“NILIOLEWA NA MALAIKA……..NIKAMUUA MALAIKA”
SURA YA KWANZA
GO MALAIKA JAMES …GO
“Go malaika
james..go…go please”
Ilikua ni
sauti yamwenyezi mungu,muumba nchi na
aridhi baba asiye na mwanzo wala asiye julikana mwisho wake ni upi.
“No my lord
god..I will not go”
James
alimwambia mungu,huku akionesha maringo,majivuno na kiburi ndani ya moyo
wake.jambo ambalo lilimchukiza sana mwenyezi mungu,lakini kwa vile mungu ni
mwenye nyingi rehema ,upole busara ,amani na utulivu alihamua kuenderea
kumbembeleza malaika james,aende duniani
Wengi
wanasema uzee ni dawa ndivyo ilivyo kua kwa mwenyezi mungu,yeye umbembereza mtu
yeyote Yule amtakaye,yeye umsonga mtu yeyote Yule ampendaye,kwa vile yeye si
athumani basi upendo wake upon kwa kila kiumbe kionekanacho na kile kisicho
onekana.
Kwanini
utaki kwenda duniani malaika jamesi?”
Mwenye
heri,rehema na neema alimuuliza malaika james,huku umati wa wazee wenye hekima
busara na elimu ya mambo ya dunia na mbingu,bahari na aridhi ukimzunguka
miguuni pake nao wakimwangukia kifundi fundi,wakimwabudu na kumyenyekea,wakimlilia
na kumwimbia,huo ulikua ni upande wa mashariki kwake na upande wa magharibi
kwake walikuwepo malaika wengi sana
idadi yao haipo duniani wala juhanamu,idadi yao ni kama wingi wa nyota zingarazo juu mbinguni kwnye giza jeusi tii.
Na malaika
hao walikua na kazi moja kuu kumwimbia mwenyezi mungu nyimbo tamu za
kusisimua,kumwimbia mwenyezi mungu mashairi,tenzi,ngonjera,tenzi za rohoni
pamoja na zaburi,malaika hao ndio malaika wa nyimbo malaika wakuu wenye vipawa
na vipaji vya kuimba kwa sauti ambazo kamwe hazipo duniani au jehanamu.na kati kati ya eneo ambalo
mwenyezi mungu mjaa neema na mjaa nguvu na haki aliketi hapo ndipo malaika jamesi alipopiga goti lake ameinama
kichwa chini,anaogopa kumtiza Yule mwenye heri Baraka na neema,anaogopa
kumtizama macho yake,anaogopa kumtizama mdomo wake,anaogopa kuisikiliza sauti yake,anaogopa ndio
anamwogopa mtu huyu aliye keti kwenye kiti cha ufahari,kiti kilicho pambwa kwa
wingi wa vito vya thamani,zahabu,lulu,almasi na madini mengineyo mengi
yasiyopatikana duniani wala jehanamu.
Baba ni heri
umtume malaika mwingine lakini sio mimi baba, nasema kweli baba siwezi na tena
sina uwezo wa kwenda duniani.
Malaika
jamesi alimjibu mwenye heri na Baraka na
upendo na huruma naupole.
\Mwenye heri
akamtizama malaika james
sio kwamba
mwenye heri asingeweza kumwadhibu malaika james kwa kiburi alicho kua
akikionesha mahari pakle patakatifu,lakini ikumbukwe kwamba mwenye heri ni
mpore nan i mwenye huruma sana,kwanza
anajari na anathamini,mawazo na chaguo la kiumbe kilicho
Hai ndio
maana mwenye heri akuchukua maamuzi ya haraka au maamuzi ya ghadhabu,zaidi ya
kumtizama malaika james akisubiria jibu kutoka kwenye kinywa chake kinywa cha
malaika james,kudhihirisha namna gani amekubari au namna gani analikataa ombi
la mwenye heri.
Mwenyezi mungu mgawaji wa neema akamtizama
malaika james,akamtizama kwa macho ya
upole huruma na wema kisha akamwita kwa sauti iliyo jaa upole malaika james
akaitika na kumtizama mwenye heri macho
yao yakagongana,wakatizamana
Nninakutuma
wewe kwa sabau nitakusaidia,nenda,nenda usiogope nenda duniani,nenda
kaitangazie dunia kua siku za mwisho zimefika,neenda kaiambie dunia kua zambi
zao zinahesabia,nenda kawaambie walimwengu kua
kila tendo,kila neno,kila fikra,kila wazo la mwanadamu,liwe jema au liwe
baya mwenyezi mungu ameliona na mwenyezi mungu
atashusha makari yake kwa wale wote walio jaa kufuru,kwa wale wote
watendao yaliyo machukizo na machafu
yasiyo pendeza katika macho yangu.”
Nenda
tafadhari,nenda james nenda kawaokoe wote walio wangu duniani,neda kawatafute
wote waliopotea duniani nawe uwarudishe katika nyumba yangu wawe ni kindoo
wenye furaha, kondoo wenye mchungaji,kondoo
na mchungaji awapaye hitaji lao lote la kibinadamu,uwalishe,uwanyweshe,uwalaze,uwavike
na zaidi ya yote uwafundishe kuwa mimi ni mungu,mimi ni mmoja nan i mim tu
ndiye ninaye paswa kuabudiwa,hakuna mungu mwingine zaidi ya mimi……
Go malaika
james go….
