Monday, July 1, 2013

USHAIRI

USHAIRI
Utanzu wa Fasihi
Nyimbo
Fasihi Andishi

Kiingereza Poetry
Andishi Fasihi Simulizi



Ushairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha teule na mpangilio fulani wa maneno badala ya kutumia lugha natharia(mflulizo).
--------------------------------------------------------------------------------
Ushairi unaweza kuwa kipera cha fasihi simulizi (nyimbo) na pia katika fasihi andishi kwa sababu mashairi yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya kukariri na pia kwa njia ya maandishi. Mashairi yanayoghanwa badala ya kuimbwa huitwa maghani.
--------------------------------------------------------------------------------


Katika ushairi, tutaangalia:

KIPENGELE MAELEZO KWA UFUPI
Aina za Mashairi  Kuainisha mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti.
Bahari za Ushairi  Muundo wa shairi kulingana vina, idadi ya mizani, vipande, mpangilio wa maneno n.k.
Uchambuzi wa Mashairi Mambo muhimu unayohitajika kuzingatia unapochambua shairi
Uhuru wa Mshairi Ukiukaji wa kanuni za sarufi
Istilahi za Kishairi  Msamiati unaotumika katika ushairi km vina, mizani n.k
Sifa za Ushairi  Sifa zinazobainisha ushairi kutokana na aina nyingine za sanaa.
Umuhimu wa Ushairi  Umuhimu wa ushairi katika jamii.

--------------------------------------------------------------------------------


Istilahi za Kishairi
Haya ni baadhi ya maneno ambayo hautakosa kukutana nayo unapozingatia ushairi. Ni muhimu mwanafunzi kuyajua vizuri.

Shairi - ni sanaa ya maneno (utunzi maalum wa lugha ya kisanaa) unaotumia mpangilio na uteuzi maalum wa maneno na sauti ili kupitisha ujumbe fulani.
Vina - ni silabi za mwisho katika kila kipande.
Mizani - ni idadi ya silabi katika kila mshororo.
Mshororo - ni msitari mmoja wa maneno katika shairi.
Ubeti - ni kifungu cha mishororo kadhaa.
Vipande - ni visehemu vya mshororo vilivyogawanywa kwa alama ya kituo(,)
Ukwapi - kipande cha kwanza katika mshororo
Mwandamo - Kipande cha tatu katika mshororo
Ukingo - kipande cha nne katika mshororo
Utao - kipande cha pili katika mshororo
Mwanzo - mshororo wa kwanza katika ubeti
Mloto - mshororo wa pili katika ubeti
Kimalizio/Kiishio - mshororo wa mwisho katika ubeti usiorudiwarudiwa katika kila ubeti.
Kibwagizo - mshororo wa mwisho katika ubeti unaorudiwarudiwa kila ubeti.

--------------------------------------------------------------------------------

Sifa za Ushairi
Huwa na vina, mizani, mishororo na beti
Hutumia lugha teule
Hufupisha au kurefusha maneno ili kutosheleza idadi ya mizani
Mashairi hayazingatii kanuni za kisarufi. (Angalia uhuru wa mshairi)
Hutumia mbinu za lugha

--------------------------------------------------------------------------------

Umuhimu wa Mashairi
Kuburudisha
Kuhamasisha jamii
Kukuza sanaa na ukwasi wa lugha
Kuliwaza
Kuelimisha
Kuonya, kutahadharisha, kunasihi na kuelekeza
Kupitisha ujumbe fulani
Kusifia mtu au kitu
Kukejeli au kukemea mambo yanayoenda kinyume na maadili ya jamii

--------------------------------------------------------------------------------

No comments:

Post a Comment