Wednesday, October 21, 2015


TAM TAM ZA   ELIA
TUNGO TAMU ZA MAPENZI

1.    ETI MAPENZI NI NINI

Eti mapenzi ni nini?,watu tunajiuliza,

Hebu kaa kwa makini,uanze kujijuza,

Mapenzi yana thamani, au tuna yapuuza,

Eti mapenzi ni nini? watu wana jiuliza.

 

Ukiamua kupenda, hakuna akuulizaye,

Mazuri ukiyatenda,mabaya humfikaye,

Ata ukiamua kwenda, mapenzi huyakutaye,

Eti mapenzi ni nini? watu wana jiuliza.

 

Mapenzi ni kitu gani,chenye kuu maana,

Hata tukiwa nyumbani, twatafakari kwa asana,

Unafikiri ni nini, kama sio ni dhamana,

Eti mapenzi ni nini? watu wana jiuliza.

 

Mapenzi kama risasi,huruka tena kwa kasi,

Wala sio kama fisi,kuzeeka kwa wasi wasi,

Mungu katupa nafasi yawe pamoja na sisi,

Eti mapenzi ni nini?,watu wanajiuliza.

 

Mapenzi kama siafu ,ambao huwa pamoja,

Wala si kama sarafu,thamani yake ni moja,

Mapenzi wala si uchafu,watu kuwaletea vioja,

Eti mapenzi ni nini?watu wanaulizana.

 

          2. PENZI LA UA CHANUA

Ninakaa ninawaza,wewe kukufikiria,

Sijambo la kupuuza,kwa makini zingatia,

Ni vema kukuhimiza,mapenzini kutulia,

Penzi la ua chanua, chanua kama maua.

 

Mapenzi ni kama ndizi,tamu isiyo kifani,

Naukosa usingizi,mapenzi ndo yangu fani,

Hata kwa wale machizi, utulia mapenzini,

Penzi la ua chanua,chanua kama maua

 

Mapenzi kama shubiri,pale usipo yapata,

Kwa hima utasubiri,bila jawabu kupata,

Utaona kama dili, pale utapoyapata,

Penzi la ua chanua,  chanua kama maua.

 

Hata wale majambazi, utulia mapenzini,

Napatwa na bumbuwazi,haiingi akilini,

Hutulia kama ndizi,hasa wawapo chumbani,

Penzi la ua chanua,chanua kama maua.

 

Nakwambia utakonda, kwa kidonda cha moyoni,

Pale atapokutenda,ulomwifadhi rohoni,

Kamwe tena hutopenda, bara hata visiwani,

Penzi la ua chanua chanua kama maua.

 

   3.PENZI LAKE KWELI TAMU

Ni mjuzi anijuza,ndani hata nje pia,

Na mahaba anifunza,na kazi nayafanyia,

Kwa kweli sitopuuza,kwani yana raha pia,

Penzi lake kweli tamu, ni tamu kama asali.

 

Muda unapowadia,kitandani kuingia,

Shuka huniandalia,jeupe linonukia,

Na mito yenye maua,ndio naiegemia,

Penzi lake kweli tamu ni tamu kama asali.

 

Baridi nikisikia,yeye hunikumbatia,

Nami ninafurahia, kifuani kutulia,

Joto linapowadia, kwa huba hunipepia

Penzi lake kweli tamu,ni tamu kama asali.

 

Hunibusu kitomvuni,hunishika kiunoni,

Hupapasa mabegani,hunibusu na shavuni,

Mwengine simtamani,nahisi nipo peponi,

Penzi lake kweli tamu ni tamu kama asali.

 

Huruma unionea,kazi kunisaidia,

Nguo ananifulia,na pasi kunipigia,

Mimi ninafurahia,huba namzidishia,

Penzi lake kweli tamu ni tamu kama asali.

 

Pale ninapougua, kwa penzi hunitibia,

Nahafuu najionia,asante nampatia,

Kwani namuhamininia,ni dokta alobobea,

Penzi lake kweli tamu ni tamu kama asali.

