KISWAHILI YETU MALI.
1. Asante sana Kaimu, kwa wingi wa ukarimu,
Nimesimama Sekomu, Na kuandika kalamu,
Maneno yangu matamu, kuyasikia wazimu
Nimekuja, na ujumbe Kiswahili yetu mali.
2. Kiswahili ni Asali, kukitamka fahari,
Kiswahili kwangu mali, faida yenye johari,
Mimi mwenyewe nakiri, utamu wake sukari,
Na tafakari fikiri, hakina mwisho bahari.
3. Katika dunia leo, twalia maendeleo,
Twatamani vingi vyeo, vilojaa upendeleo,
Vitamu tamu vyeo, twataka mafanikio,
Lakini na ipo siri, tutumie Kiswahili.
4. Ukitaka pata elimu, ukitaka pata ajira,
Jambo moja la muhimu, na ndio ngao na dira,
Nimuhimu kufahamu, kwa hekima na busara
Kiswahili ni kitamu, utamu wake sukari.
5. Kiswahili kwetu mali, utajiri wa dunia,
Utamaduni asili, lulu yetu watanzania,
Baraka za kila heri, mataifa yalilia,
Kiswahilli lulu yetu, Ni mama waki Afrika.
6. Tupo juu Tanzania, sababu ya Kiswahili,
Sisi tunajivunia, umoja wetu wa kweli,
Amani yetu dunia, sababu ya Kiswahili,
Tukilinde Kiswahili, tukitunze Kiswahili.
7. Tusijeona aibu, kukisifu Kiswahili,
Huo Ndio wetu wajibu,ngao tunaikubali
Yenye faida zahabu, lugha yetu Kiswahili,
Mwende kwao si mtoro, cheza kwenu utatunzwa.
8. Tuoneshe uzalendo, kutetea Kiswahili,
Na tufanye kwa vitendo, kutangaza Kiswahili,
Pasiwepo hata nyondo, kukipelekea mbali,
Huo Ndio ujasiri, kujaipenda asili.
9. Mungu asiye achuki, karama zake kufanya,
Africa ya mashariki, lugha bora imepenya,
Mazuri mengi lukuki, keswahili kimeshafanya,
Tuna haja kukienzi, na tunzo kukipatia.
10. Tukitangaze Arabu, kemejaa maajabu,
Na wasione aibu, lugha hiyo mahababu,
Watamke bila tabu, lugha hiyo ya mababu,
Hakika wanatamani, mali yetu ya thamani.
11. Tusiweze kukitupa, maana kinatulipa,
Furaha na kunenepa, tukipita twajitapa,
Kwa wingi kimetulipa, wingi wake wa nafaka,
Nehema nayo rehema, fadhili nazo heshima.
12. Tunahaja kukienzi, na tuzo kukipatia,
Kimekwisha jaa mapenzi, na dua ku kiombea,
Kwa mashairi na tenzi, nyimbo bora kusifia,
Kiswahili barikiwa, malaika wakwambia.
13. Kiswahili barikiwa, malaika wakwambia,
Marefu maisha jawa, dua njema twakuombea,
Kiswahili barikiwa, malaika wakwambia,
Marefu maishajiwa, malaika wakwambia,
14. Ewe Mama nenepa, wajibu ni kukutunza,
Afya ni supa supa, kula mama unaweza,
Mimi mwenyewe naapa,mama yangu kukutunza
Mbele sana utafika usiwe nayo mashaka.
15. Wengine ni mabatili, ni bora wakajinyonga,
Hawasomeki fasili, wahangaika kulinga,
Waondoke majangili, mwendo wao wa vinyonga,
Wakupishe mwana mwali, uitawale dunia.
16. Yamewafika shingoni, wamebaki tapatapa,
Nyota zao zi gizani, hata mwanga watopata,
Ewe jua dunia, uwachome fasta fasta,
Wafuta kwenye ramani, wasahaulike dunia.
17. Kipichakung’ang’ania, hatuwataki timua,
Kwanza wamesha chelewa, wataishia kunawa,
Muda watupotezea, waende wakanye jera,
Hiyo mali mkoloni, haina thaamni mama.
18. Wanaitwa kingereza, wengine ni kifaransa,
Mama hao wameoza, yatupasa kuwasusa,
Wananuka mafunza, ni bora kuwanyanyasa,
Waarudi ughaibuni, hatuwataki hasirani.
19. Hao ndio mashangingi, tena wanavuta bangi,
Wapepesuka mitungi, za fifia zao rangi,
Ndio waeneza gonjwa, tumewapima angaza,
Wamelazwa kwa vitanda, wayaona majeneza
20. Niseme kwa kinyakyusa, kibantu nakitukuza,
Kuliko sema faransa, lugha nisiyoiweza,
Napata faida gani, kutukuza kingereza,
Napata faida gani kutukuza kingereza
21. Moyoni ninawacheka, watumwa maghaaribi,
Wamemezwa wametekwa, mawazo ya kumbikumbi,
Hakikia wanateseka, jamani uongo zambi,
Kiwahili wakomboe, kiswahili waokoe.
22. Nipo hapa kuwachamba,waache jigagamba,
Kwanza hao ni washamba,shuleni hawajatimba,
Hapa mama watalemba, na kuimba wataimba,
Kiswahili wetu simba,uitawale dunia.
23. Wazee walao chumvi, vijana wapeni hekima
Siyakimbie majamvi, yasofaidisha vema,
Yamejaa maugomvi, malipo yake vilema,
Kama kawa kama dawa, kitukuzwe Kiswahili.
24. Siku njema asubuhi, dua kuku mpate mwewe,
Pole pole tutawahi,Tusikipate kiwewe,
Mwenyezi si athumani, alo juu mngoje chini
Mpanda ngazi tashuka, Kiswahili tatawala
25. Tujipe matumaini, na pia tujiamini,
Mioyo yenye amani, tufe nayo kikondoo,
Beti ishirini na sita, mkono nimeimba fasta,
Masikini mi jamni, natamani kwendelea.
26. Tamati nimefikia, natamani kwendelea,
Giza limesha ingia, kalamu yanigomea,
Mimi naitwa Elia, Mwalukali wa kumbeya,
Mwenyezi mungu jalia, kesho tuonane pia.
No comments:
Post a Comment