Sunday, November 29, 2015

ACHA DADA AOLEWE

Mawazo yake  dada ngu,anawaza kuolewa,
Ajikalie kwa chungu,moto wake kuchochewa,
Aoshe viombo  chungu,na sabuni atapewa,
Anawaza kuolewa,Anawaza dada yangu.
 
Atamania kuzaa,ajivunie  watoto,
Kamwe hawezi kata,autunze ujauzito,
Na dunia yashangaa,kulea kutunza wito,
Aolewe dada yangu,anawaza dada yangu.
 
Anatamani mapenzi,kitu hicho matatuzi,
Kinompa gugumizi,yu mpweke hana buzi,
Aibu kitu kishenzi,kiletacho uchokozi,
Chamnyima mume dada,anawaza dada yangu
 
Enyi vijana tulivu,namleta kwenu dada,
Wa mwenendo mkamavu,sanda kalawe kushinda,
Onesheni uangavu,kimpata tampenda
Ofa malumu naleta,anapenda kuolewa
 
Mwanaume na mwanamke,ndio nguzo ya umoja,
Wito mikono  tushike,tushikamane pamoja,
Ujasiri tujivike,familia kujengia,
Majukumu tujitwike,anapenda kuolewa
 
Ofa malumu naleta,wajunzi twanga pepeta,
Chelewaye sijejuta,sinambie sikupata,
Naogopa mi kusutwa,habari hiyo ni nyota,
Atakaye ameshinda,anawaza dada yangu.
 
Dada mwenyewe kigori,bikira ni mwanamwari,
Mrembo huyo mdori,mchapa kazi kijori,
Sura na rangi mzuri,msomi wa seKondari,
Elimu yake nasema,anawaza kuolewa.
 
Mwenyezi mungu kaumba,urembo nao kapamba,
Pendo jema si kasumba,namtangaza mchumba,
Tabia meitambua,mchapa kazi najua,
Sababu ni dada yangu,anawaza kuolewa.
 
Mfupi si mbilikimo,rangi yake kahawia,
Mashavuni na vishimo,nyuma tako katupia,
Hapaki tope domoni,nywereze ujisukia
Ni mrembo wa asilia,anapenda kuolewa
 
Hapatikani Asia,Hapatikani Ameika,
Zunguka zungu dunia,pande zote Afirika,
Watu wa kitanzania,binti huyo kaumbika,
kimpata taniambia,anapenda kuolewa
 
Hataki kuja chezewa,anataka kupepewa,
Ndoa ikishafungiwa,baraka mkigawiwa,
Muishi kivumiliwa,penye shida kutatuwa,
Mume na mke pamoja,mujeishi kwa umoja.

No comments:

Post a Comment