STORY MASHINDANO TALENT SHOW
WRITTEN BY ELIA ABEL MWALUKALI
WRITTEN IN ARUSHA
(USA RIVER)
STORY WRITTEN ON MARCH 2014
Story ya kwanza
MASHINDANO TALENT SHOW
SEHEMU
YA KWANZA
DAR ES SALAAM TANZANIA
Ilikua ni hasubuhi
ya saa tano na nusu nyimbo za
music wa kitanzania zinazopendwa sana na vijana wa kizazi kipya almaharufu kama
bongo fleva zilikua zina sikika kwenye televisheni kubwa yenye screen ya rangi
nyeusi ikiambatana na midundo mikali hasa ya huo muziki, midundo inayoweza
kumto a nyoka pangoni ihari nyoka hataki kutoka.kijana mdogo Mwenye umri wa
miaka ishirini alikua amelala usingizi wa fofofo,pembeni ya kitanda kile
alilala mbwa mdogo mmoja mweusi na huyu
kijana alijulikana kwa jina la BOGA TALENTER.
Akaja babaye akamwita kwa sauti kubwa sana utadhania
kipaza sauti ;
“boga…….boga…..boga…….. “
lakini boga alienderea kulala
akinguruma kama vile simba mwenye
hasira.babaye Mwenye umri wa miaka 45 mrefu mnene,bado alionekana kuwa
kijana smart Mwenye mvuto wa kipekee
ukitegemea msomi yule alifahamu umuhimu wa kula vyakula bora vinavyotia nguvu
mwili pamoja na akili.
Babaye boga akaenda kwenye
jokofu akachukua maji ya baridi sana
taratibu akarejea kwenye chumba cha
cha mwanae boga talenter akafanya
uhamuzi wa kumwagia maji ya baridi palepale kitandani,yallab mola maji yalikua
ya baridi haswa utazania barafu za
milima ya ulaya,boga akashituka mshituko mkuu ulioambatana na kukurupuka pale kitandani akiwa
anatetemeka pamoja na kukamua nguo yake iliyolowa kwa maji yale ya barafu.
Babaye boga akamwambia kwa
ukari
Boga kwanini unalala
mpaka saa hizi badala ya kuamka ili
ufanyie makazi yote usafi.vyoo vilinuka,nyumba ilichafuka,viwaja vilioza,maua
yalinyauka lakini boga hakupenda kila siku kujishughurisha na shughuri za usafi
wa nyumba.Siku ya jana boga talenter alijisaidia chooni,lakini kwa bahati mbaya
alijisaidia pembeni na pia hakumwagia maji choo ukitegemea choo kilikuwepo
ndani,harufu kali ilijipenyeneza sebuleni kwao na kuwa kero kubwa sana kwa
babaye mzee talenter liyekua anafanya kazi kwenye kiwanda cha kutengenezea nguo
cha URAFIKI DAR ES SALAAM.
Babaye akiwa amefuraa kwa
hasira akamuuliza boga kwa nini tabia yake ni mbaya namna ile,kwanza
amejisaidia pembeni ya choo na kwa makusudi akiwa anaelewa kuwa maji yapo ndani ya choo na
pia toillent paper zilikua nyingi tena za kumwaga .Boga alishindwa kulijibu
lile swali hapo ndipo hasira za babaye zilianza kuwaka kama cheche za moto wa tanuru.Babaye akamchukua boga na
kumweka kwenye kiti kirefu,viti vile vitumikavyo kukalia mezani muda wa kula
chakula cha kifamilia akamwingiza ndani ya kile kiti na kumgeuzia kwenye
televisheni screen, huyo akaerekea nje akiwa anaongea pekee yake “naenda
kuchukua fimbo mjinga mkubwa we”.
Kichwa cha boga talenter
kiliangaliana na televisheni screen,ghafla televisheni ile ikaacha ku play
muzic yakafuatia matangazo likaonekana tangazo mtangazaji akitangaza kwa
mbwembwembwe kubwa.
“ mashindano talent show,kama wewe ni
kijana mtu mzima au mzee Mwenye kipaji au ubunifu wowote ule wa kuionesha jamii nini
mwenyezi Mungu amekujaria njoo uioneshe jamii na mwisho wa mashindano talent
show mshindi au washindi atajinyakulia au watajinyakulia pesa tasilimu milioni mia nane…..waoooooo………”.
mtangazaji akaenderea;
“ fomu zinapatikana barabara
ya mwenge eneo la bamanga karibu karibu na ofisi za kampuni ya habari na
mawasiliano ya GLOBAL PUBLISHERS mamilion ya pesa yatashindaniwa,wahi sasa
nafsi ni chache”.
