Friday, October 28, 2011

''MUZIKI WA ASILI USISAHAAULIWE NI UTAMADUNI WETU''

Muziki  ni ala .....lakini kwa kamusi sanifu ya kiswahili muziki umeelezwa kama mpangilio wa ala na uimbaji unaoleta adhari fulani kwa kiumbe hii ina maana kwamba kama msaani wa muziki hapangilii ala zake na kuimba kwa ustadi basi anachofanya msaani huyo sio muziki bali ni kelele za kawaida tu.
   Muziki ni saana kama zilivyo sanaa nyingine hivyo hatuna budi kujua sanaa ninini ?hasa sanaa imeelezwa kama ufundi,ufundi wa kuwakilisha mawazo yaliyomo katika fikla za binadamu ili ya dhiirike na kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa walengwa
    Hivyo sanaa inakubali kuwa na malengomakuu ambayo ni

                  1.KUELIMISHA JAMII
                  2. KUBURUDISHA
                  3, NA HATA KUELEKEZA JAMII
         Sanaa pia ni utambulisho wa jamii husika hata kama haujawai kuishi na jamii hiyo....itakuwa kosa kubwa kama tutaisahau sekta hii ya muziki katika jamii yetu
                Muziki una historia ndefu sana tena isiyo yumba katika ustawi wa jamiiya binadamu.muziki pia umezisambaratisha ndoa na familia nyingi,muziki umewatoa watu machozi ya furaha na huzuni...Wanasayansi bado wana kesha  katika maabara kubwa duniani kutafiti ni kwa nini muziki una adhari kubwa katik ubongo wa binadamu......muziki umetumiwa kama dawa kwa wagonjwa wa wa akili na walio na msongo wa mawazo, lakini kuna mkanganyiko mkubwa baini ya muziki wa asili na na ule wenye vionjo vya usasa

            Basi nini tofauti kati ya muziki wa asili na ule uliochanganyika na usasa
       Muziki huu wenye vionjo vyaasili ni ule wenye usasa lakini una vionjo vya asili.....unaposimama na kuzungumzia muziki wa asili basi ni vema ukatafakari kwa makini ni muziki upi ambao unachukua jukumu la kutambulisha utamaduni na asili ya mtanzania ...mara nyingi wasaani wa muziki wa asili wamekuwa wakifanya  kazi  zao nchi za nje wakiutangaza utamaduni wetu tofauti na hapa nyumbani.Hili limekwisha kuwa tatizo la watanzania wenyewe  kushindwa kuuenzi muziki huu hivyo wasaani wengi wamejikuta wakifuta muziki huo ambao unatukuzwa na mataifa mengine ya huko nje..
  Hii huenda kuwa ndiyo sababu iliyowafanya hata waandaaji wa tuzo hapa nchini kutozingatia makundi halisi ya muziki wa asili wa asili kushirikishwa katika tuzo hizo.hata hivyo serikali ina dhamaaana ya kuendereza muziki wetu  kwa kuzingatia kutoa vipaumbele  kwa makundi ya saana ya muziki  wa asili ili kuweza kuuenzi sisi wenyewe ni aibu kubwa ikiwa sisi watanzania wenyewe hatufahamu vema muziki wa asili  na hii ni sababu tunashindwa kuhuuenzi utamaduni wetu , ni vigumu kujuwa iwapo hatuuenzi .serikali ina wajibu wa kujenga ukumbi wa kisasa kwa shughuri za sanaa  na kusimamia mikataba halali  kwa wasani ili kuweza kutoa kipaumbele  hivyo na pia  kutatua matatizo kadha ambayo yamekuwa yakiwakumba wasaani hao
        
            Pia vyombo vingi vya habari havitoi kipaumbele kwa sanaa na wasaani wa muziki wa asili hili ni tatizo pia kwani linafifisha utamaduni wetu na hata wadau mbalimbali wanashindwa kutambua vema muziki wa asili kuna haja ya kuanzisha tovuti mbali mbali ambazo zitakuwa zikitoa taharifa mbali mbali  kuhusu muziki huu na hata vipindi mbali mbali maaalumu katika television na radio mbali nchini.... kwani kuna makundi mengi na wasaani wengi wa asili kama vile saida kaloli,jhikoman, mbeya arts, na baadhi ya wasaani wanaotambulika kuwa ni waimbaji nyimbo za asili

               kuna haja kwa watanzania kubadilika ili tuupende,tuuenzi na kuheshimu vya kwetu kwani mwenda kwao si mtoro/mtumwa.....mcheza kwao hutunzwa.hipo siku tutavipoteza kabisa vya kwetu nakuwa watumwa wa mataifa mengine.......
                              
                               ASANTENI  SANA NA KWAHERI

                  .....................................................................
                     $$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$
                         %%%%%%%%%%%%%%%%%%
                            **************************
                               ^^^^^&&&&&&&&&&!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment