Monday, May 4, 2015

na sura ya tano je


 SURA YA TANO

PENSLAVIA NA PENIELIA WANA MUHUSUDU BOGA TALENTER

Pamera alikua na dada wawili penielia ambaye ndie kifungua mimba na penslavia  dadaye wa pili baada ya penielia. Ile siku ambayo penslavia alipoonana na boga talenter siku ambayo boga talenter aliwatambulisha dadaze  na wazazi wake kwa boga talenter ndiyo siku ambayo penslavia alijikuta anaachia mdomo wazi kwa kumwona kijana Mwenye mvuto kama boga talenter aliona wivu sana pamera alipomwambia penielia kuwa boga talenter ni mpenzi wake alijisikia tamaa ya ajabu sana  kumwona kijana Mwenye mvuto wa ajabu akipambwa na mdogo wake pamera.

Kadri siku zilivozidi kuyoyoma ndivyo afya ya penslavia ilianza kuzorota vibaya sana,jambo hilo liliwashangaza sana wazazi wake hata hawakujua ni nini kilichomsibu mwanawe penslavia,siku nazo zilivyozidi kwenda mbele ndivyo afya ya penslavia nayo ilizidi  kuyoyoma akawa hawezi kulala,hataki kuoga,hawezi kujisomea kama zamani sana alivyopenda kusoma vitabu  yva noval ndefu akawa hapendi hata kula mara kwa mara alilazwa kwenye dispensary yao ya pale Nyumbani,hakuna mtu aliyejua ni tatizo gani linalomsumbua penslavia.

Lakini siku moja penielia dadaye penislavia na pamera aliona ni heri nusu shari kuliko shari kamili taratibu akamwendea penslavia akamdadisi tatizo gani linamsumbua,mwanzo penslavia hakua  tayari  kumweleza penielia,lakini kadri penielia alivyo mbembeleza penslavia amweleze issue yenyewe ilivyo,ndipo penslavia akaona ni heri amweleze dadake kwani alijua kwamba mficha uchi hazai.

Penslavia akamdodosa dadaye issue nzima mwanzo mpaka mwisho akamwambia amempenda sana boga talenter,kidume cha pamera.penslavia akamwambia penielia amteke kimapenzi boga talenter ili awe wake. Kumbe akufaaye kwa  dhihiki ndie rafiki wa kweli hata penielia tangu siku ile alipomwona boga talenter alimpenda na kumtamania,ila kwa vile yeye ni dada lao akaona ajikaushie tu kama maji ya mtungini,lakini alipounganishwa na ile issue ya penslavia akaona ni muda mwafaka wa  wa kulimiliki lile kinda lililoachwa na mamaye.


Siku iliyofuata akajipeleka Nyumbani kwao boga talenter  kwa vile alipafahamu kwa maana siku zile chache za mazoea yao pamera  aliwaonesha dadaze  mahari anapokaa boga talenter.penielia alipofika alimwona boga talenter anafanya usafi wa nyumba maana tangu pamera amfundishe usafi wa nyumba ile boga alibadirika sana akawa ni mtu msafi nyumba ikangaa na kupendeza,ni yeye mwenyewe boga talenter aliye nunua rangi za nyumba na kupaka nyumba nzima,kila siku alifagia nyumba ile,kila siku alideki nyumba yao, kila siku alipamba na kumwagilia maua maji.kitendo kile kilimfurahisha sana babaye alimsifu kwa juhudi alizo zionesha.

Penielia akajongea na kufika karibu sana na eneo alilokuwepo boga talenter,akamwita boga talenter akajitokeza vizuri pale alipokua boga talenter,alipogundua kuwa si mingine bali ni ni dadaye pamera akamkaribisha pale Nyumbani,penielia akajizoa zoa akakaribishwa vema na baada ya hapo akamkaribisha sebuleni au kama wao waitavyo sitting room, akapewa kinywaji atakacho basi maongezi ya hapa na pale yakashamiri.penielia akamsifu boga kwa ucheshi na jinsi anavyojituma vema kwenye talent show,basi maongezi yao yakaenderea taratibu wakibadilishana ili na lile.

