MWANAUME UYAKAVA
MADHAIFU YA MWANAUME MWENZAKE
Katika suala
la mapenzi wanaume wengi sana wana madhaifu kwa mfano,kushindwa
kumjali,kuympenda kumthamini,na kumheshimu mwanamke aliye naye,sio tu hivyo
hata katika suala la nguvu za kiume,wapo wenye nguvu nyingi na wengine
madhaifu,wapo walio teke teke na pia wapo wasiojua kitu yaani ziro power ziro
percentage.
Sasa Elaija
Wanaume
wengi hudanganya mambo mengi tu lakini hawapo tayari kukuambia kuuhusu kipimo
au ujazo wa nguvu zao,wengi hujigamba kwamba wao ni strong powerfull na wenye
nguvu,hivyo mwanamke hukimbilia popote ili kupima madhaifu ya mwanaume na
mwanaume mwenzie
Elaija
Usikubali
jambo kama hilo likutokee maishani mwako,
Be strong
,jiamini,take care be always care fully and love you
MAGELIA
Elaija
NIMEKUA NA
RAFIKI YANGU WA KIKE KWA MUDA WA MIAKA MITATU
LAKINI
HATUJAPATA KUONANA SANA SANA TU,
HATUJAPATA
KULALA PAMOJA,
HATUJAPATA
KULA AU KWENDA AU KUNUNUA VITU KWA PAMOJA,KWA UPANDE WANGU NIMEKUA DHAIFU SANA
KWENYE MAPENZI, MAGELIA AMEKUA MKARI SANA KWANGU, AMEKUA NA HASIRA SANA KWANGU, HATA SIKU MOJA
ALITOROKA KWENDA MORO GORO, yote ni kwa sababu ya mapenzi
SASA
AMENINUNIA ANADAI TUACHANE ANADAI PENZI LANGU NI UPEPO,NA ANAHITAJI UHURU
WAKE,ANAHITAJI KUA NA MWANAUME WA KUMLIWAZA.NIMEYAONA MADHAIFU YANGU LAKINI PIA
SITAKI KUMRUHUSU ANIACHE
NAMPENDA
SANA MAGELIA,JAPOKUA NIMEKUA DHAIFU SANA,NIME MWAHIDI VITU VINGI SANA, SASA
AMECHOKA ANAHITAJI UHURU WAKE,JAPOKUA ALIKUA ANA UPENDO MWINGI KWANGU LAKINI
HILI NALO LINANITIA WASI WASI NAHUMIA SANA IWAPO ATANIACHA NAMPENDA SANA
MAGELIA
ASILIMIA
KUBWA YA WATU WANAOTIZAMA MPIRA NI
WANAUME
Elaija
Mchezo wa
mpira ni mcezo unaopendwa sana katika mataifa mengi sana duniani,ni mchezo
unaovuta maelfu ya watu kwenda kuutizama na pia wana furahi kuona pande mbili
zinagombana.ili ziweze kupata ushindi.
Elaija.
Siku moja
nilienda kutizama mashindano ya mpira kati ya mbeya fc na timu Fulani ngeni
kama sikosei iliitwa mtibwa sugar,nilipoingia kwenye ukumbi wa sokoine niliona
kundi kubwa la wanaume wanafurahia mpira …..lakini nilipotizama pande zingine
niliona wanaume wachache sana kwa kiasi kikubwa nilijisemea moyoni mwangu
,,mpira ni mchezo unao wavutia
vijana wengi wa kiume,,
DUU!!!!
ULEVI NOOOOMA.
Ulevi ni
kitendo cha kunywa kiasi Fulani cha
pombe,unaweza kunywa kwa kiasi Fulani au kuzidisha mpaka ubongo ukakosa
ufahamu.
Lakini
Elaija
Matokeo ya
ulevi huo ni kushindwa kuinuka kimaendereo,au kuzorota akili na kushindwa
kufanya kazi ipasavyo matokeo yake wahusika
au mhusika uwa tegemezi.
Elaija
Pombe ina
gharama zake,pombe inaweza kukufanya ushindwe kueleweka,katika jamii inayo
kuzunguka,tazama ulevi ni kitendo cha kutumia madawa ya kulevya na madhara yake
ni kifo au kupata ajari au hata ugonjwa wa kansa.