 

Yeye ni dokta hodari, wa kuyatibu mapenzi,

Atibu kwa kila hali,na bila kipingamizi,

Ana vifaa halali,vifanyavyo nyingi kazi,

Penzi lake kweli tamu ni tamu kama asali.

 

   4 PENZI HALINA MWALIMU WALA YULE SULTAN

penzi si la kulaumu,ni chaguo la moyoni,

huwezi kulishutumu, kulipinga akilini,

lisije kukuhujumu,kukutia matatani,

penzi halina mwalimu wala Yule sultani.

 

Penzi latoka moyoni,kwa kila mwanadamu,

Haulioni machoni,hili jambo mfahamu,

Litakukakaba kooni,pia kukunyima hamu,

Penzi halina mwalimu, wala Yule sultani

 

Penzi si la kuchezea,katika hii dunia,

Popote linatokea,pasipo kutarajia,

Usije kulichezea,litakapo kufikia,

Penzi halina mwalimu, wala Yule sultani

 

Penzi si kitu adimu,ndani ya moyoni mwetu,

Wala haliishi hamu ,hii indo haiba yetu,

Pia halina ugumu, katika wetu utu,

Penzi halina mwalimu ,wala Yule sultan.

 

Penzi halina mwalimu,na wala kwa daktari,

Pia hukutia hamu,kuishi kwa ufahari,

Ukupeleka kuzimu,ukilichezea shari,

Penzi halina mwalimu wala Yule sultani.

 

Penzi halina shetani,ni kila viumbe hai,

Uingia akilini,pasipo kulipa rai,

Na hata masultani,pia nao wamewahi

Penzi halina mwalimu,wala Yule sultani.

 

Penzi halina heshima,hukugeuza mtumwa,

Hukuweka hima hima,puta utaja sukumwa,

Na wala halina bima,wala sio la kupimwa,

Penzi halina mwalimu,wala Yule sultani.

 

   5PENZI LA UA CHANUA

Kama penzi ni maua,kheri acha lichanue,

Uliache kuchanua,na mizizi lichipue,

Mizizi ikichipua, na tunda lifuatie

Penzi la ua ni mbegu, tunda katika matawi,

 

Penzi la  ua si duni,ni mapenzi ya fahari

Haijali asirani, hata kama huna mali,

Penzi la ua ni cheni inayo ng’ara shingoni,

Penzi la ua ni mbegu,tunda katika matawi.

 

Na kama penzi ni tunda,kheri liache liliwe,

Lisije likaja vunda,ukakosa utamuwe,

Uchumi ulipopanda,ulile wewe mwenyewe,

Penzi la ua ni mbegu tunda katika matawi.

 

 

Penzi laua huzuni,tena ni lenye huruma,

Halijali masikini,na kile alichochuma,

Huleta purukushani,pia na nyingi dhuruma,

Penzi la ua ni mbegu, tunda katika matawi.

 

Penzi la ua ni mbegu, mwenyewe nitazipanda,

Nitayatoa magugu,na wanyama kuwawinda,

Na yote miiba sugu,lisije likanishinda,

Penzi la ua ni mbegu, tunda katika matawi.

 

Ua litapochanua,litanitia furaha,

Tabasamu nitatua,litakalonipa raha,

Pia na kufurahia,kwa kulishinda karaha

Penzi la ua ni mbegu,tunda katika matawi.

 

Na kama virutubisho,vingi nitajizolea,

Itakua ukumbusho hukonilikotokea,

Penzi la ua fundisho nililolitegemea

Penzi la ua ni mbegu,tunda katika matawi.                    

 

 6.KAMA KWELI WANIPENDA NAOMBA UNIAMBIE

Ukiniona wacheka, aibu wanionea,

Pia huwa na mashaka,ukweli kuniambia,

Mimi sio malaika,kwamba mi nitaotea,

Kama kweli wanipenda, naomba uniambie.