Uzalendo ulipomshinda penielia akamweleza kuwa yeye pamoja na mdogo wake penslavia wametokea kumpenda sana  boga talenter walimsifia sana ,hawawezi kula hawawezi kulala hata kuongea kwao ilikua ni kazi ngumu yote kwa sabababu ya boga talenter.

Hivyo mwana dada huyu akamsihi boga awe mpenzi wao.boga alimshangaa sana penielia akamwambia kinagaubaga kwamba hayupo tayari kutembea na dada pamoja na wadogo zake, yeye ameshapendwa na pamera hivyo basi hayupo tayari kupenda watu watatu kwa wakati mmoja.

Huzuni ilimjaa sana penielia alidhani kwamba labda boga anaweza kulainika kwa maneno yake,lakini kiukweli boga hakua tayari kujihusisha kimapenzi na ndugu wa damu moja,akamwambia kwa kifupi penielia please sister chukua time sijawa mind wala nini.

dah!! penielia alijisikia aibu kama nini maji kasha yamwaga lakini yanakataa kuzoleka, kasha mwambia boga lakini hataki kumsikiliza,penielia akapata wazo kwamba mapenzi sio maneno tu bali mapenzi uambatana na vitendo.

Akarejea Nyumbani  hana hata chembe ya furaha.Hata ivyo penslavia kwa kumtazama dadaye tu akajua kwamba jipu alilolipasua limegonga mwamba.penielia akamwita dadaye penslavia na kumweleza juu ya mpango mpya mpango wa kumnunulia boga talenter vizawadi akiamini kua hilo linaweza kuleta msaada mkubwa kwao.

Kwanza kabisa mabinti wale walinunua gari moja zuri la kifahari, aina ya mercedenz benz,kwa gharama kubwa haswa, maana wale ni mabinti wa tajiri na mkwanja mrefu una wazuzua,kisha wakanunua computer laptop moja kari ya shilingi milioni mbili.wakaifikiria miguu pamoja na kiuno cha boga kilivyo,wakasasambua nguo special kwa ajiri ya boga talenter,pamoja na viatu special vikari,vilivyo gharimu laki tatu tu.hawakusahau kumnunulia camera kwa ajiri ya kutumia kwenye process mbali mbali za kupiga picha.

Warembo walivyokua na haraka haraka iso baraka hao wakanunua na na pikipiki aina  ya baja,pikipiki inayoaminika kuwa na kasi kubwa tena piki piki ya gharama kubwa sana.safariyao ya kwanza ilikua ni kwenda Nyumbani kwa boga talenter walimkuta akipiga kinanda kikikubwa,kinanda  kikubwa kilichokuwepo pale sebulenipake.bila hata kukaribishwa hao wakaingia pale sitting room na kufanywa supprissment ya nguvu kwa kijana boga talenter.

Mabusu mfululizo yalimiminika kwenye uso wa boga talenter pasipo idadi maharumu,kisha wakamtaka ajongee nje ili wakampatie zawadi zake,my god!! Walipofika nje gari ilikua ina ng’ara kama zahabu,penslavia akamwambia boga hii funguo ni maalumu kwa ajiri yako.boga alibaki pale kaduwaa….hana la kusema…. Kisha wote kwa pamoja wakamwambia boga tunakupenda tafadhari tunaomba lifikirie ombi letu….kuwa muwazi kwenye penzi letu….. usihitese mioyo yetu ata kama upo kwenye mahusiano ya kimapenzi na ndugu yetu pamera.boga akiwa bado amepigwa na bumbuwazi asijue nini cha kusema, wale warimbwende wakampungia mkono wa good bye see you tomorrow.