Acha ulevi
jenga nchi leta maendereo
MAISHA YETU
NI KUFANYA KAZI
Kazi ndio
maisha yetu yanahitaji mtu awajibike kisawa sawa,usiku na mchana vijana wana
waza kazi,umasikini unatutawala kwa vile hatuna kazi na pia njaa inatunyanyasa
eti kwa sababu tu hatuna kazi..kazi ni kituy bora sana katika maisha yetu kitu
kinachoweza kutufanya sisi tukajenga maisha.
Any way
nawatizama vijana wanavyo chakarika mikono yao au miguu yao,migongo yao ina
wahuma lakini pia wanajitahidi tu kuwajibika,wanajitahidi tu kuteseka,japo
kupata ridhiki yao maisha ni ni magumu.
Vijana hao
ni wazuri sana hakika wana nivutia maumbo yao,maumbo yao yamejengeka kwa sababu
ya kufanya kazi wana hangaika siku zote ili wapate kufanikiwa.hakika kazi ndio
msingi wa kujenga nchi,
Nchi
masikini haiwezi kuenderea kwa kutegemea misahada ya mataifa mengine au
wafadhiri pasipo kufanya kazi
AMEKWISHA
ONA SASA NI KUMWACHA TU
Binti sasa
amekua,matiti yamechomoza yamekua mazito hakika yana mvuto, wowowo lake sio
dogo,yaani ni kabichi au tikiti maji,mh!!linaenderea kunesa nesa ana tabasamu
zito na mikono yake na mapaja yake pia ni mazito..
ELAIJA,
nikwambie kaka yangu
Sasa
ameshapendwa mmh!!! Mmh!! Jamani au amesha kulionja tunda? Mmh ndivyo sukari
ilivyo utamu wake ni kuonja kidogo kidogo…..ah ah ah no ..utamu wake ni kuweka kwenye chai.
Elaija
umeona eeeh!!!
Ameshakuonja
na anatoroka nyumbani kwao mmh!! Analala mbali na nyumbani kwao mmh amekatazwa
lakini mbona hasikii?
Some time am ekua ni mtumwa wa mapenzi,kwa sasa ni
mjamzito eeeh!! Amezaa lakini bado anaenderea tu na tabia yake ya kupenda penda
eti kwanini jamani? Au ndio mahitaji ya kimwili yalivyo
Mmmh!!!
Ameona na sasa ni kumwacha tu.
Elaija mbona una
ona aibu
Elaija inakuaje mbona unapotembea waogopa!!mmh!! kwanini elaija
Woga
utakumaliza,woga utkuponza na woga hautakupeleka mbali,woga na aibu ni vitu
viwili visivyo na tofauti,
Sasa Elaija
Jitahidi
kuukwepa woga,utupilie mbali woga,uambie woga kaa mbali na mimi hauna nafasi
hata kidogo kwenye mwili wangu..
Elaija
Hatuna muda
mwingi sana wa kuishi duniani,miaka tuliyonayo ni michache,sana na pia
tumebahatika nafasi tu ya kuliona jua mwezi na nyota nyota pamoja na vyote
menyezi mungu ametupatia.
Elaija
jifunze vyote ili viweze kukusaidia maishani.wala usiwe na woga Elaija jitahidi
tu kupitia hata kama ni vigumu.
Love you
Elaija
NATAMANI NINGE KUA
MUNGU
Elaija
Dunia
imeumbwa kwa ufundi,utaalamu,ujuzi na kipaji cha hali ya juu zaidi,ambapo
hakuna awezaye kufanya mambo mazito kama
yale ayafanyayo mwenyez mungu.
Elaija
Popote
utakapopita chochote utakachoona au lolote utakalo sikia,jiulize hivi hizo
nguvu zimetoka wapi,Elaija just remember mungu alipo kamilisha kila kitu kiwepo
duniani ndipo akamleta binadamu aweze kua ni mtawala wa hiyo dunia.
Elaija
nikwambie
Na mimi
natamani sana ningekua mungu mkuu mwenye nguvu zote,japo niweze kuitengeneza
dunia na vyote vilivyomo,natamani sana tenasana kumuumba binadamu natamani
zaidi lakini udhaifu wangu ni kua sina hizo nguvu
Any way
najisemea moyoni mwangu upendo wa mungu unifunike ili niweze kutendaz yale yote
makuu ayatakayo mwenyezi mungu niyatende……….
