Sura ya nne
FASHION SHOW
Baada ya pumziko fupi la siku tatu kuisha makundi yote matano pamoja na
washiriki walikutana tena safari hii
hadhira haikupewa nafasi ya kushiriki kwani
kwa siku tatu za mbeleni washiriki walipaswa kubuni mavazi na
mitindo mbalimbali na baada ya siku
tatu hadhira ilipewa nafasi ya
kushuhudia mizigo mipya kutoka kwa vijana wenye vipaji na ubunifu wa
hali ya juu.
Siku hiyo vitambaa vya aina
mbali mbali walipewa vilikuwepo vya
utamaduni wa kimasai maharufu kama lubega, ngozi za wanyama kama vile
pundamilia,simbachui,chetta,ngombe,kondoo,manyoya ya kuku,kanga,tausi,kuku na
mikufu havikukosekana.
Vitambaa vya sufu,vitambaa
vya pamba na vinginevyo laini laini walipewa sasa walichoitaji ni ubunifu wa
mavazi aina yoyote ile.sheria mpya ilitangazwa kwamba kila kundi lilihitaji
kutoa watu watatu watakaochuana vikali
iwapo kundi au makundi ya hao watu watafanya vibaya ndipo hao wenye kundi au
makundi watafungasha virago ili kurudi makwao.
Kundi la lazima tushinde
wakapewa kila kitu kilichohitajika kwenye ile shughuri pevu. Wao binafsi
walipenderea kushona aina tatu za mavazi, kwanza kabisa walitengeneza aina ya vazi la bakiti jeupe na kikoi chake
akavishwa bibie lerato. Pili wakashona vazi lipendwalo na mwanamke wa
Nigeria vazi lililo daliziwa kwa maua
maua pamoja na kiremba chake akavishwa mama silvano, na mwisho wakashona vazi
la kanga hili vazi walilipa jina la mama Africa
bibie andunje akavishwa akapendeza.kwa bahati nzuri wengi wa washiriki
kwenye kundi ili walikua na utaalamu wa kushona kwa kutumia cherehani.
Baada ya kumalizia shughuri
ile pevu likaitwa kundi la wakari classics.nao wakapewa walichotaka,hawakua na
makuu sana siku ile maana hofu ya kutokufanikiwa iliwatawala sana,ukitegemea
hakuna yeyote miongoni mwao aliyejua kushona kwa kutumia mashine ya cherehani ,lakini Mungu alivyo
mwema walipata wazo kwamba iliwapasa wasife mioyo yao,waoneshe uzarendo wao
hata kama mahari pale hakuna uzarendo, hivyo basi wakapata idea ya kushona kwa
kutumia sindano ya mkonono iliyojulikana kwa jina la sewing niddle.
vijana watatu wa kiume wakaitwa mbele yao
wakapimwa vizuri kila pande ya mwili wao, na baada ya kuridhika na ule upimaji
vitambaa vya aina mbalimbali vilikatwa,taratibu zingine zilienderea kufuatwa
kwa kutumia chalks,mikasi,uzi na sindano kulinganana na vipimo.
Kwanza kabisa walichukua ngozi ya kondoo na
kushona siglend na bahati nzuri ile ngozi ya sufu ilikua na manyoya mengi ,pili
waka shone short au kaptura yenye ngozi ya sufu, na tatu wakashona kofia ya
mkeka na kuweka ngozi ya sufu na wakamalizia kwa kushona viatu vya ngozi ya ngombe
kwa kuwekea ngozi ya kondoo vazi lile alivishwa Beni Toto.
Baada ya shughuri ile pevu
wakachukua kitambaa laini hicho wakakidarizi kwa kushona suti yenye rangi mbili
mbele nyeupe na upande wa nyuma nyeusi,pia wakatafuta kofia nyeupe iliyopambwa
ua jeusi akapewa Elia Abelia.