Bado kijana yule alibakia anashangaa tu kama vile kawaona malaika walo mtembelea au kaona kitu cha ajabu sana.akaisogerea ile gari na baada ya kulifungua akakuta piki piki ya gharama,computer laptop,camera,viatu vya gharama pamoja n anguo za gharama.hofu ikamtawala,tetemeko dogo likamvamia mshituko nao ukamwambata,kwani vile vitu vilikua ni vitu vya gharama sana,nguo za gharama,moyo wake ukamwambia laaaulah!!! Nitamwambia nini pamera iwapo atagundua vitu hivi yva gharama.taratibu akalisogeza lile gari upande mwingine wa nyumba yao,alipoimaliza ile shughuri akalejea akalejea sitting room.

Lakini kabla ajafika sitting room, akasikia mlio wa gari ikipiga honi piiiiii…….piiiiiii…….piiiiiii, alipo geuka nyuma  kuangalia ni nani aliyemshitua kutoka kwenye lindi la mawazo,akagundua kumbe si mwingine bali ni kipenzi chake pamera.Tabasamu likamtoka mwanya wake ukajiachia sana,meno yake meupe kama maziwa na pia marefu kama vile ya wazungu wa America   yakangaaa mfano wa nyot nyota,kijana yule Mwenye dimpozi kunako mashavu yake,nywere zake kama vile mtoto chotara   wa  kizungu wa America na wa africa kwa jinsi zilivyo jikunja an kujikunyata kumbe ni mtoto wa kiafrica.

Nyuma ya gari ya pamera kulikuwepo na gari linguine ambalo alikua haliendeshi yeye pamera,ila mtu mtu ambaye boga hakuweza kumfahamu au kumtambua kiurahisi.pamera akashuka ndani ya gari boga akaonesha uchangamfu wake kwa kumkimbilia pamera,wakapigana mabusu mazito mazito ya midomoni, kisha pamera akamwambia boga njoo kipenzi changu,pamera akaitwaa ile funguo aliyokua  mikononi mwa dreva yule kijana  kisha akamwambia boga talenter,

                              Natamani nikuite mume wngu mtarajiwa mpenzi nipe hiyo nafasi please.

Boga akamwambia pamera niite dear,

                             Hata mimi natamani nikuite mke wangu mtarajiwa,nipe nafasi hiyo please.

Wote wakachekeana vicheko vilivyo jaa mapenzi mazito.kisha pamera akamwambia boga

                             Naomba usiniache nitunzie penzi langu.

Boga naye akiwa na furahaa ya kukumbatiwa akamwambia pamera,

                            Sitakuacha my love nitakutunzia penzi lako mpaka siku ya mwisho wa uhai wetu.

Kitambo tu pamera akamwambia boga talenter nataka ni kufanyie supplissment ya nguvu my love,boga akamwambia  pamera supplisment gani hiyo my love. Pamera akaitwaa ile funguo kwa dreva kisha akamwambia boga talenter,

Dear kuanzia leo na wewe utakua na usafiri wako sitaki kuona una teseka au una    hangaika popote pale.

Waoooo!!!! Boga kwa furahaa ya ajabu akamkumbatia pamera,furaha ya ajabu ilimiminika moyoni mwake,hakuamini kama kweli mapenzi yanaweza kumletea utajiri wa haraka namna hiyo,kwanza kapewa  gari na vikorokoro mbali mbali,dakika chache tu akiwa na dadaze pamera,pili kapewa gari zuri na pamera mwenyewe jamani mapenzi haya.

                             mapenzi yenye nguvu, ya kusimamisha dunia,

                           mapenzi yenye nguvu, ya kumtajirisha mwanadamu,

                            mapenzi yenye nguvu, ya kuuondoa umasikini,

                            mapenzi yenye nguvu, ya kumfurahisha mwanadamu

                           

almanusura boga talenter azirai, kwa furaha iliyomiminika moyoni mwake,furaha ya kupendwa,furaha ya mapenzi, furaha ambayo kila  mtu anaililia  na kuitamania.pamera  akamwambia boga talenter baada ya talent show  nitakununulia jumba kubwa la gharama haswa, jumba la ghorofa,ila kwa sasa nitakufungulia account yako mwenyewe,account nitakayo kuwekea pesa na baada ya talent show tuta kwaa pipa twende ulaya tukachape kitabu, huko ndiko tutapanga mipango yetu ya ndoa na harusi bomba ya kifahari.

