile chumba changu kizuri kinachonipendeza,najivunia kusema kuwa chumba changu knanipendeza kwa sababu ni cha kwangu
na pia binafsi nakipenda kwani sio mbaya mtu kukipenda au kuipenda mali yake
hapo ndipo ule usemi wa chako ni chako cha mtu sio chako au ule usemi usemao
kipende sana chako kwani cha mtu ni mavi semi hizi zinaambatana na ile semi
niipendayo sana maishani mwangu “mjasiri hawezi kuiacha asili” zilinijia ndani
ya kichwa changu kimawazo sikujari sana
nilianza kutoka ndani ya kile chumba changu nikiwa na lengo la kwenda sehemu
moja tulivu niliyo izowea siku zote kwa ajiri ya kupumzika na kuyabadirisha
mawazo pamoja na fikra zangu.
Ndio ni
mawazo yangu,na mengi ya mawazo hayo nilizoea kuwaza kuhusu maisha,maisha ya kijijini,mawazo
kuhusu kilimo chetu kitukufu cha mahindi
yatuleteayo unga wa ugali,maharagwe yetu
yatuleteayo mboga mboga ya majani ambayo kwetu tunaiita ‘’nguniani’’,karanga
pamoja na alizeti zituleteazo mafuta na
masalia ya haya maalizeti yanatuletea mabaki mabaki taka yake
tunayo yahita mashudu na hayo mashudu ni chakula kitamu sana kwa wanyama
kama vile ngombe na mbuzi pamoja na ndege wetu kuku na bata.sio mazao hayo tu
bali hapa kijijini kwetu mbozi tumejaliwa Baraka tele za mazao mbali mbali ya
chakula na biashara.
Nilienderea
kuwaza
Mawazo
kuhusu nyuki watuleteao asali na sukari, mawazo kuhusu miti ya matunda matamu
kama yale ya mabhohora,mapera,mafyurisi,makatapera au waswahili wayaitavyo maparachichi,mahembe,mapeasi,ndizi
sukari,mananasi,matunda damu na matunda mengine mengi sana.
Nilisongwa
songwa na mawazo siku zote za maisha yangu ya kijijini,nikiamini kuwa jembe
halimtupi mkulima,hapo ndipo nilijipa matumaini ya kufanya shughuri za kilimo
na ufugaji kwa juhudi zangu kubwa mno.Ni ukweli usiopingika na usio pimika pale
wazee wetu wa kijijini walipo tuhusia tusikidharau kilimo daima wazee wetu walitujaza
elimu ya kilimo pamoja na ufugaji wakatuambia kwamba kilimo ndio utii wa mgongo kwa
mwanadamu,asihelima na wala asipewe chakula kwani mdharau jembe si mkulima na
huyo mdharau jembe nyumbani kwake hakuna chakula kwa hali hiyo kilimo kwetu ni kazi moja wapo tukufu kazi tunayo ienzi ili kujega nchi ya kijamaa.
Tunalima
viazi mbatata pamoja na viazi
mviringo,tunalima kunde,mbaazi pamoja na mtama,tuna mashamba ya miwa,migomba ya
ndizi sukari pamoja na ndizi zile ziitwazo matoke,hatujapungukiwa kitu chochote
kiitwacho chakula hapa kijijini kwetu mbozi na mkoa wetu wa mbeya,mkoa
mashuhuri kwa wingi wa tani za chakula cha nyumbani na biashara.nilizoea sana
kuwaza kuhusu kilimo pamoja na ufugaji wa wanyama kama vile
mbuzi,ngombe,nguruwe,kondoo na mifugo mingine mingi tu ambayo mwenyezi mungu
ametujalia.
Nilijikongoja
kongoja taaratibu na kueleke mtoni,mkono wangu wa kulia nili likamata gitaa
langu la nyuzi,gitaa nililolitengeneza mimi mwenyewe kwa ubunifu na kwa kipaji
changu,japokua mimi sio mtaalamu wa masuala ya muziki ila niseme ukweli napenda
sana muziki napenda kuimba kucheza na pia naweza kutunga nyimbo nzuri na tamu
zinazohusu masuala ya mapenzi,siasa na za dini sanasana zile za kumsifu yesu
kristo mkombozi wetu aliye tufia pale msalabani kwa sababu ya zambi zetu,makosa
yetu na hatia zetu.