Baaada ya kazi ile matata
wakashona vazi moja matata lenye rangi
nyeupe lililosheheni manyoya ya sufu nyeupe sufu safi iliyotoka nchi ya Canada
bara la Australia,sufu ile ilisheheni manyoya pande zote tena vazi likawa refu
.walipoulizwa lile vazi ni maalumu kwa ajiri ya nini wao wakajibu ni maalumu
kwa ajiri ya kipindi cha baridi au kipindi cha barafu.chini ya lile vazi
walitupia kiatu kimoja kirefu cha ngozi ya ngombe kilikua ni kirefu kama magwanda ya jeshiniukitegemea kiatu kile
kilizidia urefu mpaka kufikia mapajani viatu vile ni viatu ambavyo utengenezwa
sana nchini Kenya akapewa Nairobi akavaa akawaka kwa kupendeza.na baada ya
shughuri ile nene walipomaliza wakapewa ishara ya kuondoka.
Likaitwa kundi la sisi ni
balaa na kundi la samba dumezi na simba jikezi maana safari hii yote kwa pamoja
yaliunganishwa kwa pamoja nao wakapewa nafasi ya kubuni chochote walichoona
kingewafaa kushonwa na kuwatoa vizuri kwenye mashindano yale.wakakaa chini ili
wafikirie kwa pamoja ni kitu gani bora cha kubuni…lakini hawakua na chochote
cha kufikiria,kwani miongoni mwao wapo waliopenda kubuni vazi la shetani
wengine vazi la malaika na wengine vazi lenye mfano wa nyumba,ilimradi kila
mshiriki alitaka abuni chake kitokacho moyoni. Lakini kiongozi wao neema
mwakyusa aliingia na wazo la kiubunifu waliitaji kubuni mavazi ya kwenye maumbo
ya siri ya binadamu.
Kwanza kabisa vijana wa
watatu wawili wa kike na mmoja wa kiume wakajongea mbele utadhania
jongoo anavyotembea wanawake wawili wakapimwa mmoja sindiria pamoja na chupi,ile
sindiria na chupi vikadaliziwa maua maua akapewa sister Abella.kijana wa kiume
akashonewa singlend pamoja na chupi nyeusi yenye mchanganyiko wa rangi nyeupe,
nyuma ya ile chupi likaandikwa neno DUME LA MBEGU.zikashonwa socks ndefu
nyeusi pamoja na kiatu kimoja cheupe
akapewa Johnson John
Baada ya kumalizia kazi ile
ngumu sasa likabaki kundi moja matata na machachari kundi la hamtuwezi nalo
likapewa ukurasa wa kuonesha vitu vyao vitu vikari vyenye ujuzi wa hali ya
juu,kwa bahati nzuri vijana wengi wa kundi ili walikua na uwezo wa kushona kwa
kutumia mikono na utaalamu wa kutumia mashine ya kushonea.
Wao binafsi walikubaliana
kushona nguo za utamaduni au nguo za kizazi kipya,lakini nguo za utamaduni
zilipewa nafsi kubwa sana,wakatwaa vitambaa vya kimaasai wakatwa pia ngozi ya
ngombe,mbuzi,chui na kondoo,hawakusahau pia vijiti,fimbo,magome na urembo wa
aina mbali mbali wa kiasili ulioambatana na shanga,herein,vipini vya puani,bangiri,
na vikuuku vya miguuni.
Hatua ya kwanza ambayo wao
waliifanya ilikua ni kuliviringisha vizuri lile vazi la kimaasai,kisha pamera
akapewa alivae lilikua na rangi ya blue iliyo nakishiwa kwa nakshi nakshi nyingi za urimbwende yaani
shanga nyingi kwenye lile vazi .shingo ya pamera ikapambwa vizuri kwa shanga
zenye umbo la duara.hawakuishia hapo wakachukua ngozi ya chui na ya kondoo
wakamtengenezea pamera viatu pamoja na kikapu cha ngozi ya chui iliyochanganywa
na ya kondoo pia wakamtengenezea pamera viatu na kikapu ndani ya kikapu
wakaweka nyama,achilia mbali kibuyu kikubwa chenye maziwa kilifungashwa vizuri.
