Thursday, November 26, 2015

.PENZI LANGU KWA LOWASSA,NI SAWA NA MAGUFULI.
Peni nina shikiria,maneno ninayatoa,
Lowasa namtambua,magufuri anafaa,
Nani nitamchagua,ili kura kumpigia,
Penzi langu kwa Lowasa,ni sawa na Magufuli.
 
Nimchague Magufuli,au jamani Lowasa,
Awe kiongozi nguli,sio mfanya siasa,
Awe Raisi mahili,asiwe anapapasa,
Penzi langu kwa Lowasa,ni sawa na Magufuli.
 
Mimi nasema Lowasa,Magufuli anapeta,
Nani Raisi wasasa?,kura yangu atapata,
Yani UKAWA kwa sasa,na CCM inafata.
Penzi langu kwa Lowasa,ni sawa na Magufuli.
 
Magufuli nampenda,Lowasa sitamtenga,
Kazi zote ametenda,lowasa atatujenga,
Magufuli kumtenda,madawa nitajidunga,
Penzi langu kwa Lowasa,ni sawa na Magufuli.
 
Lowasa tunamjua,waziri alishakua,
Nchi alishikiria,maendereo katoa,
Mamia twafurahia,uraisi kugombea,
Penzi langu kwa Lowasa,ni sawa na Magufuli.
 
Tamati nimeshafika,sasa ninaitimisha,
Magufuli namtaka,Lowasa ananikosha,
Hao wote nawataka,Ikulu kuwakilisha,
penzi langu kwa Lowasa, ni sawa na Magufuli.

No comments:

Post a Comment