Baada ya kumalizia lile
tangazo yakarushwa mamiliion ya pesa
kwenye kioo cha televisheni.
Ghafra boga akahisi kama kuna kitu kimempasukia nyuma kwenye makario yake maumivu makari aliyasikia yaliyoambatana na uchungu aliousikia kumbe babaye alianza kumcharaza
viboko vya nguvu pamoja na kulalamika kuwa siku hizi boga amekua na tabia mbaya
tena isiyofaa kuigwa kwani kuoga mwilini haogi,kufuta deki chumba chake hafuti
hata akiambiwa hawezi kuitii au kuisikiliza sauti ya babaye, mtoto anawaza kula
na kulala,sasa amejisaidia chooni je ni nani atakaye hangaika kwenda kusafisha
kile choo zaidi ya mshenzi mwanaharamu yule boga talenter.Babaye akamtandika
viboko kumi na viwili,boga alilia sana,baba nisamehe sitaweza kurudia
tena,nimekosa najuta nimekosa sitorudia tena.
Hasira zilizidi kumuwaka babaye boga talenter safari hii akautwaa mkono
wake na kuupachika kwenye sikio la boga
talenter maumivu makari yaliyoambatana na churuziko la damu kwenye sikio ndiyo
aliyo yasikia bogatalenter,babaye akamvuta boga talenter mpaka nje ya lango la
getini kisha akamsukumia nje boga, boga akaanguka na kuhumia vibaya sana kwenye
got lake la kulia churuziko la damu nalo likafuatia, babaye Mwenye hasira za
mkizi akamwambia boga;
“kuanzia leo nisikuone hapa nyumbani kwangu umbwa we ,mchafu mkubwa
usofunzwa na mamayo ufunzwe na ulimwengu,kwenda zako huko”.
mzee talenter akaingia ndani na kuchukua nguo mbili tatu za boga akamrushia kisha akamwambia “toka…toka..toka…,usirudi
tena na wala nisikuone tena hapa ntumbani nenda huko huko kwenye makundi yanayo
kudanganya mtoto umejaa laana wewe,
Tangu kufariki kwa mamayo miaka mitatu iliyopita ,umepangaruka akili
hata kwenda shule unaona kama ni kazi kubwa sana,unashinda mitaani kijana mdogo
wa kidato cha nne hupendi kujifunza hufahamu ya kwamba elimu haina
mwisho……unaipuuzia elimu ondoka haraka
nisiione sura yako iliyo komaaa utadhani mbuzi”.
Boga talenter alikuakijana
mrefu, Mwenye umbo pana nene lililojazia kwa sababu ya mazoezi ya viungo aliyozoea kuyafanya kila
siku chumbani kwake.ila ukimwangalia alivyopaa hewani unaweza ukadhaniani ni mtu mzima Mwenye umri wa miaka 35 kumbe ni
mwili tu unaomsumbua,alijariwa sura nzuri yenye utanashati wa kumvutia kila
mwanamke mrembo au msichana mrembo ingawaje alikua na nyota ya mvuto vijana
wenzake wengi mtaani pao walimchukia na kudai kuwa hapendi kujiweka safi
kimwili kwa kifupi vijana wenzie
walimfananisha na nguruwe vile.
Boga akaondoka pale Nyumbani kwao UBUNGO KIBANGU mtaa wa makoka,akiwa
analia chozi lililoambatana na
maumivu ya sikio pamoja na
maumivu ya goti alilokua anatembea akiwa anachechemea,ingawaje watu wengi
walimwona walibakia kumsikitikia tu kwa jinsi alivyo onekana,lakini hawakuweza
kumsaidia kwani alikua na speed kari
utadhania ndege ya AIR TANZANIA, akakatiza barabara kadha kutoka kibangu kwenda
ubungo akapita mawasiliano toure akavuka kanisa la mchungaji kakabe la full
gosper bible fellow ship ,akatokezea mlimani city akajivuta zaidi eneo la soko la mwenge Sasa akapunguza speed na kuanza
kutembea taratibu akihema kwa kasi ya
ajabu kwani alikimbia speed nyingi na ukitegemea kutoka ubungo kibangu
kwenda mwenge ni kilomita kadha, akajipereka mbele zaidi hapo akafika eneo la
bamanga.
