SURA YA TANO
PENSLAVIA NA PENIELIA WANA
MUHUSUDU BOGA TALENTER
Pamera
alikua na dada wawili penielia ambaye ndie kifungua mimba na penslavia dadaye wa pili baada ya penielia. Ile siku
ambayo penslavia alipoonana na boga talenter siku ambayo boga talenter
aliwatambulisha dadaze na wazazi wake
kwa boga talenter ndiyo siku ambayo penslavia alijikuta anaachia mdomo wazi kwa
kumwona kijana Mwenye mvuto kama boga talenter aliona wivu sana pamera
alipomwambia penielia kuwa boga talenter ni mpenzi wake alijisikia tamaa ya
ajabu sana kumwona kijana Mwenye mvuto
wa ajabu akipambwa na mdogo wake pamera.
Kadri siku
zilivozidi kuyoyoma ndivyo afya ya penslavia ilianza kuzorota vibaya sana,jambo
hilo liliwashangaza sana wazazi wake hata hawakujua ni nini kilichomsibu
mwanawe penslavia,siku nazo zilivyozidi kwenda mbele ndivyo afya ya penslavia
nayo ilizidi kuyoyoma akawa hawezi
kulala,hataki kuoga,hawezi kujisomea kama zamani sana alivyopenda kusoma
vitabu yva noval ndefu akawa hapendi
hata kula mara kwa mara alilazwa kwenye dispensary yao ya pale Nyumbani,hakuna
mtu aliyejua ni tatizo gani linalomsumbua penslavia.
Lakini
siku moja penielia dadaye penislavia na pamera aliona ni heri nusu shari kuliko
shari kamili taratibu akamwendea penslavia akamdadisi tatizo gani
linamsumbua,mwanzo penslavia hakua
tayari kumweleza penielia,lakini
kadri penielia alivyo mbembeleza penslavia amweleze issue yenyewe ilivyo,ndipo
penslavia akaona ni heri amweleze dadake kwani alijua kwamba mficha uchi hazai.
Penslavia
akamdodosa dadaye issue nzima mwanzo mpaka mwisho akamwambia amempenda sana
boga talenter,kidume cha pamera.penslavia akamwambia penielia amteke kimapenzi
boga talenter ili awe wake. Kumbe akufaaye kwa
dhihiki ndie rafiki wa kweli hata penielia tangu siku ile alipomwona
boga talenter alimpenda na kumtamania,ila kwa vile yeye ni dada lao akaona
ajikaushie tu kama maji ya mtungini,lakini alipounganishwa na ile issue ya
penslavia akaona ni muda mwafaka wa wa
kulimiliki lile kinda lililoachwa na mamaye.
Siku
iliyofuata akajipeleka Nyumbani kwao boga talenter kwa vile alipafahamu kwa maana siku zile chache
za mazoea yao pamera aliwaonesha
dadaze mahari anapokaa boga
talenter.penielia alipofika alimwona boga talenter anafanya usafi wa nyumba
maana tangu pamera amfundishe usafi wa nyumba ile boga alibadirika sana akawa
ni mtu msafi nyumba ikangaa na kupendeza,ni yeye mwenyewe boga talenter aliye
nunua rangi za nyumba na kupaka nyumba nzima,kila siku alifagia nyumba ile,kila
siku alideki nyumba yao, kila siku alipamba na kumwagilia maua maji.kitendo
kile kilimfurahisha sana babaye alimsifu kwa juhudi alizo zionesha.
Penielia
akajongea na kufika karibu sana na eneo alilokuwepo boga talenter,akamwita boga
talenter akajitokeza vizuri pale alipokua boga talenter,alipogundua kuwa si
mingine bali ni ni dadaye pamera akamkaribisha pale Nyumbani,penielia akajizoa
zoa akakaribishwa vema na baada ya hapo akamkaribisha sebuleni au kama wao
waitavyo sitting room, akapewa kinywaji atakacho basi maongezi ya hapa na pale
yakashamiri.penielia akamsifu boga kwa ucheshi na jinsi anavyojituma vema
kwenye talent show,basi maongezi yao yakaenderea taratibu wakibadilishana ili
na lile.