 

Maneno nilisikia,kuwa wewe wanipenda,

Wanithamini pia na wala hutonitenda,

Kwangu ndo umefikia,na tena nitakulinda

Kama kweli wanipenda naomba uniambie.

 

Nami nakupenda pia,naogopa kukuambia,

Pale unapotembea, mimi nguvu huniishia,

Kwako nimeshakorea,machozi yajitokia,

Kama kweli wanipenda, naomba uniambie.

 

Nimeyasikia mengi, kuhusu wako ujana

Unapendwa nao wengi,na wana kupenda pia,

Tangu shule ya msingi,we ndo wangu mvulana,

Kama kweli wanipenda,naomba uniambie.

 

Wewe kwangu mfalme,malikia ndio mie,

Wewe ndio wangu mume ,kwengine usisogee,

Wewe ndio mwanaume, wengine ni manguluwe.

Kama kweli wanipenda naomba uniambie.

 

Tumia hii nafasi, wewe kwangu kufunguka,

Presha na wasi wasi,vinapanda na kushuka,

Unitibu upesi upesi,hata visivyotibika,

Kama kweli wanipenda, naomba uniambie.

 

Naomba niweke wazi,ili nije pata jua,

Nikuite laazizi ,nami unite dia,

Niondolie simanzi ,moyo wangu kutulia,

Kama kweli wanipenda,naomba uniambie.

 

 7.PENZI LETU LIKO POA

Waliosema siwezi,aibu wajionia,

Namuita laazizi,nae aniita dia,

Sitopatwa na mizizi, maneno ya umbea,

Mpenzi ametulia,penzi letu liko poa.

 

Nizipata natabu,wakati wa kumwambia,

Nizipata sawabu,mabaya kujiachia,

Aniita mahabubu,nami ninafurahia,

Mpenzi ametulia,penzi letu liko poa.

 

Sikwenda kwa mganga,na hirizi kupatiwa,

Nilimpeleka tanga,na mambo yakawa sawa,

Azipendaga karanga sasa mambo ni wawawa,

Mpenzi ametulia,penzi letu liko poa.

 

Mahaba nampatia , nae ayafurahia,

Macho namregezea,na nguvu humuishia,

Pale ninapotembea,na nguvu humuishia,           

Mpenzi ametulia, penzi letu limepoa.

 

Kwa mwingine hatokwenda, ahadi kanipatia,

Kwa yeye ananipenda, nami nampenda pia,

Kasema hatonitenda,yeye anihaminia,

Mpenzi ametulia penzi  letu liko poa.

 

Nampa ya moto moto,yaliyo anza kupoa,

Nampaka manukato,ashinda akinukia,

Yeye huniita toto,kwani ninamdekea,

Mpenzi ametulia,penzi letu liko poa.

 

Anaporudi kazini, huwa amejichokea,

Nampereka chumbani,kwani ameshanijua,

Akirudi sebuleni,uchovu ushamwishia.

Mpenzi ametulia,penzi letu liko poa.

 

 8.UKISHA PENDAGA BOGA.

Nikikumbuka ninalia,kwani nilimzoea,

Moyoni ninaumia,ninapomfikiria,

Mawazo yananijia,vema kuyapotezea,

Ukishalipenda boga ,ulipende na ua lake.

 

Ni kweli alinipenda,na pete kanipatia,

Na shangaa kanitenda,sababu ajizushia,

Eti mimi sikumlinda,virusi kumpatia,

Ukishalipenda boga,ulipende na ua lake.

 

Ilikua kama zali,mimi nilipo muambia,

Kutokana na dalili,nilienda kujipimia,

Majibu ya dakitali,mimi niliyapokea,

Ukishalipenda boga,ulipende na ua lake.