Boga akajivuta vema kwenye chuo kidogo cha maendereo ya jamii karibu
sana na kituo kikubwa cha televisheni cha TBC, huko akabadirisha nguo zake
chafu kishaakavaa zile safi ingawaje zilikua chakavu chakavu ukitegemea
halishindwa kuzitunza vema kwa vile hakuwa na mazoea ya kuweka mavazi yke
mahali pa safi,akajiingiza kwenye kikundi cha vijana waliokuwa wanachukua fomu
za talent show.
Nayeye akachukua fomu zile kisha akamsogelea binti mrembo
aliyejitambulisha kwake kwa jina la PAMERA,binti alikua amevaa mavazi ta
gharama kiatu kikali haswa kama sio cha laki tatu basi ni cha laki mbili na
nusu,mkoba alioubeba ulidhihirisha ya kwamba kuna kiasi kikubwa sana cha pesa
ziko kwenye ule mkoba kulingana na mwonekano wake jinsi alivyoonekana pamera
alionekana kama anatokea kwenye familia moja inayojiweza kifedha.
Boga talenter akamwambia pamera samahani sana sister utakapomaliza
kuitumia pen yako naomba unisaidie na mimi nahitaji sana.pamera akamwangalia boga
talenter kuanzia juu ya nywele za
utosini mpaka chini ya miguu yake kisha
akatabasamu tabasamu pana lililoashiria
furahaa fulani ya ghafla ingawaje boga talenter akujali ilo kisha akamwambia
nitakusaidia nikimaliza kuandika.
Boga talenter akasubilia mpaka hatua ya mwisho aliyochukua pamera ya
ujazaji wa ile fomu alipomaliza akampatia boga talenter ile pen yake aina ya
spidor nyeusi boga akiwa hana ili wala lile alienderea kujaza ile fomu ,lakini pamera alienderea
kumwangalia kwa jicho la husuda na tamaa ya kumpenda.
Lakini katika kumtazama tazama boga talenter pamera akaiona michirizi
ya damu nyepesi kwenye got la boga,pamera
akashtuka kdogo kama vile ametetemeshwa na umeme,akamuuliza boga ni nini
kimemsibu mpaka michirizi ya damu ile
boga akamtazama pamera lakini akashindwa kujibu,pamera akaiona michirizi
mingine ya damu pembeni ya sikio la boga,macho ya boga yalionesha kutoa machozi
ingawaje macho yale mekundu hayakudondosha
hata tone la chozi.
Pamera akapata mwanga kuwa mvulana yule Mwenye sura ya kiutanashati
atakua anahitaji msahaada wa haraka sana iwezekanavyo.Baada ya kumalizia ile
kazi yao ya ujazaji wa fomu za mashindano talent show wote kwa pamoja waka submitt zile fomu pamera
aliyekua na gari lake aina ya MERCEDENZ
BENZ nyeusi, akamchukua boga talenter akamwambia amfuate hospitarini jambo
ambalo boga talenter hakulipinga.
Alipokua anatembea kwa kuchechemea vijana waliokua wanachukua fomu baadhi
yao waliziba midomo yao na pua zao kwani harufu kari ya kwapa pamoja na domo la
boga liliwachechefua achilia mbali mwili uliojaa mapere mapunye na makovu
yasoeleweka chanzo chake ni nini.
Boga kwa uchafu aliita fora hata mara kwa mara alifukuzwa shule ili awe
msafi lakini hakujirekebisha.
Pamera akamchukua boga mpaka hospitary kubwa ya muhimbili,huko boga
akapewa matibabu yote ikiwemo ya kurekebisha goti lililopinda na kuzuia kutoka
kwa damu kwenye sikio lake na kwenye goti lake.
Lakini kabla ya hapo pamera alimpatia boga talenter first aid kwa
kumsafisha vizuri goti na sikio, kumtia dawa aina ya spirt na kumfunga kwa
kutumia bandage sehemu zote mbili sikioni nagotini,ndipo wakaelekea hospitarini
kwa ajiri ya uchunguzi na matibabu zaidi na walipomaliza kupewa huduma zote za
kitabibu pamera akagharamia kiasi cha shilling elfu hamsini hao wakaondoka zao.
Sasa pamera na boga taratibu wakaanza kuzoeana ,pamera yule binti Mwenye umri wa miaka ishirini na
miwili,mrefu mnene kiasi mweupe Mwenye rangi ya chungwa lililoiva, alijazia
hips,matako yake mazito mfano wake
hakuna, achilia mbali mguu wake wa bia ulo watamanisha sana vijana wengi wa kiume pale MAKONGO HIGH SCHOOL,alikua ni binti wa geti kari aso
patikana kwa uraisi.