Uzalendo
ulipomshinda penielia akamweleza kuwa yeye pamoja na mdogo wake penslavia wametokea
kumpenda sana boga talenter walimsifia
sana ,hawawezi kula hawawezi kulala hata kuongea kwao ilikua ni kazi ngumu yote
kwa sabababu ya boga talenter.
Hivyo
mwana dada huyu akamsihi boga awe mpenzi wao.boga alimshangaa sana penielia
akamwambia kinagaubaga kwamba hayupo tayari kutembea na dada pamoja na wadogo zake,
yeye ameshapendwa na pamera hivyo basi hayupo tayari kupenda watu watatu kwa
wakati mmoja.
Huzuni
ilimjaa sana penielia alidhani kwamba labda boga anaweza kulainika kwa maneno
yake,lakini kiukweli boga hakua tayari kujihusisha kimapenzi na ndugu wa damu
moja,akamwambia kwa kifupi penielia please sister chukua time sijawa mind wala
nini.
dah!!
penielia alijisikia aibu kama nini maji kasha yamwaga lakini yanakataa
kuzoleka, kasha mwambia boga lakini hataki kumsikiliza,penielia akapata wazo
kwamba mapenzi sio maneno tu bali mapenzi uambatana na vitendo.
Akarejea
Nyumbani hana hata chembe ya furaha.Hata
ivyo penslavia kwa kumtazama dadaye tu akajua kwamba jipu alilolipasua
limegonga mwamba.penielia akamwita dadaye penslavia na kumweleza juu ya mpango
mpya mpango wa kumnunulia boga talenter vizawadi akiamini kua hilo linaweza
kuleta msaada mkubwa kwao.
Kwanza
kabisa mabinti wale walinunua gari moja zuri la kifahari, aina ya mercedenz
benz,kwa gharama kubwa haswa, maana wale ni mabinti wa tajiri na mkwanja mrefu
una wazuzua,kisha wakanunua computer laptop moja kari ya shilingi milioni
mbili.wakaifikiria miguu pamoja na kiuno cha boga kilivyo,wakasasambua nguo
special kwa ajiri ya boga talenter,pamoja na viatu special vikari,vilivyo
gharimu laki tatu tu.hawakusahau kumnunulia camera kwa ajiri ya kutumia kwenye
process mbali mbali za kupiga picha.
Warembo walivyokua
na haraka haraka iso baraka hao wakanunua na na pikipiki aina ya baja,pikipiki inayoaminika kuwa na kasi
kubwa tena piki piki ya gharama kubwa sana.safariyao ya kwanza ilikua ni kwenda
Nyumbani kwa boga talenter walimkuta akipiga kinanda kikikubwa,kinanda kikubwa kilichokuwepo pale sebulenipake.bila
hata kukaribishwa hao wakaingia pale sitting room na kufanywa supprissment ya
nguvu kwa kijana boga talenter.
Mabusu
mfululizo yalimiminika kwenye uso wa boga talenter pasipo idadi maharumu,kisha
wakamtaka ajongee nje ili wakampatie zawadi zake,my god!! Walipofika nje gari
ilikua ina ng’ara kama zahabu,penslavia akamwambia boga hii funguo ni maalumu
kwa ajiri yako.boga alibaki pale kaduwaa….hana la kusema…. Kisha wote kwa
pamoja wakamwambia boga tunakupenda tafadhari tunaomba lifikirie ombi
letu….kuwa muwazi kwenye penzi letu….. usihitese mioyo yetu ata kama upo kwenye
mahusiano ya kimapenzi na ndugu yetu pamera.boga akiwa bado amepigwa na
bumbuwazi asijue nini cha kusema, wale warimbwende wakampungia mkono wa good
bye see you tomorrow.