Nahitaji
kubadirika
Nimeyapima sana mawazo yangu,nimeyapima
sana nimeyapima kwa muda
mrefu,nimeyapima kuanzia mwanzo mpaka hatua ya mwisho na hatimaye nikaja
kugundua,udhaifu na upungufu wangu katika suala zima la kufikiria namna gani
naweza kupambanua ili niweze kuchochea na kuyaleta maendereo.
Na jawabu nililolipata ni kua nina haja ya
kubadirika,nibadiriken ili niweze kujivunia maendereo na maendereo yenyewe
inanipasa niyatafute kwa majasho makubwa na makari mno,ndoto zangu hazitakuja
kutimia iwapo nitashindwa kutimiza mipango na matarajio na hapa nimeona mbali
sana ya kwamba iwapo nitafanya uzembe
nitashindwa kutimiza yale yote niyatarajiayo.
Kila siku nimekua nikilalamikiwa ya
kwamba sina maendereo au sitakuja kua na maendereo ya haraka,heshima yangu imeshuka ana kupungua kwa kiasi kikubwa
sana,nimekua ziro kwenye kila idarasina biashara sina mtaj wala sina maana
yoyote ile.
Na sasa nahitaji kubadirika nahitaji
kutafuta pesa au mkopo nijikwakwamue,
Ili na mimi japo niipate nahafuu ya
maendereo.
Imekufa lakini inaishi hai
Ndio kwa mtazamo wangu nahualisia wamaisha yao wao ni watu pia wako
hai na uhai wao ni ule uhai unaotokana na tamaa zao za kuvipata vile vyote
vyenye anasa na tamaa za kidunia
Kwa mfano walipokua hai wanaishi duniani walitamani sana kua na
nyumba nzuri ,magari mazuri ya kifahari,pesa nyingi,wanawake pamoja na watoto
wengi tena wazuri,tama yao ilikuwa kubwa na nzito sana lakini ubaya wake hawakuvipata
vyote hivyo walivyovitamani,sikatai nikikwambia ya kwamba kuna baadhi ya
vilivotamaniwa walivipata lakini ukweli wa mambo unasema kwamba hawakuchuma
vingi.Hapo ndipo walipoweka fikra zao mbele kwa mbele,wazee hawa wakaapa kuwa
wakifa tu ni lazima wawe nusu hai nusu wa wafu nani lazima mali,utajiri,fahari
na vyote wavitakavyo watavipata tu
Wachambuzi wa mambo haya wameshasema kinagaubaga kuwa hawa
waliokufa sasa wanafurahia maisha yao huko
kuzimu,kwani wanazo nguvvu za kutosha kumteka binadamu kimawazo kifikra,kiuchumi,kisiasa na
kiutamaduni,
Ndio wameweza,wanawatumia waganga wa kienyeji ,wanatumia
watu,wanyama na wadudu ili kutimiza dhima zao wameungana na
majini,mapepo au mizimu ili kutimiza adhima yao kwa mfano iwapo wewe unashida
shida yako ni ugonjwa utakao gharimu laki mbili uwaendeapo watakwambia utafute
milioni tano ili upone kwa kweli ndugu yangu unaitafuta sana hiyo million tano
ili upate unaafu ,matokeo yanaweza kuwa
chanya au hasi, utapona au usipone na usipopona hasara kwako ndugu yangu na mwisho wa yote wao hufurahia mali na
utajiri wao
Ndio hao wamekufa lakini wapo hai wanapumua lakini pia hawapumui
muda firani wa maisha yao wanakunywa pombe na damu ya binadamu na pia wanatoa ahadi kibao za kumtajirisha au
kumnufaisha mwanadamu na matokeo yake mtu hupata hasara ya kimaisha ndio haowalio hai na wafu kwa jina
lingine wanaitwa mizimu
ASANTE
YESU
Asante yesu ndio maneno niyatamkayo moyoni
mwangu siku ya leo asubuhi pamekucha salama mimi ni mzima wa afya tena afya
njema ,afya bora nimeliona tena jua ,nimeona mwanga wa asubuhi moyo umejawa
hamu za kuimba nyimbo mbali mbali
za kidunia nimejikuta nina imba
moyoni mwangu ‘’najisikia
kuweweseka ,najisikia kuweweseka ‘’ najitahidi kuimba taaratibu moyoni
nimejazwa amani na furaha ,sijui kwa nini leo.
