Tuesday, July 19, 2011

OOOOOSH... MASIKINI ALA YA SAXAPHONE HATARINI KUTOWEKA KATIKA MUZIKIII......?

Wanamuziki  wa sasa hawataki kujifunza ala ya saxaphone  hata waliopo umri unawatupa katika fani
   saxaphone maarufu kama ala za upepo ni miongoni mwa vyombo muhimu va muziki  vilivyo hatarini kutowekan katika muziki wetu  hapa nchini kwa sasa
    Nchi nyingine kama za ulaya ala hiyo inatiliwa mkazo hadi kupendwa zaidi  bemdi cmuziki kama mlimani park na msondo ngoma ndio pekee zinazo weza kutumia ala hizo katika nyimbo na muziki wao
          baadhi ya sababu zinazofanya saxaphone kupotea
    1 matumizi ya kinanda [key board] kunako fanywa na bendi pamoja na vikundi vya muzik nchini

    2.hali ya vijana kutokuwa na moyo wa kujifunza ala hiyo
          sio hivyo tu ala nyingine kama magita hali ni mbaya sana kwani vijana wanashindwa kujifunza ala hizo
    3.utandawazi unaoenderea pamoja na matumizi ya sayansi na tecknologia  na faida zake lakini kwa upande mwingine umechangia kuua vipaji vya wanamuziki vijana katika zama hizi
     uko ulaya na marekani nchi zilizoenderea zinatumia tecknologia yao sio kwa kukuza tu ata kudumaza utamaduni wetu nchini na africa kwa ujumla baada ya kufanikiwa kuua ala za upepo nguvu sasa  zinawekezwa katikaupigaji wa magita
      serikali sasa pamoja na wanamuzik WANATAKIWA KUWA MAKINI SANA NA JAMBO HILI  KWANI WATAALAMU WANAFADHILI MIDUNDO MILINDIMO KWENYE KOMPYUTA  KWA NIA YA KUZITENGENEZA HAKI MILIKI  KATIKA MIDUNDO ''MECHANICAL RIGHT''.      

       KWA VILE HATUANDAI VIJANA WETU  KUJIFUNZA KUTUMIA ALA  HIYO ITAKUWA NGUMU KUPIGA MUZIKI WETU  KWANI ITABIDI TUNUNUE MIDUNDO NA MAPIGO KUTOKA KWAO . KIBAYA ZAIDI MIDUNDO NA MAPIGO HAYO  YATAKUWA YANAUZWA KWA BEI GHARI  NA KWA BAHATI MBAYA SANA HATUTAKUWA NA UWEZO WA KUNUNUA.
        Jukumu la matunzo haya zisiachiwe taasisi za dini tu kama ilivyo kuwa nyuma  hasa miaka ya 60 na70.Ala nyingine ni trumpent  na trombone  zimo hatarini kupote
        tatizo la saxaphone kwa kweli ni ghari yaani ni ya gharama sana katika maduka ya muzik kwa mfano bei ya saxaphone inaweza kugharimu bei ya magita matatu ya solo [leading guitor] rydhim na base  na kufanya upatikanaji wake kuwa mgumu  sana          


    Bado sisi watanzania hatujaweka malengo kuwepo kwa saxaphone katika ustawi wa muziki
Serikari inatakiwa kuliangaria sualahili kwa macho manne ilikuakikisha chombo hicho kinaenderea kuwepo katika muzic wetu badara ya kutegemia muzic wa magita matatu..  kama ilivyo katika beni za africa star,akudo impacts,extral bongo na nyinginezo.

     TUNAIOMBA SERIKARI ,WANAMUZIC, WASAANI NA WADAU WA MUZIC NCHINI KUFANYA  KILA NJIA KUKINUSURU CHOMBO HICHO NA JAMII ZAKE NA IKIWEZEKANA ITILIE MKAZO MATUMIZI  YA ALA ZA ASILI KAMA VILE   ZUMARI,FILIMBI,ZEZE,VILIMBA,NGOMA, LITUNGI  NA VINGINEVYO.....

ASANTENI.....PAMOJA DAIMA  ......

          TETEA SANAA YAKO....

          MUZIKI NI BURUDANI
          INAYO ANZIA NYUMBANI.
   *****************************

Wednesday, July 13, 2011

.........NAKERWA NA TABIA HII YA WANAMUZIKI WETU.......

Nimbo za wasaani wetu zimeenderea kuwa za aina moja
ingawa zinaimbwa na wasaani tofauti wakati mwingine unaona wasaani ni wawili au zaidi lakini aina hiyo ya utunzi hufanana utunzi ufanana kwa kiasi kikubwa  jambo ambalo binafsi linanikera sana.......