Bado
kijana yule alibakia anashangaa tu kama vile kawaona malaika walo mtembelea au
kaona kitu cha ajabu sana.akaisogerea ile gari na baada ya kulifungua akakuta
piki piki ya gharama,computer laptop,camera,viatu vya gharama pamoja n anguo za
gharama.hofu ikamtawala,tetemeko dogo likamvamia mshituko nao ukamwambata,kwani
vile vitu vilikua ni vitu vya gharama sana,nguo za gharama,moyo wake ukamwambia
laaaulah!!! Nitamwambia nini pamera iwapo atagundua vitu hivi yva
gharama.taratibu akalisogeza lile gari upande mwingine wa nyumba
yao,alipoimaliza ile shughuri akalejea akalejea sitting room.
Lakini
kabla ajafika sitting room, akasikia mlio wa gari ikipiga honi
piiiiii…….piiiiiii…….piiiiiii, alipo geuka nyuma kuangalia ni nani aliyemshitua kutoka kwenye
lindi la mawazo,akagundua kumbe si mwingine bali ni kipenzi chake
pamera.Tabasamu likamtoka mwanya wake ukajiachia sana,meno yake meupe kama
maziwa na pia marefu kama vile ya wazungu wa America yakangaaa mfano wa nyot nyota,kijana yule
Mwenye dimpozi kunako mashavu yake,nywere zake kama vile mtoto chotara wa
kizungu wa America na wa africa kwa jinsi zilivyo jikunja an kujikunyata
kumbe ni mtoto wa kiafrica.
Nyuma ya
gari ya pamera kulikuwepo na gari linguine ambalo alikua haliendeshi yeye
pamera,ila mtu mtu ambaye boga hakuweza kumfahamu au kumtambua kiurahisi.pamera
akashuka ndani ya gari boga akaonesha uchangamfu wake kwa kumkimbilia
pamera,wakapigana mabusu mazito mazito ya midomoni, kisha pamera akamwambia
boga njoo kipenzi changu,pamera akaitwaa ile funguo aliyokua mikononi mwa dreva yule kijana kisha akamwambia boga talenter,
Natamani nikuite
mume wngu mtarajiwa mpenzi nipe hiyo nafasi please.
Boga
akamwambia pamera niite dear,
Hata mimi natamani
nikuite mke wangu mtarajiwa,nipe nafasi hiyo please.
Wote
wakachekeana vicheko vilivyo jaa mapenzi mazito.kisha pamera akamwambia boga
Naomba usiniache
nitunzie penzi langu.
Boga naye
akiwa na furahaa ya kukumbatiwa akamwambia pamera,
Sitakuacha my love
nitakutunzia penzi lako mpaka siku ya mwisho wa uhai wetu.
Kitambo tu
pamera akamwambia boga talenter nataka ni kufanyie supplissment ya nguvu my
love,boga akamwambia pamera supplisment
gani hiyo my love. Pamera akaitwaa ile funguo kwa dreva kisha akamwambia boga
talenter,
Dear kuanzia leo na wewe utakua na usafiri wako sitaki kuona una teseka
au una hangaika popote pale.
Waoooo!!!!
Boga kwa furahaa ya ajabu akamkumbatia pamera,furaha ya ajabu ilimiminika
moyoni mwake,hakuamini kama kweli mapenzi yanaweza kumletea utajiri wa haraka
namna hiyo,kwanza kapewa gari na
vikorokoro mbali mbali,dakika chache tu akiwa na dadaze pamera,pili kapewa gari
zuri na pamera mwenyewe jamani mapenzi haya.
mapenzi yenye
nguvu, ya kusimamisha dunia,
mapenzi yenye nguvu,
ya kumtajirisha mwanadamu,
mapenzi yenye
nguvu, ya kuuondoa umasikini,
mapenzi yenye
nguvu, ya kumfurahisha mwanadamu
almanusura
boga talenter azirai, kwa furaha iliyomiminika moyoni mwake,furaha ya
kupendwa,furaha ya mapenzi, furaha ambayo kila
mtu anaililia na kuitamania.pamera akamwambia boga talenter baada ya talent
show nitakununulia jumba kubwa la
gharama haswa, jumba la ghorofa,ila kwa sasa nitakufungulia account yako
mwenyewe,account nitakayo kuwekea pesa na baada ya talent show tuta kwaa pipa
twende ulaya tukachape kitabu, huko ndiko tutapanga mipango yetu ya ndoa na
harusi bomba ya kifahari.