Lakini
leo nimekumbuka kwamba nahitaji kubadilika
nahitaji kufanya mapinduzi na mapinduzi
yenyewe yawe yakuni toa kiuchumi,nahitaji kujikwamua kutoka kwenye
umasikini,ufukara na hali mbaya ya kimaisha,ili na mimi niwe miongoni mwa wale
wenye heri maana mawazo yenye heri
yanatoka kwa mungu nani mawazo mema yenye faida
Mungu
anibariki sana
Ninaifanya
juhudi.
Bissmillah wadudi,kukusifu sina budi,
Mola wangu saidi,nitafanya na juhudi,
juhudi na makusudi,heri zilizo jaa
sudi,
ninaifanya juhudi,
uwe wewe shaidi ,kunako kiti cha jadi,
ukinikinga na radi,maadui na maasidi,
nifanye zangu juhudi,hima hima hima,
pole pole ndio mwendo,
iwapo nimekopa mtu,au nimeazima kitu,
kurudisha isiwe katu,kuvirejesha vya
watu,
kwani wema wa kibantu,hauhozi kamwe katu,
kigagulo cha kuazima……….
Nisiwe na roho jitu,lenye sumu kama
chatu,
Nikatengwa nao watu,nikatupiwa misitu,
Bora nifanye juhudi,toka mbeya mpaka
mwanza,
Asha sitakufa moyo!!!!!
Iwapo mehaidi jambo,”promise ‘’yenye
vitendo,
Nisije haribu mambo,siasa napiga
kipondo,
Tafanya si majigambo,ni vitendo vile
vya jando
Sitoweza pata kikumbo heshima langu
kulinda,
Napigana nafsi na umbo,vyote
kuvifanyia lindo,
Kwenye milima mabonde,ntajipiga moyo konde
UKWELI WA MAMBO
Kwa sababu wewe ni binadamu kama
binadamu wengine,imekupasa uyatende yale yaliyo mema na mema hayo yawe ni yale
mema ambayo uyatenda wanadamu wenzako,yawe mema
au yawe matendo ambayo wao huyalilia kila siku.
Ikiwa wewe ulizaliwa ukala,ukanywa,ukaongezeka
ukaupita ujana ukafikia kipindi cha kuyajua yapi yaliyo mema na yapi yasiyo
mema na hivyo ndio itakavyo kua hivyo hivyo ata kwa watoto wako.
Utatamani kua na mwenzi wako katika
maisha,kwa maana hiyo basi utajaliwa kua
na watoto au mtoto na hicho kizazi chako kitatamani kuyatenda yale ambayo wewe
uliye tangulia umeyatenda….labda kinyume chake tuseme kuwa baadhi ya mambo kizazi chako hakijapata kuyatendaa.
Kama ulisoma,uliongea,ulifurahi au
ulijiunga na vikundi mbali mbali vya kiutamaduni au vya kijamii hivyo basi
tambua kua hata mtoto au watoto wako,watafanya
hivyo au wataenda mbali zaidi katika kuyatenda matukio mengi zaidi kulingana na
wakati au kulingana na hayo matukio.
sisi ni wanadamu tuna tama zetu
tunahitaji kuyatenda yale ambayo ni haki kwetu na pia ambayo ndio msingi wa
maisha yetu,tukijinyima tutakua tumezinyima nafasi zetu, na tumenyima muda wetu
pia imetupasa tuwe makini na imara zaidi,kwani dunia inaweza kutupotosha kwa
vitu vidogo vidogo tu ambavyo vinaweza kutuangamiza.
Yours
Elaija elia
TUMEPEWA VYOTE BURE.
Mwenyezi mungu amempatia mwanadamu
maisha yaliyo bora zaidi,kwa jinsi ninavyofikiria kwanza nikiutazama ulimwengu
jinsi ulivyo naweza kusema kua hatuna tulichopungukiwa,vyote tunavyo na vyote
tumepaswa kuvitumia ili tuweze kuenderea na ili viweze kutusaidia,.
