Monday, October 31, 2011

'' ..........HIVI KWANINI MUZIKI NI KITU CHA GHARAMA...........??????!!!!!!! ''

UNAWEZA SEMA MIZIKI NI KAZI, MUZIKI NI KIPAWA, MUZIKI NI MAJARIWA, NI UWEZO WA KUIMBA UKIAMBATANA NA KUCHEZA,SAUTI TAMU YA KUMTOA NYOKA PANGONI [YA MVUTO WA ALA NA VIONJO MBALIMBALI ] YOTE HAYO MIMI SIKATAI ILA MADA YA LEO NI ....KWANINI MUZIKI NI GHARAMA


  MOSI....UNAPOANZA MUZIKI HASA HUU WA KIDUNIA  MAALUMU KAMA BONGO FLEVA JARIBU KUFIKIRIA KUWA LAZIMA UWE NA MTAJI[CAPITAL] MAANA HATA KWENDA STUDIO[UNDER GROUND ,PROFFESIAL,AND TALENTIVE STUDIO]INAHITAJI PESA ANY WAY INAWEZA IKAWA STUDIO YA NDUGU YAKO[KAKA AU DADA]YA RAFIKI JIRAN AU YEYOTE YULE LAKINI YOTE CHIN JARIBU KUFIKIRIA UMUHIMU WA KUWA NA MTAJI.


PILI .....MUZIKI SIO MCHEZO WA KITOTO ,MUZIKI SIO KAZI YA KIUPUMBAVU..HII NI KAZI NGUMU HASA  LAKINI YOTE CHINI JUU POLE POLE NDIO MWENDO.. MWENYEWE UTAFURAHIA TARATIBU NA UTAPENDA MAFANIKIO YA KAZI HIYO UNAYO IFANYA.TAMBUA KUWA KIPAJI HIKI KINAHITAJI PESA  ZA KUTOSHA  KUKUTOA WEWE NA KUKUFANYA UWE JUU...JARIBU KUFUATILIA MAMBO YAKO KWENYE VYOMBO VYA HABARI HASA RADIO,[UKIPELEKA CD ZAKO]KWENYE TV NA COMPUTER HAS UKIPELEKA PICHA ZAKO KOTE HUKO ITAKUGHARIMU TU ILA USIFE MOYO.....MFANO RADIO ZINGINE ZINATAKA PESA KIDOGO KUKUWEKA TOP FULANI WANATAKA POSHO .TV NA COMPUTER NAKO NI GHARAMA KUUZAA WIMBO WAKO INTERNET NAKO YATAKA PESA HIVYO JIANDAE KIPESA .....

     WAPO WALIOBAHATIKA KUPATA WAFADHILI, MPAKA WAKAWA JUU KIMUZIKIWAFADHILI NI MUHIMU SANAMAANA WATASIMAMIA KAZI ZAKO MPAKA UNAFANIKIWA KAMA WEWE NI MSAANIMCHANGA  NA HAUNA CAPITAR  NA UKAPATA WAFADHILI TAFADHARI USIWAZARAU YAKUPASA SASA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU

         WAPENZI KWA LEO SINA MENGI YA KUWANONGONEZA NAONA MUDA WANGU NI MCHACHE SANA ....ILA NIKIPATA WAZO LOLOTE  NAAIDI KUWA SINTA WAANGUSHA.................
                            WASSALAAMU.......

.................. JE KIPAJI PEKEE NI MUZIKI ......?????????

 KAMA NIJUAVYO MUZIKI KWA KIFUPI  NI UIMBAJI UNAOENDANA  NA ALA YAANI NYIMBO ZINAZOENDANA NA VIFAAA INSTRUMENT AU ZANA MBALIMBALI ZINAZOUFANYA MUZIKI UWE MTAMU WENYE VIONJO.
       VIFAAA AU DHANA ZINAZOLETA VIONJO NI KAMA MAGITAA ,VINANDA ,NGOMA,SAXAPHONE NA VINGINEVYOVINGI TU MBALI NA  HAPO MUZIKI UNAMUHITAJI MTU YAANI MUIMBAJI MWENYE SAUTI ISIYOTETEREKA [YAWEZAKUWA YA 1,2,3,4,.........5,6.7.8.9.........IRIMRADI IWE NA MVUTO KWA WASIKILIZAJI.]
       TURUDI KWENYE SWALI LETU HAPO JUU... SIKWELI KUSEMA KUWA MUZIKI PEKEE NI KIPAJI VIPAJI VIPO VINGI SANA MBALI NA UIMBAJI KUNA  UCHORAJI,UCHEKESHAJI,[MAIGIZO] UPISHI,UKURIMA,BIASHARA,UVUVI,NA KADHARIKA, VYOTEHIVYO NI VIPAJI TULIVYOJARIWA  NA MWENYEZI MUNGU.
       MUZIKI NI KIPENGERE KIMOJAWAPO CHA SANAA PIA NI KAZI YENYE UMUHIMU SANA  MAANA INA LENGO LA KUELIMISHA ,KUBURUDISHA,KUSISIMUA, KUKOSOA,NA KUKUZA LUGHA,MBALI NA HAPO NI KAZI YENYE KUITAJI SAUTI PAMOJA NA MIRINDIMO MBALIMBALI....INA FAIDA SANA KWA SABABUNI KAZIINAYOLETA KIPATO KWA MSAANI NI KAZI YENYE THAMANI SANA INAYO MFANYA MUHUSIKA  AKAJULIKANA,AKAHESHIMIKA,  NAKUPENDWAKATIKA JAMII...
     ..........  HIVYO SISI WATANZANIA TUMEJARIWA VIPAJI VINGI SANA  SIO TU MUZIKI PEKEE NA TUVITUMIE KWA MANUFAA YETU SOTE NA TAIFA LETU.............