Pomoni dia akatengenezewa nguo ya ajabu haswa kwani
msichana yule alivikwa nguo iliyotengenezwa kwa kutumia mifuko ya naironi au kama inavyoitwa RAMBO
akafungashiwa na kifuko cha sarufet pamoja na magazeti hakika alivutia mno hata
kiatu chake kilipambwa kwa kutumia gunia la kuwekea nafaka kama vile
mahindi,maharagwe,mtama,kunde alizeti na njegere akatengenezewa ungo
ulionakishiwa kwa kutumia gunia matunda mbali na mboga mboga nazo ziliwekwa
kwenye ule ungo, akatwikwa chungu cha asili pamoja na mwiko wa asili vilivyo nakshiwa shanga za asili ili kuleta
mvuto kwa watazamaji.
Boga talenter akapewa vazi zuri
la chui akapewa upinde mshale,mkuki pamoja na fimbo.juu ya kichwa chake
akavishwa taji tukufu la kifalume lenye rangi ya dhahabu,viatu vyake
vilitengenezwa kwa kutumia ngozi ya punda milia,achilia mbali kiti alichokalia
kilinakshiwa kwa kutumia ngozi ya simba
na baada ya kutengeneza kiti chake safarii hii ilitengenezwa nyumba
maalumu,nyumba yenye umbo la mbao lililomtosha yeye mwenyewe ikapigiliwa vizuri ikapambwa
maradufu kwa rangi za
nakshi,nakshi, chumba kilikua
ni kimoja tu pasipo choo pasipo sebule ila kiti kiti kimoja cha kifalme
kiliwekwa banda lilipendeza likavutia kwa rangi ya bendera ya Tanzania.Vijana
wanne yaani god listen,ndanda ngabi,Irene paul,na saba saba walifanya kazi ya
kulibeba lile jumba kwa kutumia mbao maalumu kazi ikaisha.
Baada ya ile kazi nene tena
inayo chosha,vijana wale wakapewa muda wa siku tatu mbele ili kupumzisha vichwa
na akili zao na baada ya hapo wangerejea tena ili kuonyesha ufundi na utaalamu
wao wa kiubunifu,ubunifu wa kimataifa.
SIKU YA FASHION SHOW
Baada ya pumziko la siku tatu
kwisha sasa nafasi ilioyo bakia ilikua ni nafasi ya kuonesha nini kipya cha
kujivunia kutoka kwenye nyuso za vijana machachari vijana wa pande za
sinza,temeke,kinondoni,manzese
kawe,ubungo,studio,mbagara,sinza,kimara,tabata,gongo la
mboto,kitunda,kinyerezi,magomeni mapipa,manzese midizini,mabibo tandika na
buguruni.na wengine wengi kutokea mikoani kama vile mbeya
iringa,taabora,Zanzibar,pemba,na unguja,rukwa,pwani,rufiji, na hata Arusha
achiria mbali kilimanjaro na tanga.
Siku ile ilibadirika kidogo
kwani tofauti na siku zingine ambazo msema chochote alikua mmoja sasa mwingine
aliongezeka, masanja mkandamizaji, Bamboo pia alikuwepo Bamboo alikua ni
mchekeshaji maharafu wa vichekesho vya the comedy katika kituo cha East Africa television
Kipindi hiki waandishi mbalimbali
wa vyombo vya habari kama vile televisheni,radio,magazett,website na blog
walikuwepo achilia mbali wabunifu mbali mbali wa mavazi nao walikuwepo kama
vile mbunifu hassan hasssano,mbunifu martini kadinda, mwanamitindo wa kimataifa
miriamu odemba. Na wengineo wengi walikuwepo kushuhudia kwa macho yao kwani
macho hayana pazia wala usitegemee kuambiwa njoo ushuhudie mwenyewe.
