Thursday, November 26, 2015

nyimboooo


PENDO LETU

Pendo letu ni kama,  jua ambalo halizami

Pendo letu ni kama mwezi ,ambao  unawaka

Pendo letu ni kama nyota,nyota nyota zinangara

          Pendo hilo,pendo hilo,pendo hilo, pendo,

          Pendo hilo…(pendo hilo)Pendo hilo …(pendo hilo),

          Pendo hilo…(pendo hilo pendo hilo….pendo)

 

 

2

Pendo letu ni la thamani,pendo latoka moyoni,

Pendo letu  limejaa amani,pendo tunali amini,

Pendo letu ni la milele,pendo wawili wawili.

    Pendo hilo,pendo hilo,pendo hilo, pendo,

          Pendo hilo…(pendo hilo)Pendo hilo …(pendo hilo),

          Pendo hilo…(pendo hilo pendo hilo….pendo)

kibwagizo

Nyota,nyota zinazongara,jua nalo linapo chomoza,

Mwezi nao unavyo waka,mapenzi yetu mapendo,mapendo.

 

 

 

2WEWE

Ndiwe  wewe wa moyo wangu.

Nimekupenda sana wewe,

Ndiwe wewe wa nafsi yangu,

Nimekuchangua wewe……..

 

Kibwagizo.

Sina mwingine kama wewe,

Nimeridhika kuwa nawee

Imekupenda nafsi yangu,

Imeridhika kuwa nawe.

 

Naacha yote haya  mapinduzi,

Nageuza moyo wenye    mageuzi,

Nivute mkono nije kwako

 


 

 (Najisikia kuweweseka.)

 

 Kibwagizo

 

Najisikia kuweweseka x3]

Natamania uwepo karibu

Uwe karibu ,karibu na mimi,x3

Uwe karibu usiku huu.

 

Nalipapasa godoro la kitanda,

Nahisi kama nina kupapasa

Nahisi pia unananipapasa

(Najisikia kuweweseka)

Nimekumbata mto kulalia,

Nahisi kama nimekukumbata.

Nahisi pia umenikumbata

(Najisikia kuweweseka)

 

      4. ELIA NJOOO

Sauti yako ina niita,

Mwendo wako unaniita,

Sura yako inaniita,

Na macho yako yananiita.

                     Ninaitwa ( Elia njoo)X4

                     Ninaitwa …elaija aaah.

 

Sauti yako ina mapenzi

Sura yako ina mapenzi,

Mwendo wako una mapenzi,

Na macho yako yana mapenzi,

                     Yananiita(elia njoooo) x4

                     Yananiita Elaija aaaah

Chorus

Elia njoo(elaija aaaahh)x4

Mupenzi njoo(mapenzi njoo)x4

Elia njooo(elaija aaah)x4.

 

2

Ninayataka hayo mapenzi,

Unipatie hayo mapenzi,

Nayalilia hayo mapenzi,                            

Nayatamani hayo mapenzi,

         Nigee mie (hayo mapenzi) x4

         Nigee mie  (elaija  aahh).

 

 

Ninayataka hayo mapenzi,

Unipatie hayo mapenzi,

Nayalilia hayo mapenzi,                            

Nayatamani hayo mapenzi,

         Nigee mie (hayo mapenzi) x4

         Nigee mie  (elaija  aahh).

 

 

 

 

 

 

NI MAZITO YA DUNIA

 

                Hodi hodi naingia, ulingo upanueni,

                Nami niweze tulia, niliyonayo wambieni,

                Leo siku mefikia, ya moyoni watoleni,

                Ni mazito ya dunia, jamani yasikieni.

 

                Huku siku Elimisha, bali ni kuiharibu,

                Walianza kwa bashasha, hata pia na tarabu,

                Waliimba shirikisha, wala hawakuwa bubu,

                Ni mazito ya dunia, jamani yasikieni.

 

                Redioni siku hizi, ni mahala pa ushenzi,

                Vizazi vya siku hizi, kuendeleza uzinzi,

                Hawafanyi mazoezi, nyimbo zao kwa utunzi,

                Ni mazito ya dunia, jamani yasikieni.

 

                Mapenzi mapenzi nini?, hata wazee kwa vijana,

                Vijana tu hatarini,eti wakula ujana,

                Kuingia mapenzini,maisha kuhatarisha,

                Ni mazito ya dunia,jamani yasikieni.

 

                Muziki si ule tena, kuimba eimishana,

                Huu ni kuibiana,tena kukarahishana,

                Wazee kwa vijana,viduku kuchezeana,

                Ni mazito ya dunia,jamani yasikieni,

 

 

 

5.Nilishindwa kukulinda

Nilishindwa kukulinda,wakaja walokupenda,

Tena wakakutaka,na kukupakata,

Uliposinzia ,wakakutania

Sasa unalia,wamekuachia.                           

 

Kibwagizo

Nilishindwa kukulinda,makosa yapo kwangu,

Wakaja walokupenda,tena wakakutenda,

Makosa yapo kwangu,nilishindwa kukulinda,

Nilishindwa kukulinda,nilishindwa kukulinda.

 

Nilikuacha huru,popote unazuru,

Kumbe nafanya kosa ,hivyo ukanisusa,

Sasa umeachwa na tena umetupwa,

Rudi nimekusamehe na tena usirudie

Bridge

Nilishindwa  kukulinda(kukulinda)x5

 

 

 

6.Turudiane,tusamehane

Tumetengana,Tumeachana,

Ni mambo ya wivu,Yametutetangana,

Ninatamania,Nikukuambia,

 turudiane, tusamehane,

 wacha niseme, turudiane

 tusamehane,Ua langu moyoni.

 

Chorus

Ua langu moyoni,

mpenzi wangu zamani,

Bado mimi nakupenda ,

naomba  turudiane,

Bado  mimi nakupenda,

naomba  tusamehane

bado mimi nakupenda,

naombaturudiane

bado mimimi nakupenda,

naomba tusamehane

 

                                                                                                                 

Ninakumbuka,Sana siku zile,

Raha ulinipatia,Mahari tulipitia,

nyimbo tuliimbia,mambo yetu yalipoa,

wanifanya niteseke,

 ninapokua ni mpweke.

 

 

Verse 3

Nipo moyo mpweke,Wanaojidunda dunda,

Sioni zaidi yako,Moyoni ninakonda

,sasa masiku haya,raha sizipati,

kuimba naona haya,mahari sipiti ,

mambo yangu sio poa,

wanifanya niteseke

ninapokua ni mpweke

No comments:

Post a Comment