Kwa mtazamo huu ilidhirisha tu kwamba pamera hakukwenda kujiunga na talent show kwa lengo la kupata mamilioni ya shilingi ila tu  alikua na lengo lake lengo moja kujionesha,kujitapa na kujigamba kuwa amepata umaharufu wa kuonekana na dunia yote iliyo watazama.umaharufu ndicho kitu alicho kifata pale talent show,tofauti na mpenzi wake boga talenter aliye tanguliza mbele  pesa zile za mashindano.

Hii ilijionesha kwa pamera  kwani wazazi wake walijiweza sasa tatizo liko wapi je ni kwenye pesa au umaharufu,jibu unalo wewe mwenyewe msomaji wangu mpendwa.

Bahati iliyomwegamia kijana yule ilikua ni mara nne zaidi ya aliyo tarajia,bahati ilimtafutya naye akaipata lakini jamani sijui ni kwa sababu ya uzuri wake ,mmmmhh!! Labda…lakini…mmmh!!! Ndivyo mapenzi yalivyo,ukishalipenda boga penda na ua lake.


                             mapenzi  yatakutafuta popote ulipo,ewe mwana wa adamu,

                          mapenzi yakikupata,  si yatakukumbata na kukupakata,

                          mapenzi yasipokupata ,hayatokata tama kukutafuta,

                          mapenzi yakikutafuta yatakuitaji   popote ulipo

       

                         mapenzi yakikuona ,yatakulilia ewe kiumbe damu,

                         mapenzi  yatakulilia yatakukimbilia, na kukukumbatia,

                       mapenzi nyatakukimbilia ,na kukukumbatia ndani moyoni,

                       kwani alambaye asali si, atauchonga mzinga wake mapenzi.


                       Ni hay ohayo mapenzi,Mungu kaumba mbingu na dunia ,

                       Alipoumba dunia akaweka, kila kitu ndani ya dunia nzima,

                       Sindege siwanyama si wadudu,si mimea si milima ,

                       Kisha kwa mapendo yake akakiumba chake kiumbe.


                       Kiumbe kilichochukua,ile taswira ya mwenyezi Mungu,

                       Kiumbe kilichopewa ,mamlaka yote na mapenzi.

                       Kikaambiwa ukavitawale,vyote ulivyopewa duniani,

                       Samaki majinindege mitini,mimea ya mashambani.


                       Ni hayo hayo mapenzi,viumbe vya mola vinatamania,

                      Pamera alipomwona boga talenter,moyo ukamtamania,

                      Penislavia alipomwona boga,moyoni mwake akamlilia,

                      Penielia akaona ajitongozeshe ,kwa gharama kumzawadia


Boga safari hii akawa kwenye wakati mgumu sana,kwanin kapendwa na dadaze mtu na mtu nae kampenda,jamani afanye nini alichanganyikiwa sana.babaye alipo wasili akusita kumweleza kinagaubaga,mwanzo mpaka mwisho,hata babaye alishangaa sana bahati kama hii je mtoto wake alale lango wazi,dah!! Babaye akamwambia mwanangu kaa chini fikiria,fanya maamuzi yalo sahii,kwani mshika tatu mbili umpokonyoka,na pia kumbuka kuwa njia mbili zikimshinda fisi uchana msambaa pwaa!!.

Sasa ushari wangu kwako waambie hao warembo dadaze pamera kwamba huna haja        nao,kwani ushapata tunda linalo kuhitaji.


Babaye akamwambia boga usione aibu kumweleza pamera,nia na madhumumuni mabaya walo ya weka dadaze pamera,ili kulivunja na kuligawa gawa penzi lao,


pamera kasha penda boga kapenda na ua lake ,so usimwangushe binti  yule    aliyekupenda kwnza,ahadi yako iwe deni kwako,kwani ni zambi kumwahidi mtu na kushindwa kutimiza ilea hadi ulomwaidia.

   

Jioni ya siku ile boga na babake wakatoka kwenda kupata chakula cha jioni  hotelini.

No comments:

Post a Comment