Saturday, November 28, 2015

SHOGA ACHA KUJIPWETEKA.

Shoga acha kujipweta, mume wangu sio wako,

Kutwa kucha kwa mwenzio, kwako wewe kunanini?,

Hujasikia kilio, wakuja kama utani,

Jioni na pulizio, tushakuchoka jamani,

Wewe si mke wa mtu?!,bado una wako ndani,

Shoga acha kujipweteka, mume wangu sio wako.

Shoga acha kujipweteka,mume wangu sio wako,

Vijana wanakujua, wamama pia wadada,

Jioni wawachukua, waenda kupaka poda,

Wasema umetulia, kijiko chako gireda,

Wewe si mke wa mtu?!, bado una wako ndani,

Shoga acha kujipweteka ,mume wangu sio wako,

Shoga acha kujipweteka,mume wangu sio wako,

Nadhani hujaelewa, Somo ninakupatia,

Usiku pombe kulewa, vijana wakupitia,

Nani asiyekujuwa, jilani na bi maria,

Wewe si mke wa mtu?!, bado una wako ndani,

Shoga acha kujipweteka, mume wangu sio wako.

Shoga acha kujipweteka, mume wangu sio wako,

Wataka mume wa mtu, magonjwa huya ogopi,

Wenzako vidudu mtu, wadanganywa nazo pipi,

Wewe si mke wa mtu, bado una wako ndani?!!,

Shoga acha kujipweteka, mume wangu sio wako.

Shoga acha kujipweteka, mume wangu  sio wako,

Vijana kuwachanganya, kesho huyu jana Yule,

Unakua kama panya, kulaga sana mchele,

Wazazi walikuonya, yataja  kukuta mbele,

Wewe si mke wa mtu, bado una wako ndani,

Shoga acha kujipeteka, mume wangu sio wako.

Shog acha kujipweteka, mume wangu sio wako,

Wenzako tuliwafunda, na sasa wametulia,

Majola na mama sonda, leo unawasikia,

Mume ni kama kidonda, siku utaja umia,

Wewe si mke wa mtu, bado una wako ndani,

Shoga acha kujipweteka, mume wangu sio wako.

Shoga acha kujipweteka,mume wangu siowako,

Ni kweli umetukela, waume kuwachukua,

Mimi na mama laila, wote twalalamikia,

Huu ni wako msala, lazima kuwachia,

Wewe si mke wa mtu, bado una wako ndani,

Shoga acha kujipweteka,mume wangu sio wako

 SHOGA ACHA UMBEA

Shoga acha ushangingi, shoga acha umbea,

Tadhani kunywa mitungi, na pia umeshalewa,

Au tafuna mirungi, domoni meelemewa,

Maneno yaso msingi, domoni umepaliwa,

Shoga acha ushangingi, shoga acha ushambenga,

Shoga acha umbea.

Shoga  acha umbea,shoga acha ushangingi,

Kutwa kucha watembea, machoni mepaka rangi,

Kuchonga na kuchongea, hata visivyo msingi,

Domo lako melegea, guu limeota gigi,

Shoga acha ushangingi, shoga acha ushambenga,

Shoga acha umbea.

Kwani watulisha sie, au  watuvisha shoga,

Tuache tujikaangie, miogo hata maboga,

Mavazi tujivalie, tupendeze kwa kukoga,

Ewe mbea ulie, tafurahi kijinyonga,

Shoga acha ushangingi, shoga acha ushambenga,

Shoga acha umbea.

Kutwa kucha kuchunguza, kutwa kucha kupeleleza,

Vijana wabembeleza, wataka kuwapoteza,

Jahanamu kwenye kiza, nenda mwenyewe kuoza,

Shoga acha ushangingi,shoga acha ushambenga,

Shoga acha umbea.

Bwana asie wa kwako, wamtakia kinini?,

Walegeza jicho lako, wamvalia kimini,

Watingisha lako tako, lainika kiunoni,

Na vingi vingi vituko, umtupe kitanzini,

Shoga acha ushangingi, shoga acha ushambenga,

Shoga acha umbea.

Tuliza wako mtima, katulie sebuleni,

Uache kutuchochoma, kama nyama ya jikoni,

Kwani unavyo loloma, faidaze huzioni,

Jitafutie heshima, utapendwa abadani,

Shoga acha ushangingi, shoga acha ushambenga,

Shoga acha umbea.

Nenda shamba ukalime, matunda utayapata,

Wanini hao waume?, ambao unawafata,

-hghWengine mapaka shume, utapigwa utajuta,

Mara ukishikwa shime, ngumi zitakukumbata,

Shoga acha ushangingi, shoga acha ushambenga,
Shoga acha umbea.

No comments:

Post a Comment