Monday, December 24, 2012

shairi

 FREE MASON

1.Imezuka hiyo din,hiyo dini ya shetani,
   watuwangu sikieni,msipotee duniani,
   fundisho makuhani,nduguzangu shikeni,
   njiabwana nyosheni,mkakuone mbinguni,
   hiyodin freemasoni,ni dini ya motoni.


2.hiyo dini freemasoni, ni dini ya motoni,
   kwani yawadanganyeni,vitabu vyafunzeni,
   biblia na kurani,mwenyezi mwabuduni,
   assalamu alekuni,bwana asifiweni,
   amwabudiye shetani,kalaaniwa jameni.
  
3.amwabudiye shetani,kalaaniwa jameni,
   huyo yupo utumwani ,ataikosa peponi,
   anateswa fikirani, kwa kumwabudu firauni,
   mapepo na majini, umleta mikosini,
   utiwa masharitini,magumu majaribuni.

4.utiwa masharitini,magumu majaribuni,
   uwatupa kaburini,ndugu zake wa damuni,
   awezi aga umasikini, kwa kupenda rahani,
   fanya kazi juhudini, ujiwekee rehani,
   mungu sio athumani,kila riziki gaweni.

5.mungu sio athumani,kila riziki gaweni,
   leo watu tafuteni, kwenye milima bondeni,
   huko msujudieni,na sadaka toeni,
   zambi zenu tubuni, na zabihu chomeni,
   na ubani fukeni, shetani mfukuzeni,
   machozi lieni, mola awasameheni.

6.machozi yalieni,mola awasameheni,
   nendeni na jangwani,arobaini fanyeni,
   vizazi vitazameni, huruma vioneeeni,
   laana epukeni,mungu mtamanieni,
   hapa nina komeni mungu awabarikini.
                                                                                     dec 2012
 

No comments:

Post a Comment