Hatuna tusichokua nacho vyote tunavyo
na vinaidi kuongezeka,kila siku inayoitwa siku ya leo,achilia mbali ongezeko la
hivyo vitu pia tunavyo vitu ambavyo
tumepewa lakini hatuvioni au labda tuseme vimejificha sana ulimwenguni.
Lakini mwenyezi mungu ni pendo
pendo,pendo lisilo na mapungufu pendo la dhaati,pendo jema la asubuhi, pendo la
mchana na jioni ni lile pendo lililoleta wagunduzi waganguzi, wenye vipaji na
vipawa,ubunifu,ujuzi maharifa juhudi na elimu isiyo weza kuchuja,hata kama
itachuja japokua ipo lakini pia itaenderea kuwepo milele na milele
Vyote vilivyojificha twaweza vigundua
twaweza vitambua twaweza viona,kwa nguvu na kwa uwezo wake mwenyezi mungu
jalia.ikiwa hatujaviona leo basi tegemezi letu ni kuviona kesho ikiwa sio kesho
basi tutegemee kuviona kesho kutwa au siku yeyote ile,
Daima hatutakiwi kujisifu kuwa tu
wajuzi sana,tukumbuke basi kua ikiwa mungu mwenyezi hajatuonesha sisi basi anao mpango wa kuwaonesha wale au
wajao au vizazi na vizazi dunia imeumbwa na vitu vinavyoonekana au visivyo onekana…..dunia
imeumbwa na kupewa mwanga pamoja na giza kwa kifupi basi tunajua kua mungu
ametupa na wala mungu hajatunyima..
Wasalaam.
Wenu katika bwana
Elaija Elia
MBEGU YA MUNGU
MBEGU ILIYO BORA ZAIDI
NDIYO NGUZO IMARA
Mbegu iliyo bora ndiyo ile mbegu
inayozalisha na kujaza dunia,pasipo hiyo mbegu bora ni vigumu kwa dunia yetu
kujivunia kwamba nafsi yake ya kuongezeka itakua pale pale.
Mbegu hiyo ni mungu na mungu ndiye
mbegu bora zaidi duniani,ndiyo mbegu inayo zalisha dunia ndiyo mbegu ambayo
inajivunia, ndiyo mbegu ambayo pasipo yeye dunia au nafsi haiwezi kuongezeka au kuwepo pale pale.
Daima wanadamu hujisemea wao ndio
walio bora zaidi au wao ndio imara zaidi japokua wamesahau ya kwamba mungu ndiye
bora zaidi aliyewaumba ndiye imara zaidi ominipotent god, god of ominisience,
the powerfull world mighter,world qoncquarol since the beginning of human
creature.
Daima siku zote mwanadamu ujigamba ya
kwamba yeye ni yeye,yeye ni mtawala mfalme atakayeshinda vita vyote yeye ni
nguzo imara,nguzo ya kumpinga adui yake,ingawaje ndio huyo huyo binadamu anaye
weza kujua kua ni macho yake ndiyo yanayo weza kumuokoa au kumuweka katika
hatari Frani. Akizubaa tu kidogo au
akishindwa kupigania nafsi yake basi hatari inaweza kumjia na hapo ndipo
anapoweza kupoteza cheo chake sifa yake au utawala wake,ngazi yake,utawla wake
au na vyote alivyo navyo.
Na jambo la msingi hapa ni kwamba kifo
ndicho kitu kibaya zaidi kinachoweza kummaliza mwanadamu,yeyote Yule mwenye
nyama nafsi,pumzi na damu,lakini pia ikumbukwe kwamba sio hivyo tu mbegu ya
mwenyezi mungu itaenderea kuwepo milele na milele hata kama kifo cha mwanadamu
kimetukia mwenyezi mungu ataenderea kuishi milele na milele.
Assalam allaykum
Na bwana asifiwe
Amen
Ndimi Elaija Elaia
NI VIZURI SANA KUFIKIRIA
Kabla ya kutenda yampasa mtu awe na
fikra za kufanya uamuzi huo,lakini pia
ni vizuri kujua fikra hizo ni negative au posttive,fikra zitakua chanya
pale mtu afikiriaro litakua ni jambo jema lenye kumletea faida,mabadiriko au
hamasa Fulani ya kumletea maendereo,lakini pia fikra zikiwa negative uleta
matokeo negative, yakiwemo yale ya kutaka kudhuru mwili wa binadamu
kutusi,kuiba au jambo lolote lile hovu.
