TAM TAM ZA
ELIA
TUNGO TAMU ZA MAPENZI
1.
ETI
MAPENZI NI NINI
Eti mapenzi
ni nini?,watu tunajiuliza,
Hebu kaa kwa
makini,uanze kujijuza,
Mapenzi yana
thamani, au tuna yapuuza,
Eti mapenzi
ni nini? watu wana jiuliza.
Ukiamua
kupenda, hakuna akuulizaye,
Mazuri
ukiyatenda,mabaya humfikaye,
Ata ukiamua
kwenda, mapenzi huyakutaye,
Eti mapenzi
ni nini? watu wana jiuliza.
Mapenzi ni
kitu gani,chenye kuu maana,
Hata tukiwa
nyumbani, twatafakari kwa asana,
Unafikiri ni
nini, kama sio ni dhamana,
Eti mapenzi
ni nini? watu wana jiuliza.
Mapenzi kama
risasi,huruka tena kwa kasi,
Wala sio
kama fisi,kuzeeka kwa wasi wasi,
Mungu katupa
nafasi yawe pamoja na sisi,
Eti mapenzi
ni nini?,watu wanajiuliza.
Mapenzi kama
siafu ,ambao huwa pamoja,
Wala si kama
sarafu,thamani yake ni moja,
Mapenzi wala
si uchafu,watu kuwaletea vioja,
Eti mapenzi
ni nini?watu wanaulizana.
2. PENZI LA UA CHANUA
Ninakaa
ninawaza,wewe kukufikiria,
Sijambo la
kupuuza,kwa makini zingatia,
Ni vema
kukuhimiza,mapenzini kutulia,
Penzi la ua
chanua, chanua kama maua.
Mapenzi ni
kama ndizi,tamu isiyo kifani,
Naukosa
usingizi,mapenzi ndo yangu fani,
Hata kwa
wale machizi, utulia mapenzini,
Penzi la ua
chanua,chanua kama maua
Mapenzi kama
shubiri,pale usipo yapata,
Kwa hima
utasubiri,bila jawabu kupata,
Utaona kama
dili, pale utapoyapata,
Penzi la ua
chanua, chanua kama maua.
Hata wale
majambazi, utulia mapenzini,
Napatwa na
bumbuwazi,haiingi akilini,
Hutulia kama
ndizi,hasa wawapo chumbani,
Penzi la ua
chanua,chanua kama maua.
Nakwambia
utakonda, kwa kidonda cha moyoni,
Pale
atapokutenda,ulomwifadhi rohoni,
Kamwe tena
hutopenda, bara hata visiwani,
Penzi la ua
chanua chanua kama maua.
3.PENZI LAKE KWELI TAMU
Ni mjuzi
anijuza,ndani hata nje pia,
Na mahaba
anifunza,na kazi nayafanyia,
Kwa kweli
sitopuuza,kwani yana raha pia,
Penzi lake
kweli tamu, ni tamu kama asali.
Muda
unapowadia,kitandani kuingia,
Shuka
huniandalia,jeupe linonukia,
Na mito
yenye maua,ndio naiegemia,
Penzi lake
kweli tamu ni tamu kama asali.
Baridi
nikisikia,yeye hunikumbatia,
Nami
ninafurahia, kifuani kutulia,
Joto
linapowadia, kwa huba hunipepia
Penzi lake
kweli tamu,ni tamu kama asali.
Hunibusu
kitomvuni,hunishika kiunoni,
Hupapasa
mabegani,hunibusu na shavuni,
Mwengine
simtamani,nahisi nipo peponi,
Penzi lake
kweli tamu ni tamu kama asali.
Huruma
unionea,kazi kunisaidia,
Nguo
ananifulia,na pasi kunipigia,
Mimi
ninafurahia,huba namzidishia,
Penzi lake
kweli tamu ni tamu kama asali.
Pale
ninapougua, kwa penzi hunitibia,
Nahafuu
najionia,asante nampatia,
Kwani
namuhamininia,ni dokta alobobea,
Penzi lake
kweli tamu ni tamu kama asali.