Watu walitulia wakijisikilizia muziki mwororo
kutoka kwa kijana machachari aliyekuja kwa kasi na kupachikwa jina la mwanamuziki DIAMOND
PLATTINUMZ wa kundi laWASAFI CLASSICSS aliwafanya watu wa injoy kwa wimbo wake
matata wa NUMBER ONE alio tengenezea video south Africa
Baada ya hadhira ile kukaa na
kungojea kwa muda ili kujua ni nini vijana watawavumbulia Mc massanja akishirikiana
na Mc bambo walifungua pazia ili kuyakaribisha makundi yale yaoneshe utundu
wao.kundi la wakari classics likapewa salute na heshima zote kwani safari ya
kwanza ya kupanda milima na kuvuka mabonde walifanya vema sasa walitegemewa
kuvumbua vitu vipya zaidi kwani waswahili wana kawaida ya kusema kipya kinyemi iweje
kikose kidonda,kipya utembezwa na kibaya utangazwa.
Kwa mada na mapozi akapita
kijana beni toto pale kwenye zuria
jekundu zuri refu utadhania bara bara ya rami,akawaonesha hadhira na waandishi
wa habari nini cha kujivunia,singlend short,na viatu vya sufu watu wakapiga
makofi na kumshangiria,Elia Abelia akakatiza kwa heshima zake zote utadhania
anaenda kwenye harusi tena harusi yake yeye mwenyewe,vigere gere na vifijo
vilimulika ukumbi ule kama vile taa ya group yenye mwanga mkari kama jua.hakika
alipendeza kwani baadhi ya wanawake uvumilivu uliwashinda wakaachia mabusu ya
midomoni mwao ……mwaaaaaaaa…….mwaaaaaaa…….kisssssss….kissssssss…..mwaaaaaa baby.
Safari hii Nairobi akaonesha
kitu chake kikari cha kimataifa we acha tu kijana aling’aa,aliogaaa,alitakataaa,alipakaa,alivutia
na kuacha midomo wazi kwa vazi lake refu lenye manyoya ya sufu,tena vazi la
kipindi cha joto na viatu vikari kama
meno ya simba, picha ziliwaka waaaaaa…..waaaaaaa……waaaaaaa…..kila upande
wenye blog wakaandika vyao na wenye website wakaandika vyao ili kupamba picha
za habari.
Mc bamboo akawang’ata sikio
ndugu watazamaji kuwa kundi lijalo ni kundi la pili maharufu la lazima tushinde
watu waka kaa chonjo kuwatazama ,lerato binti mrefu mweupe akajivuta pale
ukumbini kwa vazi lake la batiki nyeupe akifuatana na mama silivano kwa vazi
maharufu la kina igeria zito lililo gharimu mamilioni ya shilingi, na baada ya
mama silivano anduje naye akakatiza kwa kanga yake moja iliyoonesha maumbo yake
yote ukitegemea binti huyu kutokea mkoa wa tabora alijaliwa hips za moto,mguu
wa bia makalio yalonesa nessa hali iliyowapa wakati mgumu wanaume wakware
kwani kanga moja na miondoko
ile ilisababisha miti yao iliyo jaa utomvu isimame kwa hasira kwani mingine
ilianza kumwaga utomvu bila heshima na adabu lakini kwa bahati nzuri walikua
wameketi kwenye viti na pia kila mtu alikua bussy kutazama kilicho mleta hakuna
aliyejua la mwenzie maana jambo waso lijua litawasumbua.Kundi hili halikutia
fora kwani hata baadhi ya wanafiki waliinama chini chini na kuanza kupiga midomo
wakidai kuwa kundi limedorora, halina jipya
Mc masanja akalialika kundi
la sisi ni balaa pamoja na kundi la simba dumezi na simba jikez waje waoneshe
kipi ambacho wanajivunia mbele ya hadhira inayo watazama.
yallab!!!
Toba……astaghafrah!!!laana hii laahaulaaah!!!! Msalie mtume!!aibu gani hii
iliyoibua vicheko na kuvunja mbavu za watazamaji,wapo walioziba nyuso zao kwa
aibu ya mwaka wapo walicheka mpaka mbavu zao kupasuka,waandishi na watazamaji
pamoja na makamera men wao walimiminika kujichukuria habari iliyowacha midomo
wazi.