Nilipo kua njiani natembea kwenda
mtoni,taaratibu na kwa uangalifu mkubwa ili nisije kuchomwa na miiba au
kungatwa na nyoka wa porini,kwani siku zote mimi pamoja na marafki zangu
tumezoea kutembea peku peku popote pale tunapo kwenda, na jambo hili ni kama
utamaduni wetu kwa sisi watu wa kijijini,moyoni mwangu nilikua najiimbia
wimbo ambao niliubuni kichwani mwangu
muda ule ule nilio kua natembea kwenda kwenye kijito cha maji.
‘’ Zambi
zetu pamoja na hatia,
Zambi zetu pamoja na makosa,
Mwenyezi
mungu ametuhaidi,
Atatusamehe
milele daima.
Ila tu iwapo
tutamkufuru,
Mwenyezi mungu hawezi kutusamehe,
Imetupasa tusienderehe kutenda
zambi,
Makosa
,hatia na kufuru,
Bali tumwombe mungu atusamehe.
Nikaenderea
kuimba moyoni mwangu, huku nikitembea taaratibu;
Utusamehe makosa yetu,
Utusamehe zambi na hatia,
Utusamehe bwana yesu
Utusamehe milele daima…….”
Nilifika
mtoni mvua nayo ilienderea kutima,sikujari sana kama ningelowana au ningepatwa
na homa kari kutokana na ubaridi wa mvua ile,sikujari hilo kwani mimi na mvua ni mtu na rafiki yake,naipenda
sana mvua,napenda maji yake matukufu yatokayo juu mbinguni,napenda sana kila
niisikiapo ikilia juu ya makuti na
manyasi ya kijumba chetu,napenda sana kila nitizama mazao yetu yanavyo sitawi
yanavyo mea na yanavyo kua kwa kasi kwa sababu ya uwepo wa mvua,natambua kua
maji ni uhai pasipo maji binadamu hana uhai,pasipo maji mimea na wanyama wa
kufugwa au wa mwituni au wa majini hawawezi kuishi .
Mvua kwangu
ni rafiki yangu,ni mpenzi wangu na mwandani wangu,mimi na mvua ni chaunda chema
kivikwacho pete,mimi na mvua hakika ni kidole na pete,tunapendana,na leo naiona
mvua kubwa ya rasha rasha,inavuma pamoja na kusindikizwa kwa nguvu za upepo
mkari,hilo siliogopi kwani najua kua mpenzi wangu mvua amekuja kwa faida yangu
na pia kwa faida ya watu wote duniani pamoja na viumbe wengine wa porini au
majini.niwe mkweli na muwazi ndugu zangu tusihizarau mvua mvua ni uhai wa dunia
hii wapo ambao kwao mvua ni kitu nadra sana kupatikana,wapo ambao wanaishi
kwenye majangwa ya kiu ya kukosa hata matone ya maji na maji yenyewe ni haya
haya ya mvua,iweje sisi tuliobarikiwa
kwa uwepo wa mvua tunaidharau na kuona kuwa inatubugudhi.
Sikatai
kusema kwamba aisifuye sana mvua inaweza ikamyea,ndio ni kweli kuwa mpenzi
wangu mvua ana madhara yake mengi tu,japokua sina dhumuni lengo au haja ya
kueleza madhara yatokanayo na uwepo wa mpenzi wangu mvua,lakini pia ni vema na
itapendeza sana ikiwa sisi kama sisi tutajitahidi kuifadhi vyanzo vya mvua
pamoja na kuyahifadhi maji yatokanayo na mvua ili yaje kutusaidia kwenye maisha
yetu ya baadae kwani sisi binafsi hatujui yatakayojiri baadaye mara tutakapo idharau mvua ni
mwenyezi mungu pekee ajuaye yale mambo yote yaitwayo “future event”..