Kwa
mtazamo huu ilidhirisha tu kwamba pamera hakukwenda kujiunga na talent show kwa
lengo la kupata mamilioni ya shilingi ila tu
alikua na lengo lake lengo moja kujionesha,kujitapa na kujigamba kuwa
amepata umaharufu wa kuonekana na dunia yote iliyo watazama.umaharufu ndicho
kitu alicho kifata pale talent show,tofauti na mpenzi wake boga talenter aliye
tanguliza mbele pesa zile za mashindano.
Hii
ilijionesha kwa pamera kwani wazazi wake
walijiweza sasa tatizo liko wapi je ni kwenye pesa au umaharufu,jibu unalo wewe
mwenyewe msomaji wangu mpendwa.
Bahati
iliyomwegamia kijana yule ilikua ni mara nne zaidi ya aliyo tarajia,bahati
ilimtafutya naye akaipata lakini jamani sijui ni kwa sababu ya uzuri wake
,mmmmhh!! Labda…lakini…mmmh!!! Ndivyo mapenzi yalivyo,ukishalipenda boga penda
na ua lake.
mapenzi yatakutafuta popote ulipo,ewe mwana wa adamu,
mapenzi
yakikupata, si yatakukumbata na
kukupakata,
mapenzi yasipokupata
,hayatokata tama kukutafuta,
mapenzi yakikutafuta
yatakuitaji popote ulipo
mapenzi yakikuona
,yatakulilia ewe kiumbe damu,
mapenzi yatakulilia yatakukimbilia, na kukukumbatia,
mapenzi nyatakukimbilia
,na kukukumbatia ndani moyoni,
kwani alambaye asali si,
atauchonga mzinga wake mapenzi.
Ni hay ohayo
mapenzi,Mungu kaumba mbingu na dunia ,
Alipoumba dunia akaweka,
kila kitu ndani ya dunia nzima,
Sindege siwanyama si wadudu,si mimea si
milima ,
Kisha kwa mapendo yake
akakiumba chake kiumbe.
Kiumbe kilichochukua,ile
taswira ya mwenyezi Mungu,
Kiumbe kilichopewa ,mamlaka yote na mapenzi.
Kikaambiwa
ukavitawale,vyote ulivyopewa duniani,
Samaki majinindege
mitini,mimea ya mashambani.
Ni hayo
hayo mapenzi,viumbe vya mola vinatamania,
Pamera alipomwona boga
talenter,moyo ukamtamania,
Penislavia alipomwona
boga,moyoni mwake akamlilia,
Penielia akaona
ajitongozeshe ,kwa gharama kumzawadia
Boga
safari hii akawa kwenye wakati mgumu sana,kwanin kapendwa na dadaze mtu na mtu
nae kampenda,jamani afanye nini alichanganyikiwa sana.babaye alipo wasili
akusita kumweleza kinagaubaga,mwanzo mpaka mwisho,hata babaye alishangaa sana
bahati kama hii je mtoto wake alale lango wazi,dah!! Babaye akamwambia mwanangu
kaa chini fikiria,fanya maamuzi yalo sahii,kwani mshika tatu mbili
umpokonyoka,na pia kumbuka kuwa njia mbili zikimshinda fisi uchana msambaa
pwaa!!.
Sasa ushari wangu kwako waambie hao warembo dadaze pamera kwamba huna
haja nao,kwani ushapata tunda
linalo kuhitaji.
Babaye
akamwambia boga usione aibu kumweleza pamera,nia na madhumumuni mabaya walo ya
weka dadaze pamera,ili kulivunja na kuligawa gawa penzi lao,
pamera kasha penda boga kapenda na ua lake ,so usimwangushe binti yule aliyekupenda
kwnza,ahadi yako iwe deni kwako,kwani ni zambi kumwahidi mtu na kushindwa
kutimiza ilea hadi ulomwaidia.
Jioni ya
siku ile boga na babake wakatoka kwenda kupata chakula cha jioni hotelini.