Binti yule mrembo sasa akazidiwa
kwa matamanio yake kwa yule kijana mchafu ingawaje mtanashati,pamera akamtwaga
swali boga talenter;
“vip unaye mpenzi wako wa kukuriwaza”.boga akajibu akiwa na aibu usoni pake
“ la asha!! Sina”
pamera akamuuliza tena;
“ kweli huna”.
boga akatikisa kichwa chake
ikiwa ni ishara ya kuhafikiana na lile
swali,pamera akamwambia boga;
“ naitaji uwe wangu wa moyoni”.
boga akacheka na kujawa na aibu
usoni baada ya dakika chache akasema;
“ hamna noma sister hata mimi nime kuzimikia haswa”.
Oooosh……… pamera aliyekua anaendesha
gari akapumua pumzi nzito iliyoambatana na harufu nzuri ya marashi yaliyonukia
mwilini,alifurahi sana kukubaliwa ombi lake
walipofika mataa ya ubungo pamera akasimamisha gari ili taa za kuruhusu
magari ziwape nafasi ,kisha akamsogerea boga na kupiga busu la shavuni akatamka
neno moja la kimahaba I LOVE YOU BOGA boga
naye aliyekua anachekacheka akajibu ILOVE YOU PAMERA.
Pamera akamuhuliza boga ni wapi anapoishi boga akamwelekeza njia ya ubungo kibangu gari
iliporuhusiwa kupita pamera akalitoa gari lake moto moto huyo akakata mitaa miwili mitatu kisha wakawa wamesha
wasili Nyumbani kwa wakina boga talenter.gari ilipofika Nyumbani kwa wakina
boga talenter pamera alishuhudia nyumba ikiwa ni chafu haswa kila eneo hali iliyomfanya pamera ajiulize maswali
inakuaje nyumba ni chafu namna hii je wanaishi watu mahari hapa maswali
yalilindima kichwani mwake paso majibu.
Akakaribishwa ndani ndani namo mlimstaajabisha sana kwa uchafu wa namna
ile ila kwa vile yeye ni mwanamke na kwa asilimia kubwa wanawake wanapenda sana
suala la usafi.
Akamwambia boga anaitaji kupaweka mahari pale pawe safi na penye mvuto.
pamera akawaita vijana wa kike watatu pamoja na vijana wa kiume wawili kwa njia
ya simu yake ya mkononi,vijana wakawasili kama walivyo mwahidi kufika
mapema,kazi ya kuipamba ile nyumba ikaanza .chap chap kama vile mashindano ya
farasi wakimbiavyo,vijana wakaisafisha ile nyumba vizuri wakapanga kila kitu
mahari pake, wakafyeka zile nyasi ndefu utadhania nywere za wanawake wa asili
ta kiasia yaani wahindi.
Bahada ya kumalizia kushirikiana vizuri katika kuipamba ile nyumba pamera
akawalipa wale vijana posho zao,vijana wakamshukuru sana wakamweleza kuwa iwapo
akiwahitaji tena wao wapo tayari kwa msahada atakaohitaji .
pamera msichanma yule aso aibu akamsindikiza boga talenter bafuni huko akamsafisha vizuri mpenzi wake, kisha akamtaka waende shopping
hao wakaerekea MADUKANI BOTIQUE huko
akamsasambulia viwalo special,viatu
vizuri pea tatu,laba za ngozi pea mbili,shirt tatu za kitambaa cha sufu,tshirt tatu pamoja na trouses tatu zote aina ya
jeans.
Bibie huyo Mwenye huruma zake akampeleka boga talenter BARBARING kunyoa
nywele zake ili kichwa kiwe swaafi boga akapenderea style ya kiduku style
inayopendwa sana na vijana wa kisasa wanaojiita MASHAROBARO au wasafi classics maana safari hii boga naye
alikua msafi hasa,pamera aligundua kuwa boga talenter hana pocket money
akaingiza mkono wake na kutoa burungutu la pesa
tasilimu shilingi million moja akampatia mpenzi wake mpya boga
talenter,boga alifurahi sana shukrani alizozimwaga boga zilikosa kuhesabika alimshukuru sana
pamera akamwona kama ni mkombozi wake.bahada ya manunuzi yale pamera
akamrudisha Nyumbani boga talenter akamuaidi kuja kumchukua siku iliyofuata.