Yeye ni
dokta hodari, wa kuyatibu mapenzi,
Atibu kwa
kila hali,na bila kipingamizi,
Ana vifaa
halali,vifanyavyo nyingi kazi,
Penzi lake
kweli tamu ni tamu kama asali.
4 PENZI HALINA MWALIMU WALA YULE SULTAN
penzi si la
kulaumu,ni chaguo la moyoni,
huwezi
kulishutumu, kulipinga akilini,
lisije
kukuhujumu,kukutia matatani,
penzi halina
mwalimu wala Yule sultani.
Penzi latoka
moyoni,kwa kila mwanadamu,
Haulioni
machoni,hili jambo mfahamu,
Litakukakaba
kooni,pia kukunyima hamu,
Penzi halina
mwalimu, wala Yule sultani
Penzi si la
kuchezea,katika hii dunia,
Popote
linatokea,pasipo kutarajia,
Usije
kulichezea,litakapo kufikia,
Penzi halina
mwalimu, wala Yule sultani
Penzi si
kitu adimu,ndani ya moyoni mwetu,
Wala
haliishi hamu ,hii indo haiba yetu,
Pia halina
ugumu, katika wetu utu,
Penzi halina
mwalimu ,wala Yule sultan.
Penzi halina
mwalimu,na wala kwa daktari,
Pia hukutia
hamu,kuishi kwa ufahari,
Ukupeleka
kuzimu,ukilichezea shari,
Penzi halina
mwalimu wala Yule sultani.
Penzi halina
shetani,ni kila viumbe hai,
Uingia
akilini,pasipo kulipa rai,
Na hata
masultani,pia nao wamewahi
Penzi halina
mwalimu,wala Yule sultani.
Penzi halina
heshima,hukugeuza mtumwa,
Hukuweka
hima hima,puta utaja sukumwa,
Na wala
halina bima,wala sio la kupimwa,
Penzi halina
mwalimu,wala Yule sultani.
5PENZI LA UA CHANUA
Kama penzi
ni maua,kheri acha lichanue,
Uliache
kuchanua,na mizizi lichipue,
Mizizi
ikichipua, na tunda lifuatie
Penzi la ua
ni mbegu, tunda katika matawi,
Penzi
la ua si duni,ni mapenzi ya fahari
Haijali
asirani, hata kama huna mali,
Penzi la ua
ni cheni inayo ng’ara shingoni,
Penzi la ua
ni mbegu,tunda katika matawi.
Na kama
penzi ni tunda,kheri liache liliwe,
Lisije
likaja vunda,ukakosa utamuwe,
Uchumi
ulipopanda,ulile wewe mwenyewe,
Penzi la ua
ni mbegu tunda katika matawi.
Penzi laua
huzuni,tena ni lenye huruma,
Halijali
masikini,na kile alichochuma,
Huleta
purukushani,pia na nyingi dhuruma,
Penzi la ua
ni mbegu, tunda katika matawi.
Penzi la ua
ni mbegu, mwenyewe nitazipanda,
Nitayatoa
magugu,na wanyama kuwawinda,
Na yote
miiba sugu,lisije likanishinda,
Penzi la ua
ni mbegu, tunda katika matawi.
Ua
litapochanua,litanitia furaha,
Tabasamu
nitatua,litakalonipa raha,
Pia na
kufurahia,kwa kulishinda karaha
Penzi la ua
ni mbegu,tunda katika matawi.
Na kama
virutubisho,vingi nitajizolea,
Itakua
ukumbusho hukonilikotokea,
Penzi la ua
fundisho nililolitegemea
Penzi la ua ni mbegu,tunda katika matawi.
6.KAMA KWELI WANIPENDA NAOMBA UNIAMBIE
Ukiniona
wacheka, aibu wanionea,
Pia huwa na
mashaka,ukweli kuniambia,
Mimi sio
malaika,kwamba mi nitaotea,
Kama kweli
wanipenda, naomba uniambie.