Friday, October 28, 2011

NAMWAGA TANOKWA WASHIKAJI WANGU MWANA FA ...NA MEMBER WENGINE KAMA TID [TOP IN DAR]KALA PINA NA KEISHA ...BIG UP MA MEN MUME DONE GOOD JOB..........

 Mwana fa msaani wakizazi kipya na wenzake keisha wanaaounda umoja uliochini ya mwamvuli uitwao Tanzania fleva unit [tfu]walipiga hatua kubwa dhiidi ya mapambano ya maharamia  wa kazi zao baada ya kule kulalamika kwao kusikokuwa na hukomo juu ya madai ya dhuruma dhiidi ya jasho lao  hatimae safari hii wameibuka kivingine wametoa mapendekezo kadhaa wa kadhaa wanayo amini kuwa yakiungwa mikono  na mamlaka inayo husika tatizo la uharamia litapungua sana nchini..
          kama mapendekezo yao yatazingatiwa serikali itavuna fedhab nyingi kupitia kodi itakayo kusanywa katika mauzo ya kazi zao,kinyume na hali iliyopo sasa a mbapo mauzo ya kazinyingiza wasaaninchini hayainufaaishi serikali kwasababu ni feki na wauzaji wake sio rasimi
          NIWAZO LIPI
     Wamepania kupeleka mapendekezo ya kuitaka serikali iwasilishe  mswaada bungeni utakao walazimisha wafanya biashara kuuza cd ,vcd ,dvd na kazi nyingine za kisaani ambazo zina nembo maalumu  ya tra [mamlaka ya mapato tanzania] .kupitia mpango huo mwana faa na wenzake wanaamini kuwa walaji wa kazi zao za kisaani watapata nafasi ya kutambua kirahisi kazi halisi zitakazo kuwa na nembo ya TRA dhiidi ya feki ambazo hazitakuwa na nembo hiyo..pia polisi na vyombo vingine vya vya kusimamia utekelezajiwa sheria halali za nchi watapata unaafuu wa kuwanasa wauzaji wa kazi feki na kuwapeleka mbele ya mkono wa sheria
                faida nyingine aliyoitaja mwana fa,kuwa jambo hili litaongezea taifa mapato kwani bada ya hapo hawatakuwa wakiibiwa sana kama zamani faida zitapatikana ikiwaserikali itatekeleza mapendekezo yao bila shaka kupitiawizara za viwanda  na biashara na habari utamaduni ,vijana na michezo....binafs ninawapongeza wakina mwana fa na pia kuwaunga mkono katika kubuni utaratibu mzuri  kama huo sasa ni kipindi cha mamlaka husika kushirikiana na TRA katika kubuni utaratibu mzuri wa kutekeleza haraka mapendekezo yaliyoenda shule  ya mwana fa na wenzake tena bila kusubiri ya pelekwe kwenye mamlaka  ofisini
    
        Wanaoshikilia dhamaana walizopewa na taifa  ktk kushughurikia haki za wasaani wawe wa kwanza kuwaita wakina mwana fa na kusikiliza hoja zao kuanzia AtoZ hawana sabab za kuchelewa kwani kila walichozungumza kuhusu uharamia kina fahamika  mifano ni mingi na tena ipo wazi sana  ....mwanzoni mwa mwaka jana maofisa wa chama cha haki miliki tanzania[cosota]kwakushirikiana na wenzao kutoka chama cha waandaaji filamu tz walitekeleza cd bandia5,200na mikanda bandia ya video 2,600
                         
   Wahusika wa wizi wa kazi hizo wananufaika na wasaani wanaishia kufa njaa na kubaki na umaharufu mkubwa wa majina yao ..kama TRA itatumika   serikali itaingiza mapato makubwa na wakati huo huo wasaani watanufaika kwa sababu kila kitu kitakuwa rasim sio kama ilivyo hivi sasa ...kama ungelipia kodi ya ongezeko la dhamani[VAT].  maaana mzigo huo mmoja uliowai kukamatwa  na kosota na watu wa filamu  ungeingiza serikali asilimia 18% ya thamani ya shilingi milion 5.94
                  Huo ni mfano wa namna ambavyo serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kutokana na kodi isiyokusanywak kupitia mauzo ya kazi za wasaani zinazorudufiwa kinyume cha sheria ..sasa cosota iunge mkono wazo la akina mwana fa na kulipigia chapuo serikalini ili atimaye kupunguza uharamia wa kazi za wasaani kwa kufanya hivyo