Mvua
ilienderea kutima,ikanilowanisha mwili wangu wote ikalowanisha gitaa
langu,nilijihisi kama vile nabarikiwa
kwa kubatizwa mar azote niwapo
katikati ya maji ya mvua,macho yangu yalilowana,nguo zangu zililowana tipwa
tipw,nywere zangu ndefu zililowana shagharabagha,gitaa langu bado lilikua lipo
“stable”linanguvu ya kuimiri yale mawe mawe yatokayo juu kwa sababu ya barafu
ya mvua.taaratibu nilizigusa nyuzi za gitaa langu na taaratibu nilianza
kulikunguta,kulicharaza na kuliponda ponda gitaa langu kwa vidole vyangu virefu
katika mikono yangu.
Mvua
ilienderea,ikaenderea na kuenderea bila kukomaa na mimi kadri mvua ilivyozidi
kuninyea nilipandwa na hisia kari sana mara baada ya kuanza kuimba wimbo wangu
mtamu niupendao kila siku,na wimbo niuimbao usiku na mchana,pasipo kuchoka;
Kwenye
kijito cha maji,hapo naoga,
Maji safi
yatokayo,yatokayo mbinguni,
Kwenye
kijito cha maji,kuna damu ya yesu
Imenisafisha
zambi,imeniponya magonjwa.
Kwenye
kijito cha maji,njoni ndugu zangu,
Njoni
tuhogerehe,maji safi yatokayo,
Yatokayo
mbinguni,kuna damu yesu
Atatusafisha
zambi atatuponya magonjwa….
Hisia zangu
zikanivuta nienderehe kuimba ,nami kwa vile nimejariwa kipaji cha kumwimbia na
kumsifu mwenyezi mungu nikaughani wimbo mwingine.
Nataka,nataka,nataka,nataka,nataka
Nataka
kumjua mungu,nataka nataka
Nataka
kumjua mungu,nataka,nataka,
Nataka kujua
mapendo yake,nataka,nataka,
Nataka kujua
rehema zake,nataka,nataka
Nataka kujua
nehema zake nataka nataka
Nataka
nataka,nataka,nataka,nataka,nataka
Nataka,nataka,nataka,nataka,nataka,nataka
Amenipenda
bwana,nataka,nataka,
Amenivuta
kwake,nataka,nataka nataka
Ameniita yesu,nataka
nataka
Na kadri nilivyo
zidi kuimba wimbo wangu ule mtamu,hisia zangu zilizidi kupanda na sauti yangu
ilipanda na kushuka ,ilipanda kwenda juu mbinguni,ikashuka kuja duniani na nina
uhakika mkubwa kwamba watu wengi sana katika kijiji chetu walisikia jinsi
nilivyo kua naimba,kwani ni kawaida yangu kuimba kwa sauti ambayo wanakijiji
huisikia vema,na mara nyingi hawasiti kunisifu au kunipongeza kwa sababu ya kua
na sauti tamu sauti nzuri ya kuwatoa nyoka, mapangoni.
Mara baada
ya kuimba ule wimbo wngu kwa kurudia rudia
mara nyingi zaidi,nilishusha pumzi zngu ndefu nikapepesa pepesa macho
yangu huku na uko kushoto na kuria
katika kijito kile name nikaona jiwe
moja kubwa la chuma lipo hapo upande wa kuume kisha nikajivuta jivuta taaratibu kwa kujilazimisha mfano wa kinyonga
anae tembea na baada ya kufika kunako
ilo jiwe nilijikarisha kimatanga nikiwa nakitamani kughani wimbo mwingine ndani
ya moyo wangu.
Ghafra mvua
ika stop kuenderea kutima na kustop kule
kulikua ni kama tukio la ghafra mno tukio lililonifumbua mdomo wangu na kunifanya
nipigwe na mshangao kwani sikujielewa elewa kwa nini nipo katika hali ile,hali
ya kunishangaza na kunigeuza bumbuwazi.mwili wangu ulikua umekauka kau kama
vile nilipigwa na jua la saa sita kwa
muda mrefu,nguo zangu nazo zilikua zimekaukaa na kuwa kama vile zilianikwa
kwenye jua kwa muda mrefu,sio nguo na mwili wangu tu,bali hata gitaa langu nalo
lilikua limekaukaa kau acilia mbali neo ambalo nilikuwepo hapo mwanzo lilijaa
matope matope pamoja na mrundiko wa maji machafu lakini sasa lilikua ni eneo
ambalo limekauka limeota nyasi na kutoa maua maua,nilijisha ngaa na nilishangaa
eneo lile,sikuelewa na wala sikujielewa elewa nilibaki kujiuliza kwa sekunde
kaza nini kimetokea?kuna nini ?je naota au ni kweli?mbona sielewi.