Maneno
nilisikia,kuwa wewe wanipenda,
Wanithamini
pia na wala hutonitenda,
Kwangu ndo
umefikia,na tena nitakulinda
Kama kweli
wanipenda naomba uniambie.
Nami
nakupenda pia,naogopa kukuambia,
Pale
unapotembea, mimi nguvu huniishia,
Kwako
nimeshakorea,machozi yajitokia,
Kama kweli
wanipenda, naomba uniambie.
Nimeyasikia
mengi, kuhusu wako ujana
Unapendwa
nao wengi,na wana kupenda pia,
Tangu shule
ya msingi,we ndo wangu mvulana,
Kama kweli
wanipenda,naomba uniambie.
Wewe kwangu
mfalme,malikia ndio mie,
Wewe ndio
wangu mume ,kwengine usisogee,
Wewe ndio
mwanaume, wengine ni manguluwe.
Kama kweli
wanipenda naomba uniambie.
Tumia hii
nafasi, wewe kwangu kufunguka,
Presha na
wasi wasi,vinapanda na kushuka,
Unitibu
upesi upesi,hata visivyotibika,
Kama kweli
wanipenda, naomba uniambie.
Naomba
niweke wazi,ili nije pata jua,
Nikuite
laazizi ,nami unite dia,
Niondolie simanzi
,moyo wangu kutulia,
Kama kweli
wanipenda,naomba uniambie.
7.PENZI LETU LIKO POA
Waliosema
siwezi,aibu wajionia,
Namuita
laazizi,nae aniita dia,
Sitopatwa na
mizizi, maneno ya umbea,
Mpenzi
ametulia,penzi letu liko poa.
Nizipata
natabu,wakati wa kumwambia,
Nizipata
sawabu,mabaya kujiachia,
Aniita
mahabubu,nami ninafurahia,
Mpenzi
ametulia,penzi letu liko poa.
Sikwenda kwa
mganga,na hirizi kupatiwa,
Nilimpeleka
tanga,na mambo yakawa sawa,
Azipendaga
karanga sasa mambo ni wawawa,
Mpenzi
ametulia,penzi letu liko poa.
Mahaba
nampatia , nae ayafurahia,
Macho
namregezea,na nguvu humuishia,
Pale ninapotembea,na nguvu humuishia,
Mpenzi
ametulia, penzi letu limepoa.
Kwa mwingine
hatokwenda, ahadi kanipatia,
Kwa yeye
ananipenda, nami nampenda pia,
Kasema
hatonitenda,yeye anihaminia,
Mpenzi
ametulia penzi letu liko poa.
Nampa ya
moto moto,yaliyo anza kupoa,
Nampaka
manukato,ashinda akinukia,
Yeye huniita
toto,kwani ninamdekea,
Mpenzi
ametulia,penzi letu liko poa.
Anaporudi
kazini, huwa amejichokea,
Nampereka
chumbani,kwani ameshanijua,
Akirudi
sebuleni,uchovu ushamwishia.
Mpenzi
ametulia,penzi letu liko poa.
8.UKISHA PENDAGA BOGA.
Nikikumbuka
ninalia,kwani nilimzoea,
Moyoni
ninaumia,ninapomfikiria,
Mawazo
yananijia,vema kuyapotezea,
Ukishalipenda
boga ,ulipende na ua lake.
Ni kweli
alinipenda,na pete kanipatia,
Na shangaa
kanitenda,sababu ajizushia,
Eti mimi
sikumlinda,virusi kumpatia,
Ukishalipenda
boga,ulipende na ua lake.
Ilikua kama
zali,mimi nilipo muambia,
Kutokana na
dalili,nilienda kujipimia,
Majibu ya
dakitali,mimi niliyapokea,
Ukishalipenda
boga,ulipende na ua lake.