''MUZIKI WA ASILI USISAHAAULIWE NI UTAMADUNI WETU''

Muziki  ni ala .....lakini kwa kamusi sanifu ya kiswahili muziki umeelezwa kama mpangilio wa ala na uimbaji unaoleta adhari fulani kwa kiumbe hii ina maana kwamba kama msaani wa muziki hapangilii ala zake na kuimba kwa ustadi basi anachofanya msaani huyo sio muziki bali ni kelele za kawaida tu.
   Muziki ni saana kama zilivyo sanaa nyingine hivyo hatuna budi kujua sanaa ninini ?hasa sanaa imeelezwa kama ufundi,ufundi wa kuwakilisha mawazo yaliyomo katika fikla za binadamu ili ya dhiirike na kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa walengwa
    Hivyo sanaa inakubali kuwa na malengomakuu ambayo ni

                  1.KUELIMISHA JAMII
                  2. KUBURUDISHA
                  3, NA HATA KUELEKEZA JAMII
         Sanaa pia ni utambulisho wa jamii husika hata kama haujawai kuishi na jamii hiyo....itakuwa kosa kubwa kama tutaisahau sekta hii ya muziki katika jamii yetu
                Muziki una historia ndefu sana tena isiyo yumba katika ustawi wa jamiiya binadamu.muziki pia umezisambaratisha ndoa na familia nyingi,muziki umewatoa watu machozi ya furaha na huzuni...Wanasayansi bado wana kesha  katika maabara kubwa duniani kutafiti ni kwa nini muziki una adhari kubwa katik ubongo wa binadamu......muziki umetumiwa kama dawa kwa wagonjwa wa wa akili na walio na msongo wa mawazo, lakini kuna mkanganyiko mkubwa baini ya muziki wa asili na na ule wenye vionjo vya usasa

            Basi nini tofauti kati ya muziki wa asili na ule uliochanganyika na usasa
       Muziki huu wenye vionjo vyaasili ni ule wenye usasa lakini una vionjo vya asili.....unaposimama na kuzungumzia muziki wa asili basi ni vema ukatafakari kwa makini ni muziki upi ambao unachukua jukumu la kutambulisha utamaduni na asili ya mtanzania ...mara nyingi wasaani wa muziki wa asili wamekuwa wakifanya  kazi  zao nchi za nje wakiutangaza utamaduni wetu tofauti na hapa nyumbani.Hili limekwisha kuwa tatizo la watanzania wenyewe  kushindwa kuuenzi muziki huu hivyo wasaani wengi wamejikuta wakifuta muziki huo ambao unatukuzwa na mataifa mengine ya huko nje..
  Hii huenda kuwa ndiyo sababu iliyowafanya hata waandaaji wa tuzo hapa nchini kutozingatia makundi halisi ya muziki wa asili wa asili kushirikishwa katika tuzo hizo.hata hivyo serikali ina dhamaaana ya kuendereza muziki wetu  kwa kuzingatia kutoa vipaumbele  kwa makundi ya saana ya muziki  wa asili ili kuweza kuuenzi sisi wenyewe ni aibu kubwa ikiwa sisi watanzania wenyewe hatufahamu vema muziki wa asili  na hii ni sababu tunashindwa kuhuuenzi utamaduni wetu , ni vigumu kujuwa iwapo hatuuenzi .serikali ina wajibu wa kujenga ukumbi wa kisasa kwa shughuri za sanaa  na kusimamia mikataba halali  kwa wasani ili kuweza kutoa kipaumbele  hivyo na pia  kutatua matatizo kadha ambayo yamekuwa yakiwakumba wasaani hao
        
            Pia vyombo vingi vya habari havitoi kipaumbele kwa sanaa na wasaani wa muziki wa asili hili ni tatizo pia kwani linafifisha utamaduni wetu na hata wadau mbalimbali wanashindwa kutambua vema muziki wa asili kuna haja ya kuanzisha tovuti mbali mbali ambazo zitakuwa zikitoa taharifa mbali mbali  kuhusu muziki huu na hata vipindi mbali mbali maaalumu katika television na radio mbali nchini.... kwani kuna makundi mengi na wasaani wengi wa asili kama vile saida kaloli,jhikoman, mbeya arts, na baadhi ya wasaani wanaotambulika kuwa ni waimbaji nyimbo za asili

               kuna haja kwa watanzania kubadilika ili tuupende,tuuenzi na kuheshimu vya kwetu kwani mwenda kwao si mtoro/mtumwa.....mcheza kwao hutunzwa.hipo siku tutavipoteza kabisa vya kwetu nakuwa watumwa wa mataifa mengine.......
                              
                               ASANTENI  SANA NA KWAHERI

                  .....................................................................
                     $$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$$
                         %%%%%%%%%%%%%%%%%%
                            **************************
                               ^^^^^&&&&&&&&&&!!!!!!!!