Nikiwa bado
nimepigwa na butwaa nilisikia mlio wa sauti kubwa pamoja na miungurumo ya radi
kari,radi ambayo hakika katika maisha yangu sijawahi pata kuisikia ,kwani
ilikua ni radi moja yenye mlio mkari sana,mlio ambao hakika wewe ndugu msomaji
kama ungepata kuisikia ilke sauti ndani ya sekun de chache ungekua uhu marehemu safari yako ya kwenda kumwona bwana
yesu juu mbinguni ingekua karibu kutimia,lakini namshukuru mungu nipo hai
sikuona madhara yoyote ya pasuko la ile radi.
Nikiwa bado
naenderea kupigwa na butwaa mahari pale kwenye kijito cha maji nilikuja
kuisikia sauti moja ya mwanamke,ikininongoneza
kunako masikio yangu na kunongoneza huko
kulikua ni kwa taaratibu.nikasikia sauti
ya mwanamke huyu ,mwanamke mtu mzima ikiniambia;
“Tizama juu”
Nami nikaitii
ile sauti,sauti laini na nyororo,,nikatizama juu ilikuona ni nini ambacho
napaswa kukiona
Sikuona kitu
zaidi ya mawingu mawingu yale yaliyo jikusanya kuanza kujikunjua kunjua na
kuacha anga la bluu.ndipo nikayashusha
macho yangu chini ya aridhi
Moyo wangu
ukaniulza tena
“je umeona nini”.
Name
nikaujibu moyo wangu kwa heshima zangu zote na taadhima
“nimeona
mawingu mawingu meupe yakijitawanya tawanya na kuliacha anga la buluu”
Kisha moyo
wangu ukaenderea kusema.
“ Umejibu
vema Tizama tena anga la juu”
Mvua ilikoma
kwa muda ule,muda ambao binafsi niliona kama ni miujiza au mauza uza
flani fulani,yakitendeka mahari pale nilipokua nimesimama bado sikuelewa
nini maana ya mabadiriko yale, nikajisemea kimoyo moyo au je ninaota, na je
ninaota ndoto za mchana, la hasha!! Moyo wangu ukanijibu,hauoti ndoto za mchana
ni kweli haya yote unayoyashuudia yana tokea.
Nikatizama tena
juu ya anga la dunia.
hapo ndipo
woga hofu na kutetemeka kukanivamia sana,tetemeko langu lilikua ni kama vile
napigwa na nguvu furani za umeme,nguvu ambazo ziliinyonya damu yangu yote na
kunikausha mwili wangu wote na mwili huo nilihisi umekauka kama mfano wa gogo
au mti mmoja mgumu uliokaushwa na jua.niliogopa nikatamani kukimbia,nilihofu
almanusura haja zangu zote kubwa na ndogo zinitokee kwa pamoja,niliogopa kwa
sababu ilikua ni mara yangu ya kwanza kukumbana na hali ile.
Nikauinua
mguu wangu wa kushoto lakini mguu huo haukuweza kuamka,nikauinua mguu wangu wa
kulia vivyo hivyo mguu wangu wa kulia nao haukutaka kusimama,mpango wangu wa
kukimbia ulishindikana,nikajiona kama nipo katikati ya kifo nipo njia panda
wala sijui ni wapi pa kukimbilia.