Tuliporudi
nyumbani, ugomvi ajiaanzia,
Eti mimi ni
shetani,kaburini ninamtia,
Mara mimi ni
muhuni,akhera aingojea,
Ukishalipenda
boga,ulipende na ua lake.
Ni kweli
alifungasha,nami akanikimbia,
Na moto
aliuwasha,virusi vikaenea,
Aliye
mkaribisha,virusi alimgea,
Ukishalipenda
boga,ulipende na ua lake.
Watu
waliangamia,jamii ukoo pia,
Na kinga
hakutumia,ugonjwa ukaenea,
Kinga(dawa)zimemuishia,kabaki
kujikondea,
Ukishalipenda
boga ulipende na ua lake.
Mimi
najinenepea,na dawa nazitumia,
Masharti
najifatia,dokta alonambia,
Huruma na
muonea,kwani ameshajifia
Ukishlipenda
boga,ulipende na ua lake.
9.PENZI
MPENI RABUKA.
Pendo mpeni
rasula,ndie mwenye haki,
Acheni toa
kafara,wala hiyo sio haki
Pia acheni
papala,mungu yote hayataki
Mapenzi
mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula
Yatende
mambo ya heri,fanya ibada kwa wingi,
Waepuke
mataperi,hawana bora misingi,
Utunze wako
uzuri,ujifunike ushungi,
Mapenzi
mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula.
Saidia
masikini,na wote wasiojiweza,
Wengi
waketishe chini,mazuri kuwaeleza,
Uwapate
kampani,ili kuwaendeleza,
Mapenzi
mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula.
Epuka
purukushani,watu usio wajua,
Utakua
matatani,pasipo kujitambua,
Usije
kuwekwa ndani,macho utayatumbu
Mapenzi
mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula
Tenda yaliyo
ya kheri,rabuka atafurahi,
Ujiepushe na
shari,shetani asikuwahi,
Na pia acha
kejeri,ndugu yangu na kusihi,
Mapenzi
mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula.
Fanya ibada
kwa wingi,yaache mambo mabaya,
Upate bora
msingi,motoni hutoingia,
Uache vuta
mabangi,pia achana na umbea.
Mapenzi
mpeni rabuka,mapenzi mpeni rasula
10.MPENZI NIBEMBELEZE
Mpenzi
nibembeleze,na tena nidekeze,
Usinifanye
nikuwaze,tufurahi na tucheze,
Ukiweza
nikupongeze,ukikosa nikuelekeze,
Mpenzi
nibembeleze,usinifanye niwaze.
Nimezama kwa
mapenzi,sijui kama nitazeeka,
Kujikwamua
wala siwezi,taabani nateseka,
Ingelikua
kama ni dozi,tayari ningeshamaliza,
Mpenzi
nibembeleze usinifanye niwaze.
Nimezama,nimezama,kwenye
kina kirefu,
Nimebaki
natizama,moyoni Napata khofu,
Illahi mola
karima,ndiye ataninahafu,
Mpenzi
nibembelezee ,usinifanye niwaze.
Nibembeleze
kwa zeze,nilale kwa utulivu,
Nipeti peti
nidekeze,ili watu waupate wivu,
Nikuimbie
nawe ucheze,wimbo wa utulivu,
Mpenzi nibembeleze
usinifanye niwaze.
Mapenzi yalo
adhimu,mimi yameniingia,
Simchezo
yalivyo matamu,tena nayafurahia,
Watakao
nilaumu,bado hawajayajua,
Mpenzi
nibembeleze,usinifanye niwaze.
Nikulaze
kifuani kwangu,ulipate langu joto,
Mahaba
nikupe mazito,makubwa si ya kitoto,
Tuachane na
michepuko penzi liwe lenye mvuto,
Mpenzi
nibembeleze,usinifanye niwaze.
Tusiache
kupendana,mapenzi kuyaboresha,
Watakaokuja
kwa fitina kwetu sisi wamechina,
Tusiache
kupendana,mapenzi kuyaboresha,
Mpenzi
niembeleze,usinifanye niwaze.