Si jingine bali ni yale
matukio ya kundi hili la nne na la tanokupita wakiwa wamepigilia vichupi,vimini,skafu
na vikoi,achilia mbali sindiria.
waandishi wambeya wa magazeti
ya udaku kama vile RISASI,UWAZI,IJUMAA,AMANI,na mengineyo mengi tu hawakua
nyuma kuandika walicho kinyaka.wasomi na wana falsafa wengi waliibua maswali
kuwa sasa mashindano talent show yanaelekea pabaya iweje midume mizima na
mijike mizima ioneshe uchi wao mbele za watoto,watoto wa taifa la kesho taifa
lililojaa maadili heshima na hekima taifa linalomcha Mungu na yesu kristo mwana
wake wa pekee leo hii wana buni sifa chafu jamaniii nyie jamani!!!!.
Wapo walio coment kwenye
magazet yao na dibate zao kuwa yale yalikua ni mashindano tu kwa maana hiyo
ubunifu na utaalamu ni kitu kilichopewa kipaumbele….therefore wenyechuki waache
chuki zao …chuki zao ni za bure tena
zina wasumbua.any way makundi haya mawili yalipongezwa na kuambiwa kwamba
yamefanya vizuri jambo la msingi ni ku keep it up wasonge mbele maisha ni
safari ndefu,maisha ni milima,maisha ni mabonde,maisha ni mito,maisha ni every thing.
Mc massanja pamoja na Mc bamboo,waliwataka
ndugu watazamaji wakae mkao wa kula na kunywa kwani tayari chakula kiliandikwa
mezani na wagawa chakula walikua wapo tayari kuwalisha na kuwanywesha
watazamaji vitamu tamu vinono nozi
hawakuwa wengine bali ni kundi la hamtuwezi.kwanza kabisa akapita bibie
pamera…….yelloooo!!!! kwa vazi lake la kimasai bibie aliita fora mno,bibie
alivyo mrefu kama twiga wa mbunga za ngorongoro akajipamba mavazi yenye shanga
akajiachia kwa urembo wa herein,kipini,mikufu ya kimaasai na bangiri za
kimaasai bibie alijipaka tope usoni na kila mtu alimsifia.
Dj choka alipomwona bibie
pamera anakata mbunga bila wasi wasi,akaweka wimbo wa msanii mmoja maharufu ila
kwa sasa hatunaye tena duniani si
mwingine bali ni ABEL LOSHIHIRARA MOTIKA
almaharufu kwa jina la MR EBBO na
wimbo wake wa mi mmaasai bwana…nasema mi mmaasai.
Pamera akaanza kucheza kama
vile wanawake wa asili ya kimaasai.pomoni dia binti yule naye akafuatia akiwa amejikwatua na kujipamba swaafii
sana kwa mavazi yake ya karatasi kila
mtu aliye mwona alibaki kupigwa na butwaa
na bumbuwazi kwani hawakuamini kama kweli magazeti yana weza kushonwa na
kuwa vazi zuri lenye mvuto wa aina ile hadhira ilifuraia sana kwani vijana
walionesha hali ya kujituma zaidi kwani kutokana na jinsi pomoni alivyopendeza
hakukosa mchumba pale pale.
Docta bingwa wa matibabu ya
moyo katika hospitary ya muhimbili alivutiwa sana na ulimbwende wa pomoni
dia,docta Erick akainuka na kwenda kumtunza manoti mekundu mekundu kibao,
mapedeshee nao hawakua nyuma kwani walipoona
docta Erick anafanya yake nao wakajitoma zaidi kumwagia manoti bibie pomoni dia.
ilipofika zamu ya boga
talenter kila mtu alibakia na maswali mchanganyiko kwani hawakuelewa ni nini
kilichokuwemo ndani ya ile nyumba,wapo waliodhani ni maiti ,wapo waliodhani ni
gaidi,wapo waloidhani ni ni nyumba tu iliyo buniwa wala hakuna chochote……..lakini ukweli ni
kwamba uzaniacho ndio kumbe sio na jambo uso lijua ni kama usiku wa kizaa.
Mlango ulipofunguliwa vijana
waliombeba boga talenter wakapiga saluti ya heshima kwa mfalme na pia hadhira
nayoikafanya ishara yakupiga magoti kama vile waumini wa dini ya kiislamu
wafanyavyo wakiwa kwenye ibada zao ilikua ni ishara ya heshima na taadhima kwa
mfalme aliyebebwa kwenye kiti chake kitakatifu.