Juu ya lile
anga la ubuluu ubuluu wa rangi iliyokorea
alisimama mwanamke,mtu mzima wa makamo,mnene na unene wake ni unene wa mtu
mzima,mrefu ameachia tabasmu mdomoni mwake,na tabasamu ilo halimtoki kwa muda
wote tangu namtia machoni pangu,ni wa rangi ya chungwa lililoivaa haswa au waswahili
wa kisasa wao wanaita ngozi ya kizungu,nywere zake ndefu nyeusi tii zenye mg’aro
kichwani mwake.amevaa mavazi meupe na weupe wake ni weupe ajabu hakuna mavazi
kama yale duniani popote,nilienderea kumtizama huku nikiwa na hofu kuu ya
kumwona kiumbe Yule juu ya anga la dunia,niliogopa kwani ile ilikua ni mara
yangu ya kwanza kushuhudia kiumbe kile kikiwa juu ya anga la dunia,kwangu mimi
ilikua ni zaidi ya maajabu au miujiza kwani kwa hisia zingine nilihisi labda
kiumbe Yule ni roho mwovu aliye tumwa kuja kunidhuru,haikua hivyo nilikua
katika hali ya kuandikia mate wino ungalipo,kwani nisilolijua litanisumbua na
nisilolifahamu ni kama usiku mnene wa manane.
Nilienderea
kumtizama mwanamke Yule naye alienderea kunitizama,macho yake yenye mboni zenye
ubuluu yalizidi kupendeza usoni mwake,lakini kupendeza huko kwangu mimi
kulinitisha kwani sikuwahi kumwona
mwanadamu mwenye macho ya rangi ile ya kibuluu,nimezoea kuwaona watu
wenye macho yenye mboni nyeusi,nyekundu au ile ya kaki lakini macho haya ya
rangi ya kibuluu yalinitisha sana niliogopa hakika niliogopa na kuhisi kuwa
nipo hatarini.
Sikua na
nguvu tena za kukimbia au kumkwepa mwanamke Yule,kwani miguu yangu haikuweza
kufanya jambo lolote lile sembuse iwe kukimbia,kutoroka au kumkwepa mwanamke
Yule.nilienderea kumchunguza ,kwani umbali aliokuwepo yeye ni umbali ambao
macho yangu yaliweza kumwona,yaani hakua mbali sana na upeo wa macho
yangu,ilikua ni kama mbingu alizokuwepo yeye zilikaribiana na dunia hivyo basi
shida ya kumwona haikuwepo kabisa ,alinitizama na mimi nilimtizama,aliniangalia
na mimi nilimwangalia,tulienderea kutizamana.
Mikononi
mwake alishika kitu kama kitabu chenye rangi ya dhaabu safi kunako jarida
lake,nilikitizama kile ktabu na baada ya kukitizama niligundua kua ni biblia takatifu,ameikamata
mkono wa kulia kwake,mkono wake wa kushoto hakua na kitu chochote mkono huo ulikua mtupu.nikamtizama tena
katika pembe za mabega na mgongo wake
alikua na mabawa makubwa sana ,yalikua ni makubwa kuliko hata ndege wa
angani,yalikua makubwa yenye manyoya
marefu yameambatana pamoja na kushikana na mifupa ya mbawa zake.
Tuliendelea
kutizamana kwa sekunde chache mbeleni.
Kisha
nikamwona anapaa kwa mbawa zake anashuka chini kutoka kwenye lile anga la dunia
hofu na woga vilizidi kunitawala nilijua labda anakuja kunidhuru nafsi
yangu,lakini hapana moyo wangu ulinikataza kuamini hivyo kwani macho yangu
yalipotua kwenye mikono yake na kumwona amekumbatia biblia takatifu nilijua
kiumbe huyu hana madhara yoyote kwangu,amekuja kwa nia njema na pia amekuja
lengo au dhumuni fulani.
Akashuka
taratibu hata akanifikia pale nilipo simama
na baada ya kunifikia yale mabawa yake yakapotea kwa ghafra,lile vazi
lake jeupe likapotea kwa ghafra na ile asili yake ya kizungu ikampotea kwa
ghafra sasa akawa ni mwenye rangi ya mkaa au ile rangi ya chungu kilichopigwa
sana na nguvu za moto wenye kuni nyingi, rangi nyeusi rangi ya kiafrika,mwili
wake ulikua vile vile,labda niseme macho yake yale ya kibuluu nayo yakabadirika
yakawa yana mboni ya rangi nyeusi,urefu wake ulikua vile vile,unene wake nao
pia ulikua vile vile.