Mwenyezi
mungu alihitimisha kwa kumwambia kwa upole malaika james
James bado tu alionesha hali ya kusita sita,hali ya
kuogopa,hali ya kutia hofu na hali ya kujaa mashaka na woga ulio mtawala,
Hakutaka
kuja duniani hakutaka na tena hakutaka,sijui ni kwa nini hakutaka hata mimi
sijui kwanini james hakutaka kuja duniani kuuleta ujumbe mtakatifu wa mwenyezi
mungu mwenye heri mwenye Baraka mwenye nyingi huruma na rehema.
Kwa ghafra
mbingu zikaanza kufunguka,sauti za wale malaika walio kua wakimwimbia mungu nazo
zilienderea kuvuka kila pande ya
ulimwengu ule,na wale wazee walio
kua wakimwangukia na kumwabudu Yule mzee mwenye heri bado tu walienderea
kufanya hivyo hivyo wakimwangukia kifundi fundi,pasipo kuchoka.
Sauti
za mabaragumu,mataumbeta,vinanda ngoma na vifaa vinginevyo vingi vinavyo
zalisha muziki zilisikika kila pande ya ulimwengu ule,malaika walienderea
kuimba na kusifu malaika walienderea kucheza na kuzunguka pande za ule
ulimwengu,ulimwengu ambao hakuna mwanadamu aliye hai ameweza kufika,ni
ulimwengu wa kipekee sana ni ulimwengu war oho,ni ulimwengu wa wale ambao
hawaonekaniki kamwe si kwa macho si kwa darubini na wala si kwa uchawi wala kwa matun guri,ni ulimwengu wa
kipekee sana kuwepo ulimwenguni.
Sauti za wale malaika zilienderea kusikiaka
zikapanda na kushuka,zikivuma na kuvumuka,zikipaa na kupaika
“Mwibieni
nyimbo enyi mbinguni
Mwimbieni
nyimbo za kumsifu,
yeye ndiye
mkuu,yeye ndiye mkuu
yeye ndiye
mkuu,yeye ndiye bwana wetu
anayepaswa
kuabudiwa,halleluya jehhova
haleluya jehhova,halleluya
jehhova halleluya”.
Malaika wale
walienderea kuimba kwa furaha.na kadri walivyozidi kuimba ndivyo malaika james
alivyo zidi kupotea kutoka katika ulimwengu wake na kueleka ulimwengu
mwingine,ulimwengu ulimwengu aliotumwa
kupeleka ujumbe,ujumbe mtakatifu ujumbe wa mwenyezi mungu,ndio ujumbe na ujumbe
huo james alipaswa kuupereka mara moja na
na baada ya kupereka jumbe hizo
alipaswa kurejea tena katika dunia ya
kwao dunia ambayo hakun mateso,hakuna shida,hakutana taabu,maangaiko,maumivu,
ni dunia yenye raha na starehe ni dunia yenye wingi wa huba,mahaba na
mapenzi,dunia ya watakatifu,dunia ya wavaao mavazi meupe yangaayo kupita kiasi
yaani mavazi hayo hayapo na
haytakuja kuwepo duniani.
James sasa
alishaa aga kwao na sasa anaingia katika dunia mpya na dunia,dunia ambayo
hakuitaka,alikubari tu kuja kwa shingo upande,alikubari tu kwa sababu mwenye
heri na mwenye huruma alimwomba
akubari,atii na afanye kama vile
aLivyotakiwa kufanya,japokua roho yake iligoma,lakini ili kuonesha utiifu kwa
babaye james alikubari,alikubari kwa sababu ya tama zake tu,tama za kuvikwa
taji na cheo kikuu ajapo rejea tena katika dunia yake,ajapomaliza kazi ambayo
ameagizwa kuifanya ndi ni tama tu ndizo zilizo mvuta james hadi akachukua
uamuzi wa kwenda ulimwengu ambao sio wake.
*****************************
“Mmhhh!!!”
Nilibaki nashangaa na kupigwa na butwaa yaani
kusikia yale yote ambayo mume wangu
james alikua akiniadithia,kisu kikienderea kuninginia kwenye tumbo lake, damu
nayo ilienderea kumchuruzika ikalowanisha nguo zake zote nyeupe nazo zikawa
nyekundu zinatisha kwa wingi wa damu ambazo zilimtoka mume wangu pasipo kikomo,
Nilishangaa
sana kwa jinsi mume wangu james alivyo kua akieleza,nilishangaa na nikabaki
kumshangaa zaidi,kwani sikutarajia katika maisha yangu kusikia maneno yale,siku
zote nilizoishi naye alikua na alionekana ni binadamu wa kawaida lakini iweje leo
aniambie yeye ni malaika na malaika ambaye
alitumwa kuleta ujumbe duniani.
“Niletee
maji ya kunywa Sophia,”
James
aliniomba nimletee maji
Huku bado
anatetemeka,mwili wake amekishikiria kisu nilichomchoma,anatamani kukiondoa
klakini nguvu hana na nguvu zimemwishia,anapumua kwa taabu,anapepesa pepesa
macho yake huku na huko hajiwezi yu mahuuti masikini james nilianza kumwonea
huruma nilianza kujutia kitendo nilicho kifanya lakini nifanyeje ndugu zangu
tendo nimeshaalifanya na pamoja na
majuto yanaenderea kuutesa mtima wangu.
Niliamka
mahari pale haraka nikajifunga kanga yangu,mikononi nimejaa damu nyingi zilizo
gandiana,nikayatwa maji ya kunywa kwenye
glass na baada ya kuyatatwaa nikampa mume wangu james ayanywe.
Sijui
kwanini niliingiwa naroho ya kinyama namna ile,sijui ni kinini kilicho nifanya nighadhibike na kutenda tendo
hovu kama lile,japo kua inauma na inasikitisha wacha nienderee kusimulia.
No comments:
Post a Comment