Hakika ukumbi ulijawa na
furaha siku ile boga aliwavutia kila mtu si wana michezo si wana siasa si wana
falsafa,siwatu wa kimataifa aliwavutia kila mtu ukitegemea duniia nzima ilikua
ikiwaangalia wanavyofanya maajabu yao kupitia vyombo vya habari kama vile
television ya TBC,ITV,STAAR TV,CHANNEL TEN,SIBUKA TV NA CITZEN TV na zinginezo
nyingi.
Hadhira ilishangiria na
kupiga makofi na baada ya kuondoka ile fulsa hadimu iliyo tazamiwa na
wengi na iliyotegemewa na wengi
kuangalia product mbali mbali zilizotengenezwa na vijana wale wengi wlizinunua
na wengine wakatoa oda ya kutengenezewa na kulipia baada ya kazi kukamilika .
Lakini kabla ya matokeo
kutajwa ya nani kashindwa na nani kashindwa Mc masanja nja Mc bamboo waliwataka
ndugu watazamaji na ndugu wasikilizaji kutoa michango ya harambe ya kuwasaidia
watoto yatima na wajane pamoja na wakina
mama wenye ugonjwa wa kansa ya matiti,pesa nyingi zilichangishwa karibia
milioni ishirini ukitegemea ziliitajika million sita tu.Hakika kutoa ni moyo na
usambe ni utajiri kwani damu ni nzito kuliko maji.
Baadaya ya kuchangisha pesa zile
Mc masanja pamoja na Mc bamboo
waliwashukuru ndugu wageni ,majaji pamoja na washiriki, kwa moyo mzuri
walijotolea na kwa ushirikiano bora walioufanya.lakini pia Mc bamboo aliwatangazia watu wote mahari pale
kwamba kuna mtu amepoteza funguo zake za gari,gari aina ya prado gari la
kifahari zaidi akamtaka mtu yeyote aliyeiona funguo iyo arudishe mapema.kwani
lile gari lilikua ni gari la kigogo fulani wa serkiali ya jakaya mrisho
kikwete.lakini hakuna aliyejitokeza.
Baada ya nusu saa kupita
majaji wakakaa mezani ili kutoa majibu ya mashindano yale.ukweli ni kwamba
majaji walipendezwa sana na kazi ya makundi yote ,kwani ilikua ni kazi ngumu
sana ,waliwapongeza sana na pia hawakuacha kuwakosoa pale ambapo waliona kuwa
washiriki wamekosea. Au washiriki wanaitaji kurekebisha makosa au kutofanya
makosa kabisa katika mashindano yajayo.
Ikafikia kipindi cha
kutangaza washindi wa mashindano yale ya mavazi jaji salama jabiri,akalitangaza
kundi la hamtuwezi kuwa ndilo kundi bora na lililofanya vizuri katika
mashindano yale ya fashion show,furaha zililipuka sangwe na nderemo
vilimiminika utadhania maji ya mto Nile mto usiokauka milele katika jangwa la
sahara.
Muheshimiwa waziri mulungu
akasimama na kuwapamba maua kundi la wakari classics,kuwa ni kundi bora na la
pili katika mashindano yale,vigeregere vilivyo ambatana na muziki wenye beat
kari vilisikika mahari pale,ngoma na midundo ya aina mbali mbali vilitawala
eneo lile.
Maadam ritta paulsean akawapa
hai kundi la tatu la lazima tushinde kuwa ndilo kundi bora machachari nalo
lilishika nafasi ya tatu kuibuka katika kinyanganyioro kile.jaji na producer
maharufu bongo master jay naye akawatangazia ndugu watazamaji kuwa kundi la sisi
ni balaa pamoja na kundi la simba dumez na simba jikez yalikamata nafsi ya nne
ila aliyataka kuji keep bussy maana hawakufanya vizuri sana watu wakawapigia
vigeregere makofi na nderemo.