Hebu tuachane na hayo mambo ya
negative and positive thinking,mimi mwenyewe nimejiwa na fikra nyingi kichwani
mwangu,fikra zangu zinaniambia kua mimi sio masikini kama ninavyojidhania.mimi
nimeajiriwa na serikari ni na uwezo wa kuazima benki kiasi cha pesa karibia
milllioni kumi na tano kwa lengo la kufanya biashara ili nijikwamue na madhaifu
ya uchumi na je nikishajikwamua si
nitaondokana na mazaifu yangu kiuchumi, na maisha yangu yatakua positive zaidi
ya kuwaza negative…..
KWA VIJANA
Nikweli isiyo pingika kusema kua
vijana wakiachwa mitaani bila ya kukombolewa huweza kufanya mambo mbali mbali
yasiyo faa katika jamii na suala hili lina wafanya vijana kuonekana kama vituko
au vitu vya ajabu ajabu katika jamii kivipi? Ni hivi wanahitaji kufanya kazi za
kijamii kiuchumi au hata za kiutamaduni bila kusahau hamu yao kisiasa.
Namna gani?
Wameachwa mitaani,wengi wao hawana
elimu,hawana pesa hawana chochote, cha kujivunia, kitu ambacho kitaitwa kitu
cha kuleta maendereo na matokeo yake wamejazana barabarani hawana kazi hawana
kipato hawana mali hawana chochote.na je mipango yao ni hipi kuiba kuvamia au
kupora,kupiga watu kubaka au kufanya matukio mengi ya kutisha na ya aibu yasiyofaa
eti sababu tu wameachwa,hawajitambui na wala hawana kazi za za kuwatoa kimaisha
SIKU ZOTE MNAFQI HAJIKUMBUKI
Mnafqi ana sifa ya kupinga au kupingua,
mnafqi ana sifa ya kukubali au kukataa Na matokeo yake Ni kwamba mnafqi
hajikumbuki Na wala hakumbuki matukio au mawazo yake hujikuta ana paranganyika
mpaka akili zake zinavurugwa.
Mnafqi ana sifa ya kushashia, kuropoka
au kusereleka Na kubwabwajuka na hizo ndizo sifa pekee zinazoweza kumfanya
mnafqi aonekane amepoteza mwelekeo.
Unajua mnafqi ana tabia moja hawezi
kuyatunza yaliyo moyoni mwake,kwani apingapo jambo upande huu pia utetea jambo upande ule ni sawa sawa na kusema yeye
ni shabiq wa samba na pia ni shabiqi wa yanga hana upande mmoja mbadara
anazipepea bender azote mbili hana msimamo na kwa bahati nzuri hadhira humjua
tu kwa sababu ya kuparanganyika kwake.
Basi tukumbuke ya kwamba mnafqi hana
kumbukumbu.
Nisijadiliwe
Nashangaa japokua sitaki kushangaa
sanaa mpaka kufikia hatua ya kugeuka mwendawazimu,mjaa kasoro, kwanini mtu anijadili
anastaha gani,sifa gani,mwelekeo gani, mpaka anijadili.mmh! leo kuna jirani
yangu mmoja kaniambia eti mimi ni mbairi.
Sikua
na hasira ila nilimfikiria vibaya kwani moyo wangu umeniuliza swali au maswali
furani yaendayo,na malezi yangu.nimejiuliza imekuaje mtu huyu asiyejua
nilipotoka ninapokwenda au nilipo anafikia hatua ya kunijadili na baya zaidi
ana nisema kwa moyo wake wote.
Sitaki mtu kama yeye anijadili labda
angekua yeye ni mzazi wangu hapo ndipo napaona ni sawa wazazi wangu ndio
walionifikisha hapa nilipo wao ndio walionilisha,nivalisha,ninywesha nilaza na
kunikuza kimaadili bila kusahau gharama zote za kielimu hawa hawanijadili au
kunisema kimakosa iweje yeye jirani
yangu abwabwatuke.kwani yeye ni nani haswa au ndio uhuru wa kuongea chochote ulivyo…the!teh!teh!(nacheka
mwenyewe)
No comments:
Post a Comment