Sasa
alionekana amevaa gauni lenye rangi rangi mchanganyiko rangi zilizo kolezwa na
kupambizwa madalizo ya maua maua mazuri ajabu,maua ambayo sijapata kuyaona
duniani hataleo hii sitakuja kupata kuyaon.
Mara baada
yay eye kushuka chini ya aridhi kutoka katika anga la dunia,nguvu za miguu
yangu zilinijia,niliweza kutembea kama nilivyozoea,ile hofu woga na tatiziko la
moyo wangu vikapotea na sasa sikuweza kuogopa au kutatizika tena,hali hii
ilinishangaza mimi binafsi kwani ni kitambo tu niyaone mabadiriko haya
yakinitokea,kwani mwanzo nilikua na tetemeko,hofu na woga,lakini ajabu ni
kwamba sasa nina amani furaha na tumaini.
Nilijiuliza
mara mbili mbili mimi ma moyo wangu,nini ni haswa maana ya kutokewa kwa hali
kama hii,lakini moyo wangu haukuwza kunijibu kinagaubaga zaidi ya kuwa na
subira kwa kadri ya nuckta,dakika na masaa yatakavyo kwenda mbele.
Tulitizamana
tukiwa wote tumesimama sentimita chache mbele yetu,tabasamu lake pana
halikumtoka mdomoni kwani meno yake meupe yaso na mfano yalimpendezesha zaidi
na kumfanya awe mzuri zaidi,mara baada yayeye kutabasamu name pia
nilitabasamu,tukatizamana,akatembea kunijia mahari nilipokua nimesimama pale
pale kwenye jiwe kubwa la chuma,pale nilipoweka gitaa langu nilililotumia
kuitumbuizia nafsi yangu dakika chache zilizo pitaa.akatembea mwanamke
Yule,akatembea mpaka nilipokua nimesimama,nikamwona anaunyosha ule mkono wake
wa kulia mkono alioikamata biblia
takatifu akaielekeza kwenye mkono wangu wa kulia,kama ishara ya kunipa ile
biblia takatifu.
Name
sikusita,nikainyosha mikono yangu yote miwili ili kuipokea ile biblia
takatifu,sijui niliupata wapi ule ujasiri wa kupokea ile biblia,na baada ya
kupokea ile biblia akanitizama kwa macho yake yote mawili kisha
akatabasamu,tabasamu lile lile zuri lenye utajiri wa hekima,busara,wema pamoja
na mambo mema yenye neema na yenye rehema.na baada ya
kuipokea ile biblia taktifu mwanamke
yule akanipita pembeni yangu nikamwona anaelekea eneo ambalo
kijito kile kilikua kinayapeleka maji kwenye mkondo wake.
Nilienderea
kumsindikiza kwa macho yangu yote mawili ili nione ni wapi anaelekea nan i wapi
mwisho wa safari yake,hatua kwa hatua nilimsindikiza kwa macho yangu yote mawili
hata alipofika kwenye ule mto nilimwona akiinama chini kwa mtindo wa
kuchuchumaa,na baada yay eye kuchuchumaa nilimwona akiokota kopo kubwa la
platik kisha akautwaa na mtungi ambao mpaka leo hii najiuliza maswali ni wapi
aliupata ule mtungi na lile kopo kubwa
la plastick kwa sababu mtoni pale hapakuwa na kitu chochote cha kutekea maji
zaidi ya maji yenyewe yalivyo kua yakisafiri kwa mwendo wa kujisukuma chini
chini pamoja na mchanga mwingi ulio kuwepo pale mtoni kama vile mchanga wa
baharini.
Na
alipokwisha kutwaa lile kopo la kutekea maji pamoja na ule mtungi,mwanamke Yule
akaanza kuyachota yale maji safi ya mtoni na kuyaweka kwenye ule
mtungi,alifanya hivyo kwa kurudia rudia
mpaka pale aliporidhika yeye mwenyewe kwamba ametosheka na kiasi cha
maji ambayo alikua anayateka.