Sasa ikawa ni zamu ya nani
atoke nani abakie kuenderea na michuano ile,kila mtu aliye kaa upande wa
hadhira alijisemea moyoni kuwa kundi la nne ni lazima wafungashe virago vyao
kwani walionekana kuwa si lolote si chochote kwenye yale mashindano kazi gani
kuonesha vichupi na miili yao ya heshima watu wazima hovyo….vya wazungu wa
waachie wazungu na vya wa Africa viachwe Africa.jaji joyce kiria akapewa nafsi
ya kutangaza kundi lipi linastahiri kutoka na kundi lipi au yapi yana stahiri
kuenderea kudunda.
Maadam joyce kiria akasimama
mahari pale naye akayapongeza makundi yote wala hakusita kuyakosoa pale
yalipostahiri kukosolewa,lakini mwisho maadam kiria akatangaza kuwa
halitakuwepo kundi lolote la kutoka kwani yote yame perform better ushindani
ulikua ni mzito na pia ni wenye tija hivyo basi makundi yote yajiandae vema kwa
mashindano mapya yajayo.
ooooosh……my god!!!ndivyo
sauti za washiriki zilisikika kumshukuru Mungu kwa kuwa nusuru kuingia kwenye
kikapu cha takataka.
Makofi nderemo na vigere gere
vilitawala eneo lile,mc masanja akawataka washiriki wote wajumuike kucheza
muzik na kisha baada ya hapo ukumbi ule ungefungwa wakatangaziwa kuwa watakua
na pumziko la juma moja na baada ya pumziko ilo walitakiwa kurejea tena kwenye
mashindano.
mwanamuziki machachari wa
muziki wa kizazi kipya bongo naasibu
abdul au diamond platinumz akapewa
nafasi ya kutumbuiza singo yake machachari
tamu masikion mwa hadhira iliyo kwenda kwa jina la NIMPENDE NANI.kila mara hadhira waliposikia
neno nimpende nani, wote kwa pamoja
wakajibu neno ……woteeee…..
Ukumbi ule ukafungwa na watu
wakatawanyika kurudi majumbani kwao maana ilikua ni mida ya saa sita usiku.
yule kigogo wa serkiali alibaki
amechanganyikiwa asijue nini cha kufanya ili aliondoe gari lake maana ufunguo
ulipotea na hakujua ni wapi ataipata.alichanganyikiwa…akawa anatembea tembea
hapa na pale….masikini kigogo alijiuliza maswali kibao yaso na majibu.
Oh my god who stole my car key?........imeenda
wapi?.......nani kachukua ?.......nitamwambiaje mama watoto kuwa fungua ya gari
zuri kama lile la kifahari imepotea?……..aaaash!!!!..... kadri alivyozidi
kutembea ndivyo akawa anahisi kama kuna maumivu kidogo kwenye mguu wake wa
kushoto,haraka haraka akavua kiatu ili kuangalia ni nini klinacho muumiza,Mungu
wangu wee!!kumbe ni ufunguo,ufunguo wa gari yake mwenyewe furahaa ilimjia chozi
lilimbubujika chozi la furahaa chozi la kuuraani uzembe na usahaulifu ulo
mkabiri.
Taratibu akaenda kwenye gari
lake na kuliwasha kisha akalitoa moto likapaa kama ndege ya BRITSHI AIR WAYZ.
Tatizo la yule kigogo wa
serkiali alikua na tabia ya kusahau sahauvitu mara kwa mara,hata akiwa bungeni
muda mwingi alikua akiuchapa usingizi mate yalimtoka mdomoni utadhania mboga mboga ya mrenda yalimsaidia sana
kuchafua karatasi zake za hotuba hata alipoulizwa maswali kwani alijibu?
hapana alienderea na usingizi
wake mnono kama samaki aliye shiba.
Hakukumbuka kwamba ni mambo yake
ya kitoto yaliyomfanya aiweke funguo kwenye kiatu chake,hata hivyo kigogo yule
siku ile alisahau kurudi Nyumbani kwake akajikuta anapita njia ya ohio huko
nako akakumbana na wanawake wenye tabia ya kujiuza.