Pamera alikua ni binti wa tatu katika familia ya Mr and Mrs Patrick ludoslovic ludwing na
katika familia yao walizaliwa wote wakiwa ni wasichana dadaye wa kwanza aliitwa
penslavia dadaye wa pili aliitwa penielia na yeye pamera alikua ndio kitinda
mimba katika familia ile.Babaye pamera
alikua anamiliki kampuni yake ya kununua na kuuza magari ina ya PAJERO,LAND
CRUISER,MITSUBISH,LAND LOVER,TAX,MERCEDENZ BENZ,TRECTORZ,BAJAJI na Mapiki piki
aina ya TOYO na BAJA.Mbali na kuuza
magari pia alikua na biashara yake ya kuuza na kununua madini aina ya GOLD,DIAMOND
na TANZANITE,ndio hizi biashara zilizompatia pesa na umaharufu jijini
Dar es salaam kwani watoto wake walisoma vizuri,walikulavizuri,walivaa vizuri
,walihishi kwa fahari sana tofauti na familia nyingine nyingi za majirani waliowazunguka.
Mamaye pamera alipenda sana kujushughurisha na shughuri mbali mbali za
kiuchumi lakini babaye pamera Mwenye asili ya watu wa ROMA ITALIA ,alijawa na kaji wivu kidogo
hivyo hakumruhusu mkewe kujishughurisha na kazi za biashara zaidi ya kukaa tu
na kustarehe.
Pamera na wazazi wake waliishi kwenye jumba la kifahari sana kwani
jumba ilo lilikua ni ghorofa tatu na kila kitu kilikuwepo ndani,kuanzia
wafanyakazi, walinzi pia huduma za DISPENSARY
yao wenyewe ilikuwepo.
Mchana ule babaye boga akawasili Nyumbani kwake akakaribishwa na harufu
nzuri ya marashi aina ya PERFUMER JELLY
kwanza alistaajabu kuona nyumba yake imebadirika ghafra ,kwani
hakutarajia kuyaona yale mabadiriko,taratibu akajongea mpaka ndani huko
akasikia sauti ya kinanda ikitoa music mwororo,walipokutanisha macho wote kwa
pamoja wakatabasamu boga akaanza kuimba wimbo wa siku maalumu ya kuzaliwa
babaye maana siku ile ilikua ni siku maalumu kwa ajiri ya kuzaliwa babaye,
Happy
birth day to you,……happy birth day to you,
Happy
birth day dear father,……happy birh day toyou
How old are you……..how
old are you
How
old dear father…….how old are you.
Alipomaliza kuimba ule wimbo haraka haraka boga talenter akaamka kwenye
kiti alicho kalia akamsogerea babaye akamkumbatia naye babaye akamkumbatia pia
wote wakawa ni wenye nyuso za furahaa iliyo kuu.Babaye akamwambia boga
talenter mwanangu mbona umenifanyia
supprisment ya nguvu namna hiyo nyumba imebadirika ghafra,boga hakujibu kitu
ila tu almwabia babaye
“Dady ….,dady .umesahau
kwamba leo ni siku yako muhimu ya
kuzaliwa”.
Dady akasema
“haloow!!! thanks so much my son”.
basi dady akaisogerea ile meza,wimbo wao ukaenderea safari hii
waliuimba kwa Kiswahili.
Kata keki
tuleeee……..kata keki tuleeeeee
Kata keki dear dady…….kata keki
tuleeee
Dady akakata kipande cha keki akamlisha boga naye boga akafanya hivyo
hivyo akamlisha dady.baada ya furahaa yao kurindima boga talenter akamsimulia
babaye mwanzo mpaka mwisho jinsi alivyo
kutana na pamera kwenye mashindano ya talent show,jinsi pamera alivyo mtongoza
boga mpaka kuja kufanya usafi wa nyumba pamoja na kumpeleka shopping ,hakusahau
kumweleza kuwa ni huyo huyo pamera aliyem peleka boga talenter hospitary ya
muhimbili.
Mzee talenter alifurahi sana
maana alijua kua sasa mwanawe anaelekea kuwa kijana mtu mzima,pia yale
mabadiriko ya harakaharaka yalimvutia sana mzee talenter alimpongeza sana
mwanawe akamtaka awe na juhudi zile zile kila
apatapo muda na nafasi,pia
alimtaka mwanawe kuzingatia masomo ihari alimruhusu kwenda mashindano talent
show
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Itaenderea toleo jalo……usikose tuwe pamoja
No comments:
Post a Comment