Ni hapo ninapoanza kuoji uelewa  na vipaji  vya wasaani wanaoshindwa kufanya kazi nyingine zaidi ya sanaa  sasa nyimbo ni za aina moja sasa utata unakuja zinapokuwa ni za mapenzi  ni jambo baya kupita kiasi  maana wakati mwingine mashairi ni yaleyalr  ila wanacho fanya ni kuyapindua juu chini au kulia na kushoto

hHili ni kushangaza  kama sio kuhuzunisha  lazima wasaani wenyewe mjitambue  kuwa nyie ni nani na mnafanya nini  na sanaa kwa ajili ya nani na nini  huu ni utumbo na unatakiwa upigwe vita na wadau wote  wakiwemo wasaani wenyewe wanaofanya kazi kwa kuangalia  na kuyabadirisha ili tungo hizo zionekane ni tofauti

Msaani  kama hana uwezo wa kuandika mashairi yake  ni vema akaachana nayo ili ajifunze kama mungu amempa kipaji  na hafanyi mzaa kwa kuuza sura na nyimbo mbaya au nzuri lakini imewai tungwa  na wasaani wenzao waliohumiza vichwa  kwa ajiri ya kazi hiyo

sanaa ni kazi kweli  lakini sio kwa wasaani wetu  kuona mtindo mzuri ni kubadirisha aina ya mashairi ya wenzao  na kuimba wao  tena jambo linalo fanya tungo zao kufanana kiasi kikubwa

Unafikia wakati  mtu anashindwa kutofautisha wasanii husika  kutokana na kero hiyo ya kuchakachuriana nyimbo zao wao kwa wao  kwa kuigana kiajabu ajabu  bila haya kwa wahusika


vichwa si navyo  na mnajiita kweli wasaani , sasa huo mtindo wa kuigana nyimbo zenu  kama kasuku una tokea wapi....please   and please tuache wizi mtupuuuuuu... kama sanaa imekushindeni tafuta kazi nyingine itakayo kuretea kipato na sio kufakamia vya wenzenu................................

                           tumia jasho lako.......

Tuesday, July 12, 2011

WANYAKYUSA..... HURITHI WAKE ZA NDUGU ZAO WANAPO FARIKI......

wanyakyusa ni kabila linalopatikana mkoani mbeya
wanaume ulithi wake pale inapotokea mume amefariki
mila hii ipo kwa wapogoro, wahee na makabila mengine
kwa sasa mila hii imepungua kutokana na presha ya watetezi
wa haki za binadamu na kutolewa kwa elimu inayoelezea ubaya
wa jambo ilo. zamani mila hii ilipew kipaumbele sana ndugu
waririthi mali nyingine za marehemu kama vile mashamba na
walikuwa wakipiga mahesabu na wake zao....
 
wakati wa msiba huwa kama wanaanzisha makazi kwa kwenda na vitu vya nyumbani  kama
vile mswaki mataulo na vinginevyo.....walifanya hivyo eti kwa kisingizio kuwa marehemu aliacha watoto wadogo wa kuwatunza

wapo ndugu walio lemazwa na fikra hizo  ndugu yao anapoumwa upiga mahesabu ndugu yao atakapo kufa warithi chochote kizuri ..... mwanamke akikataa kurithiwa na mume mpya utengwa mbali sana.......... lakini
kwa vile sasa kuna utandawazi na sheria kari watu ao wameanza kupunguza mila hizo

            ''  TUNAOMBA CHONDE CHONDE SERIKALI
HIINGILIE KATI HIZI NI MILA POTO
FU  KAMA TUTAENDEREHA KUKUMBATIA MILA HIZO ULE UGONJWA WA UKIMWI KAMWE HAUTAPUNGUA''
     ASANTENI.........

JINI AITWAYE ''MAIMUNA'' Saqiwtwaye

jini aitwaye maimuna saqitwi  huyu ni shetani mwovu  na umtia mwanadamu athari nyingi sana ...jini huyu aitwaye saqitwi l-jini akimnasa binadamu humsababishia  mikosi  maradhi  kuchukiwa au kuchukia.....

         jinsi anavyo mletea mwanadamu mabalaa
       1.kuumia kwa ajali mbaya mfano safarini,
       2.kudhulumiwa mali zako,
       3.kusingiziwa usilo litenda,
       4.kuhisiwa kuwa wewe ni mchawi,
       5 kuvamiwa na wezi au maadui zako hata kama hauna mali wan
         akuja kukutesa tu
       6.kupatwa na mikasa na askari na kufungwa tu 
       7.kukosa kila bahati
       8.kukataliwa/kukataa kuoa au kuolewa hapendwi  kutopata ba
         hati ya kuoa  kila mkienda wakataliwa
       9.wachumba wengi lakini ndoa hakuna
       10.viungo kukosa nguvu ukiwa kwenye masomo ,
       
          
                BAADHI YA MAGONJWA YA JINI MAIMUNA

         1kuchezwa chezwa na nyama kwenye mwili
         2.ganzi mwilini
         3kukaukwa na koo na kuchomwa kooni kama moto
         4kiungulia na kutapika mapovu
         5kuumwa kichwa na kuisi kitu kinatembea utosini
         6.kupatwa na ganzi kichwani ,laki inahamahama  
             na kwenda sehemu nyingine
          7.kuumwa tofauti tofauti mwilini mfano ugonjwa ukiwa k
             wenye miguu unaenda sehemu nyingine mfano mgongoni
          8 kushituka kujirusha kughara ghara ovyo usingizini na
             kucheka cheka ovyo .
          9. kusonya kila wakati usingizini na kutukana tukana
          10.kupoteza isia zote mwilini asa hisia za tendo la
              ndoa
          11.kuzaa watoto wabovu hata kufa kila mtoto atakaye zal
              iwa.
          12.kuzaa watoto wenye ulemavu
          13. mimba uweza kupitiliza miezi kumi na mbili na m    
                  toto atakaye zaliwa ufa
                
   
         
                    ....ASANTE NI SANA........
                       ''naomba toa maoni yako ili kuongeza mawazo yako''