Nilimtizama
tena nikamwona anafungasha ngata kwa kutumia kitenge chake kizuri alichojivika
kiunoni,na bada ya kufungasha ngata
malaika Yule akauinua mtungi wake wenye maji yaliyo pwaa hadi juu ya
mdomo wa ule mtungi kisha akajitwika kichwani
pake.tendo lote lile alilokua akilitenda mwanzo mpaka hatua ya mwisho ya
utekaji way ale maji mimi nilisimama
mahari pale pale aliponipita nikimtizama
kwa kila tendo alilokua akilitenda.
Alipojitwika
ule mtungi wa maji mwanamke Yule akakanyaga hatua moja kutoka kwenye pembe ya kile kijito cha maji nikamwona
anainua mguu wake ili aondoke mahari pale lakini ghafra ule udongo ulioshikilia
kile kijito cha maji ukamengenyuka
mengenyuka na baada ya kumengenyuka udongo ule ulididimia chini na
kuingia kwenye mto ule yaani kwa kifupi
ilikua ni kama mmongonyoko mdogo wa udongo .mmongonyoko ule ulitokea kwa ghafra
sana hali ambayo hakuna aliye itarajia si mimi wala si
mwanamke Yule.
Kitendo cha
kumongonyoka kwa ule udongo kuliperekea mwanamke Yule ambaye muda mfupi tu
alipotua chini kutoka juu ya anga la dunia nilipoteza kumbukumbu za kumtambua
yeye kama malaika name nikamwona kama binadamu
wa kawaida kama binadamu wengine walivyo, ujio wa mwanamke huyu lilika ni kama tukio la ajabu
sana katika maisha yangu binafsi kwani mbali nay eye kuja kama malaika
alijibadirisha ule mwili wa kiroho na kuwa binadamu wa kawaida akaichukua nafsi yangu ya kumbukumbu na kuipoteza kimiujiza hata sikuweza
kukumbuka wala kutambua kuwa nipo na roho wa kimungu ambaye amejibadiri na kuwa
roho wa kibinadamu.
Nilishuhudia
mmongonyoko ule wa udongo ukimwangusha chini ya aridhi na kumsukumia mwanamke Yule,akaanguka na kudondokea kwenye mto kitendo cha yeye kuanguka na kudondokea
ndani ya maji ya ule mto kilimfaanya apige ukulele wa kuomba msaada,akitapatapa
na kuvutwa na maji mengi ya ule mto,akitapatapa na kusukumizwa mbali sana na
ule mto.niliogopa nilipo ona tukio kama lile likitendeka tena mbele ya
macho yangu,niliogopa na niliingiwa na hofu kuu kumwona mwanamke Yule
akigugumia vikombe vya maji yale ya
mtoni.
Maji ya ule mto yalienderea kumvuta na
kumsukumizia mbele ambako mto ulikua unayapeleka maji yake,yalikua yakimvuta
kwa mwendo wa kasi sana,yalikua yakimvuta kama vile mafuriko ya mvua yanavyo
vuta takataka au kitu chochote kile kinachoweza kubebwa na maji nilishuhudia
namna anavyo zama na kuibuka akipiga kelele za kuomba msahada .
Haraka sana
kengere ya hatari ikaria ndani ya ubongo wangu,ikaniambia nifanye jambo la
ziada ili kuyaokoa maisha ya mwanamke
Yule,nikazipiga mbio mpaka usawa wa ule mto na kisha nikajitoma mpaka
ndani ya maji ya ule mto nikazama na kuibuka ……nikazama na kuibuka….nikazama na
kuibuka nikimtafuta mwanamke Yule ambaye
baadaye sana niligundua jina lake anaitwa magdallena,nikazama tena sikumwona
nikaibuka tena sikumwona nikajua sasa hapa kuna hatari kubwa ndani yam to ule, kwa vile nilikua na ujuzi
wa kucheza na maji sikupata shida sana kuzama na kuibuka kwani staili hizi
mbili ni staili nilizozizoea sana mara ninapokuja kuogerea katika mto huu.
No comments:
Post a Comment