 

Tuliporudi nyumbani, ugomvi ajiaanzia,

Eti mimi ni shetani,kaburini ninamtia,

Mara mimi ni muhuni,akhera aingojea,

Ukishalipenda boga,ulipende na ua lake.

 

Ni kweli alifungasha,nami akanikimbia,

Na moto aliuwasha,virusi vikaenea,

Aliye mkaribisha,virusi alimgea,

Ukishalipenda boga,ulipende na ua lake.

 

Watu waliangamia,jamii  ukoo pia,

Na kinga hakutumia,ugonjwa ukaenea,

Kinga(dawa)zimemuishia,kabaki kujikondea,

Ukishalipenda boga ulipende na ua lake.

 

 

Mimi najinenepea,na dawa nazitumia,

Masharti najifatia,dokta alonambia,

Huruma na muonea,kwani ameshajifia

Ukishlipenda boga,ulipende na ua lake.

 

 9.PENZI  MPENI  RABUKA.

Pendo mpeni rasula,ndie mwenye haki,

Acheni toa kafara,wala hiyo sio haki

Pia acheni papala,mungu yote hayataki

Mapenzi mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula

 

Yatende mambo ya heri,fanya ibada kwa wingi,

Waepuke mataperi,hawana bora misingi,

Utunze wako uzuri,ujifunike ushungi,

Mapenzi mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula.

 

Saidia masikini,na wote wasiojiweza,

Wengi waketishe chini,mazuri kuwaeleza,

Uwapate kampani,ili kuwaendeleza,

Mapenzi mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula.

 

Epuka purukushani,watu usio wajua,

Utakua matatani,pasipo kujitambua,

Usije kuwekwa ndani,macho utayatumbu

Mapenzi mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula

 

Tenda yaliyo ya kheri,rabuka atafurahi,

Ujiepushe na shari,shetani asikuwahi,

Na pia acha kejeri,ndugu yangu na kusihi,

Mapenzi mpeni  rabuka,mapenzi mpeni rasula.

 

Fanya ibada kwa wingi,yaache mambo mabaya,

Upate bora msingi,motoni hutoingia,

Uache vuta mabangi,pia achana na umbea.

Mapenzi mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula

 

  10.MPENZI NIBEMBELEZE

Mpenzi nibembeleze,na tena nidekeze,

Usinifanye nikuwaze,tufurahi na tucheze,

Ukiweza nikupongeze,ukikosa nikuelekeze,

Mpenzi nibembeleze,usinifanye niwaze.

 

Nimezama kwa mapenzi,sijui kama nitazeeka,

Kujikwamua wala siwezi,taabani nateseka,

Ingelikua kama ni dozi,tayari ningeshamaliza,

Mpenzi nibembeleze usinifanye niwaze.

 

Nimezama,nimezama,kwenye kina kirefu,

Nimebaki natizama,moyoni Napata khofu,

Illahi mola karima,ndiye ataninahafu,

Mpenzi nibembelezee ,usinifanye niwaze.

 

Nibembeleze kwa zeze,nilale kwa utulivu,

Nipeti peti nidekeze,ili watu waupate wivu,

Nikuimbie nawe ucheze,wimbo wa utulivu,

Mpenzi nibembeleze usinifanye niwaze.

 

Mapenzi yalo adhimu,mimi yameniingia,

Simchezo yalivyo matamu,tena nayafurahia,

Watakao nilaumu,bado hawajayajua,

Mpenzi nibembeleze,usinifanye niwaze.

 

Nikulaze kifuani kwangu,ulipate langu joto,

Mahaba nikupe mazito,makubwa si ya kitoto,

Tuachane na michepuko penzi liwe lenye mvuto,

Mpenzi nibembeleze,usinifanye niwaze.

 

Tusiache kupendana,mapenzi kuyaboresha,

Watakaokuja kwa fitina kwetu sisi wamechina,

Tusiache kupendana,mapenzi kuyaboresha,

Mpenzi niembeleze,usinifanye  niwaze.

No comments:

Post a Comment